NEC: Hakuna sheria wala kanuni yoyote ya uchaguzi wa Rais, wabunge au madiwani inayotaka mawakala wapewe nakala ya kiapo

Ninajiuliza mara mbili mbili ni kipi kinawafanya cdm wasiende mahakamani kwa huyu jamaa anayejichanganya hivi nawokosea jibu. Hapo ndio ninasema Mbowe kachoka, na katibu wake mkuu ndio kichekesho cha karne, ni kweli hatuziamini mahakama, lakini kwa sasa ndio wangalau njia ya kudai haki.

acha kuropoka sasa hivi hakuna mahakama kuna kitengo kidogo cha maamuzi toka lumumba hata walete ushahidi wanamna gani hawawezi shinda ng'o ,kwa hiyo usifikiri CHADEMA vichaa wanajua hilo
 
majaji na mahakimu wakubahatisha tu wengi wao vilaza tu wanapokea maelekezo kutoka lumumba hawana tofauti na nec ila wewe huwezi kuona maana ni kilaza mwenzao
Akili yako umeiacha kwenye soksi za mbowe ,achana na mimi level yako ni too low kwenye mjadala huu,utakua std 4
 
Ninachojua mimi kailima ni kada wa ccm
Tume yenyewe imekaa kiccm
Mara ngapi tumshuhudia watu wakitolewa nje kisa hawana nakala ya viapo
 
Huyo mkuu tume sura,macho yake tu inaonyesha mtumikaji mtiifu,simpendi.
 
Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefafanua kuhusu malalamiko ya kucheleweshwa kwa fomu za kiapo za mawakala wa Chadema kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kinondoni uliofanyika Februari 17 ikisema hakuna sheria wala kanuni inayotaka iwe hivyo.



Mkurugenzi wa uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhan amesema vyama vya siasa vinapaswa kusoma sheria na kanuni zilizopo ili kuweka mikakati itakayovisaidia kufanikisha malengo yao na kushiriki uchaguzi kwa misingi iliyowekwa.

“Hakuna sheria wala kanuni yoyote ya uchaguzi wa Rais, wabunge au madiwani inayotaka mawakala wapewe nakala ya kiapo,” alisema Kailima jana kwa simu.

Alifafanua kuwa kutokana na changamoto inayojitokeza kwa wasimamizi wa kituo kuwatambua mawakala wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi husika, NEC imeandaa utaratibu.

Alisema msimamizi wa kituo anapaswa kuwasiliana na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo husika ili ampe orodha ya wasimamizi hao ili kurahisisha utambuzi.

Kwa kuwa, mara nyingi, msimamizi wa kituo huwa hayupo wakati mawakala hawa wakiapa, Tume hutoa nakala ya kiapo na barua ya utambulisho na msimamizi wa uchaguzi hukubaliana na mawakala hawa muda wa kuzichukua.

Kuhusu madai kwamba msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aaron Kagurumjuli alikiuka sheria kwa kuchelewa kutoa viapo kwa mawakala wa Chadema, Kailima alisema hakuna alichokosea.

Utaratibu unamtaka msimamizi wa kukubaliana na mawakala muda wa kuchukua nakala hizo kabla hazijatumika siku ya uchaguzi.

“Msimamizi hakuchelewesha fomu. Alikubaliana na mawakala wote zitolewe Februari 16, saa 12 jioni na ilikuwa hivyo. Wawakilishi wa vyama vyote waliokuwapo walipata nakala hizo,” alisema Kailima.

Kosa analoliona mkurugenzi huyo ni Chadema kuhitaji fomu hizo kabla ya muda huo haujafika tofauti na vyama vingine kumi na moja vilivyobaki na kukifanya kuwa pekee kilicholalamika.

“Siha walipewa fomu zao saa 12 jioni na hakuna aliyelalamika. Utaratibu ulifuatwa. Uchaguzi tarehe 17 inakuwaje unazitaka fomu saa 10 jioni ya tarehe 16, unataka kuzifanyia nini?” alihoji Kailima.

