NEC: Hakuna sheria wala kanuni yoyote ya uchaguzi wa Rais, wabunge au madiwani inayotaka mawakala wapewe nakala ya kiapo

Kailima itafute profile ya Kivuitu wa Kenyaa uisome pamoja na yaliyomkuta baadaye yakuongoze kutambua kuwa maadili ni muhimu kuliko amri unazopokea kutoka kwa mhimili uliojichimbia chini! Kivuitu aliachwa peke yake mahakamani na wale aliowapa ushindi wa bao la mkono! Kama nawe upo tayari kwa hilo sawa, ila aibu ya taifa na taswira ya taifa juu ya demokrasia inachafukia mikononi mwako! Zingatia kanuni na taratibu za ofisi na hayo mengine changanya na zako!
 
Najaribu kumwitisha ruhani wangu anipe mwongozo wa nn nifanye kwa mabwana wale

Nitakujuzeni
Karne hii unategemea maruhani?
Ingekuwa hivyo sefu angeshakua Rais huko zanzibar,yeye sefu alifika mbali kutuambia ruhani kishapanda bado kutaja jina tu mpaka leo kimya sijui ruhani wake kaishia shingoni
 
Ni kweli kabisa,haipo kwa wapinzani tu,bali kwa ccm ipo na ndiyomaana walipewa hati zao mapema kabisa.
 
Nasikia hata ukiwa baunsa vipi; siku ukifumaniwa utaamkia hata watoto wadogo shikamoo.
 
Uchaguzi wa siku hizi unaingia chumba cha kupigia kura unaangalia kushoto kulia unabeba boksi unakimbia nalo mpaka miguu inagonga chogo linarudi limejaa kura ukimuliiza polisi anayesimamia anakuambia mi nimeeona vumbi limetimka hapa
Kula like kwanza
 
Huyu kailima akili yke iko kwenye masaburi yke,aanze kuvaa kijani mana anapenda sana hizo nguo
 
Acha siasa ,nenda mahakamani ,ndiko tafsir na haki hupatikana kikatiba,kama mnangangania media kutafuta huruma badala ya kuutumia muhimili wa mahakama ni kazi bure ,nendeni huko wawadhulumu ndio tuone sasa haja mbadala sio blabla

majaji na mahakimu wakubahatisha tu wengi wao vilaza tu wanapokea maelekezo kutoka lumumba hawana tofauti na nec ila wewe huwezi kuona maana ni kilaza mwenzao
 
Je mawakala wa ccm hivyo viapo walipewa mapema au hawakuwanavyo kama wa chadema? Na kama wa ccm walikuwa navyo why wa chadema nao waspewe..........kama ilivyo kwa wa ccm.

ccm hata wasipopewa hawana shida ya kuvitafuta maana wasimamizi wote wa uchaguzi ni wanachama wao tena wangazi za juu
 
Back
Top Bottom