Uchaguzi 2020 NEC: Kila Chama cha Siasa kimeruhusiwa kuweka wakala kwenye kila kituo ili kulinda maslahi ya Chama na Wagombea

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Jumla ya Makundi 16 ya waangalizi wa nje wapewa fursa na vibali vya kufuatilia mwenendo wa shughuli ya uchaguzi Tanzania huku asasi za kiraia na taasisi 97 za ndani pia zikipata nafasi hiyo.

Amebainisha hilo Kamisha wa tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) Jaji mstaafu Mary Longway wakati wa mkutanao na wadau wa uchaguzi uliofanyika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeruhusu watazamaji wa ndani na nje,katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambapo imetoa vibali kwa asasi za kiraia na taasisi 97 za ndani na vibali kwa makundi 16 ya watazamaji wa nje” alisema Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi

Anasema “Siku ya uchaguzi vyama vya siasa vimepewa nafasi ya kuweka wakala katika kila kituo cha kupigia kura, wakala atakuwepo kituoni kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa uchaguzi zinazoendelea kituoni pale na kama zinazingatia sheria, kanuni, taratibu na maelekezo yanayotolewa na tume, lengo kubwa ni kulinda maslahi ya Chama na wagombea wake”amesema Jaji mstaafu Mary Longway Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi

Hata hivyo amesema “Tayari vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi, vimepata nakala tepe ya orodha ya wapiga kura waliomo katika orodha ya daftari la kudumu la wapiga kura hii ni kuwawezesha mawakala kutimiza wajibu wa kuhakiki wapiga kura wanaofika kituoni” Jaji mstaafu Mary Longway Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi

Jaji mstaafu Mary Longway amesisitiza kuwa “Tume inasisitiza umuhimu wa vyama vya siasa na wagombea kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kampeni zao, ikwemo kuepuka Lugha za kashfa, maneno ya uchochezi yanayotishia usalama na amani ya Nchi” Jaji mstaafu Mary Longway

Aidha amesema“Wakati tume inaendelea kuratibu, kusimamia na kuendesha uchaguzi huu kwa kutumia sheria za uchaguzi. Vyama vya siasa, wagombea na wananchi wanakumbushwa kuwa katika kipindi hiki sheria nyingine za nchi hazijasimama” Jaji mstaafu Mary Longway Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi

Amewahakikishia wananchi kuwa tume itaendelea kufuata katiba na sheria katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Tume inawahakikishia wananchi kuwa, imejipanga katika kusimamia uchaguzi wa mwaka huu kwa kufuata katiba, sheria, kanuni na miongozo mbali mbali na inaamini kuwa kila mdau akitimiza wajibu wake kwa kufuata taratibu basi watanzania wataweza kupiga kura kwa amani” Jaji mstaafu Mary Longway Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi
 
Maneno laini ila siku ya uchaguzi mawakala wa upinzani ni wanazinguliwa kama kawa kama ilivyokuwa Kinondoni kwenye chaguzi za serekali za mitaa!
 
CCM wahuni sana wale hawaoni hasara kumpa mtu nyumba na million100 ili acheze rafu
 
Hawa ni kuwa nao makini. Mawakala wataenguliwa na kuwekwa mawakala feki. Hivi kama nchi nzima wameunguliwa wagombea wa chadema pekee na hakuna wa ccm aliyeenguliwa hata mmoja bado tunatarajia hii tume ifanye haki?

Hapa hakuna uchaguzi ni uchafuzi tu. Ila ipo siku itafika kwa sababu taratibu naona tunasogea hapo
 
Kuweka mawakala sio suala la 'kuruhusiwa' bali ni utaratibu, au tuseme ilikuwa wazuiliwe!!
Sasa inapotokea vyama fulani kutoa malalamiko kuwa huwa mnaibiwa kura, hawa mawakala huwa hawatekelezi majukumu yao?
 
Back
Top Bottom