Alibainisha kwamba kutokana na wingi wa mawakala waliokuwapo, msimamizi wa uchaguzi alitoa viapo hivyo kwa wawakilishi wa mawakala wa vyama husika ambao walipaswa kuvigawa kwa wenzao mchakato ambao alisema Chadema walishiriki pia.

Kutokana na ucheleweshaji wa fomu hizo kama ilivyolalamikiwa na Chadema, wafuasi wa chama hicho wakiongozwa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe waliamua kuongozana baada ya kumaliza mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Buibui hatua ambayo ililifanya Jeshi la Polisi kuwatawanya na katika tukio hilo, mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini, aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala.

Kailima alisema ucheleweshaji unaolalamikiwa haukufanywa na Kagurumjuli, bali mwakilishi wa Chadema aliyechukua viapo hivyo, “Tena kwa kusaini ‘dispatch’ lakini akakawia kuzifikisha nakala hizo kwa wenzake ambao mpaka asubuhi walipotakiwa kuzionyesha hawakuwanazo.”

Licha ya tukio hilo lililotokea siku ya kufunga kampeni, Kailima alizungumzia madai ya kuibwa kisha kurejeshwa kwa sanduku la kura katika Kituo cha Idrissa, Kata ya Magomeni.

Alisema hakuna malalamiko rasmi yaliyowasilishwa kwake ingawa siku hiyo alizungumza na katibu mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji akitaka uchaguzi uahirishwe kutokana na jambo hilo.

Alisema, kwa kutambua matakwa ya sheria katika utekelezaji wa pendekezo la Dk Mashinji, aliona hakuna uwezekano wa kufanya hivyo na akamshauri cha kufanya akinukuu alivyomweleza.

“Kaka (kama wanavyoitana), hatuwezikuahirisha uchaguzi kwa makosa ya kituo kimoja. Mwambie wakala wenu ajaze fomu namba 14 akieleza mapungufu aliyoyaona.”

Hata hivyo, alisema hafahamu kama Chadema walifuata ushauri wake ama la na ripoti ya kituo hicho haikuwa na maelezo ya kushawishi kurudiwa kwa uchaguzi.

Chanzo: Mwananchi

KUKOSEKANA KWA SHERIA NDIO CHANZO CHA VURUGU.....NEC HAIWEZI KUKWEPA,MAANA MKURUGENZI ALITUMIA OMBWE LILIOPO KUTAKA KUMINYA HAKI ZA WATU.
 
Kuna watu wazandika sana,kwamba kaelema yupo sahihi?!kwamba chaguzi hizi tume imezingatia sheria zilizopo mbali ya mapungufu yake?! Uchaguzi huru na wa haki?! Wajinga mmeshikiwa akili na uelewa wenu.
 
Kama viapo siyo lazima kwa nini wengine hasa mawakala wa CCM walipewa? Kama hakuna ulazima wa wakala wa chama kuwa na nakala za hivyo viapo basi asiwepo wa kupewa, wote wasipewe ili ijulikane moja kwamba wakala hapewi kiapo. Hili la kusema hakuna kanuni ya kuwapa mawakala nakala za viapo halafu tunawaona mawakala wa CCM wakiingia vituoni kusimamia uchaguzi huku wakimwonyesha msimamizi wa uchaguzi nakala ya kiapo chao waliyopewa na NEC hiyo hiyo si sawa.

Swali ni kwa nini kama siyo lazima mawakala wale wasio na nakala za viapo hivyo wazuiwe kuingia kwenye chumba cha kupigia kura?
 
Kailima alikuwa kiongozi wa UVCCM Singida,ukijua haya tu utaelewa anamtumikia nani!
Tuna katiba ya hovyo sana ambapo Rais anamteua kada wa CCM kushika nafasi muhimu kama hii!
Katiba mpya yenye NEC huru ni lzm!
 
Hata Sugu aliambiwa alete ushahid kwamba Magu kampiga lissu risasi akashindwa na kufungwa halaf wengine mnaona mnaonewa,kwel laana ya watu haiwez kuwasitiri mwangani

Siamini hata kwenye ndoto kama JPM kahusika katika tukio la Lissu. Lakini kama mimi ningekuwa Sugu ningemwambia jaji ushahidi wangu wanao Scotland Yard au FBI na ningemtaka jaji aniruhusu kuwaleta wafanye uchunguzi wao ili wamkabidhi ushahidi!
 
acha kuropoka sasa hivi hakuna mahakama kuna kitengo kidogo cha maamuzi toka lumumba hata walete ushahidi wanamna gani hawawezi shinda ng'o ,kwa hiyo usifikiri CHADEMA vichaa wanajua hilo

Nashukuru kwa kwa kuniambia naropoka, hiyo ni haki yako. Nimesema hatuziamini mahakama, ila ndio njia pekee iliyopo. Ili watu wakiambiwa waandamane ni lazima tuwe na ushahidi usioacha shaka kwamba hata mahakama nazo hazitoi haki. sasa cdm kutokwenda mahakamani kwa mambo yaliyo wazi hivi, itajengwa propaganda kwamba hawafuati vyombo vya kudai haki.
 
Amekwepa hoja. Huyu jamaa anajifanya yeye anajua sana sheria, anafuata sheria, na kwamba CHADEMA wanavunja sheria, au hawajui sheria ndio maana mambo yako hivyo. Ni kweli kwamba sheria hailazimishi Mawakala wapewe hati za viapo. Lakini wasimamizi wa vituo wanawadai wawe na hati hizo. Mawakala wengi wamekataliwa kuingia vituoni kwa hoja hiyo. na hapo ndipo penye mchezo wenyewe. kuna njama zinaliwa kati ya wasimamizi wa vituo na msimamizi wa uchaguzi, ambaye ndiyo Mkurugenzi. Kimsingi Serikali ya JPM haitaki CHADEMA washiriki chaguzi hizi. wanataka wakae pembeni ili wao wenyewe watengeneze kura zao na ushindi wao wa kuchonga. Polisi wako pale kuhakikisha kwamba hayo yanawezekana, chini ya ma OCD na RPC, na mkuu wa wilaya na mkuu wa Mkoa. wote hao lengo lao ni moja.

JPM anajivuna na kujiona INVINCIBLE, kwa sababu ana majeshi, ana dola, anaona anaweza kufanya chochote atakacho na hakuna wa kumzuia. Anasahau kwamba Historia ina kanuni zake, na huwa inajirudia. Anasahau kwamba Mungu, Bwana wa Majeshi ndiye mtawala wa Ulimwengu wote, anatawala vinavyoonekana na visivyoonekana. kuna siku atasema SASA BASI! Hata hivyo mpaka sasa JPM ameshaingia kwenye historia kama Rais aliyechukiwa sana na raia wake.

Kitendo cha Mange Kimambi kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutengeneza hiyo hofu ya maandamano, ni dalili kwamba hapa nchini kuna nyasi kavu nyingi, na karibu yake kuna dumu la petroli na kuna mtu mwenye kiberiti hayuko mbali.
Tukutane 2604. Hatushindwiiii. Ni lazima tupambanie Uhuru wetu. Tukutane barabarani. Mtapiga risasi tutapiga mayowe.
 
Je mawakala wa ccm hivyo viapo walipewa mapema au hawakuwanavyo kama wa chadema? Na kama wa ccm walikuwa navyo why wa chadema nao waspewe..........kama ilivyo kwa wa ccm.
Kuna watumishi wako madarakani wanadhani wako mbinguni. Hakuna wa kumgusa tena. Kailima anasahau kwamba yeye sio wa kwanza kwenye hiyo nafasi wala hatakuwa wa mwisho
 
Uchaguzi wa siku hizi unaingia chumba cha kupigia kura unaangalia kushoto kulia unabeba boksi unakimbia nalo mpaka miguu inagonga chogo linarudi limejaa kura ukimuliiza polisi anayesimamia anakuambia mi nimeeona vumbi limetimka hapa

Daaah hii comment imenifanya nionekane chizi sio bure nouma san
 
Back
Top Bottom