Ndumo ya Jerry Muro imejaa ngunja

Ndumo ya Jerry Muro imejaa ngunja

Hussein J Mahenga

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2012
Posts
751
Reaction score
656

Nilipotonywa kuwa leo kutakuwa na Press conference ya Jerry Muro, sikutaka kabisa kuikosa. Sikutaka kuikosa kwa sababu sikumjua kabisa kijana mwenzangu huyu pamoja na kuwa anadai Taifa zima linamjua, wallah sikuwahi kabisa kumjua bighairi ya jina lake. Basi nikataka kumjua, Muro ni nani, ukizingatia hivi karibuni alikuja na usemi wa kusema ‘walimu wafurahia sera za CCM’ na kwa kuwa na mimi nipo kwenye career hiyo, basi nikajikuta najawa na shauku kumjua kwa kweli maana andiko lile lilinitia shaka juu ya razini yake.

Kwanza kabla ya yote nimejifunza kuwa, unaweza kuwa umesoma sana, lakini kumbe ni hohehahe na mzigo sana kwa taifa, na hivyo ili uonekane umesoma, basi utaendelea kusifia waliokuzidi ili wakupe promo ujulikane kuwa umesoma, na ndicho anachokifanya kuwa, kumbe alipewa scholarship ya kwenda kusoma Marekani. Nadhani ndiyo maana sahihi aliyokuwa akiirudia mara kwa mara kwamba, ‘ukimuona mbuzi yupo juu ya mti, basi kapandishwa’. Nadhani inatosha kuona kuwa, Jerry ni mbuzi aliye juu ya mti, sasa sitarajii niulizwe kapandishwa na nani.

Bw. Jerry kaita press kwa riboribo kubwa sana kujibu tuhuma za kinachodaiwa kuwa aliandika kitu chenye kiashiria cha kuleta uchochezi, na mimi ni kati ya waliosoma andiko lile ambalo leo anajidai kulifafanua. Labda hapa nipate lau fursa ya kuwakumbusha waandishi kuwa, wasisahau kuliomba andiko lile lililooneshwa na yeye mwenyewe na walisome wajiridhishe, maana ukimuona hata anavyolisoma ni kwa mashaka makubwa kana kwamba kuna kitu kasahau kukiweka sawa, waandishi zingatieni hili. Vilevile kwa vyombo vya dola hasa jeshi la polisi, press ya Muro si ithibati ya kumfanya Muro asiwe na kesi ya kujibu, ni lazima ajibu na apeleke ushahidi mzuri.

Sasa alichokifanya Muro nadhani kwa Kiswahili sahihi ni ‘ubaghamu’ kama si ‘ubahaluli’, maana imefikia hatua hadi anahisi yeye ndiye yeye hata waandishi waliokuwapo pale si kitu. Nitafafanua. Lakini pia, bado hajajibu hoja kabisa, isipokuwa kajikuta ana-attack wengine ambao hata hawamhusu kabisa wala hawajawahi kumzungumza popote. Pamoja na hilo, nadhani sasa Jerry Muro amelisaidia taifa kwenye jambo muhimu kabisa ambalo pia nitalisemea kwenye andiko langu hili, lakini namuona Jerry kama replica ya ‘wasaka tonge’ wa juani, mvuani na kivulini, ambao kwa kawaida ni lazima wawe wanafiki.

Labda nianze na mambo makubwa ambayo ameyasema Bw. Muro ambayo yanatia ukakasi, na kwa kweli nashangaa watanzania wengi wanashindwa kabisa kuyaona. Badala yake wanabaki kuwa ni watu wa kusifia tu pasi na hoja.

Murro anadai, hakuna watu wanaoweza kumtafuta Lema kwa sababu hana kitu cha msingi ambacho kingeweza kuwa ni sababu ya yeye kuuawa. Akaenda mbali zaidi na kusema kuwa, kama watu hawa, actually atakuwa anawajua, wangekuwa na nia ya kumuua, basi wangekuwa wameshamuua zamani kipindi anafanya biashara zile (hajazitaja) na kipindi anasokota rasta. Hii ndiyo hoja anayoweza kuitoa Bw. Muro aliyesoma Marekani, tena kwa scholarship. Labda tujiulize, Muro anataka kutuambia kuwa, hata Nape aliposema kuna watu waliokuwa wanamfuatilia alikuwa hana sababu ya kuuawa? Sitaki kumsemea Lissu. Je, yeye amekuwa ni afisa usalama wa kujua kuwa fulani hawezi kuuawa na fulani anaweza kuuawa? Hivi, ni kijana wa aina gani ambaye anaweza kusema hadharani upuuzi kama ule na kujipambanua kuwa amesoma? Mimi nadhani Bw. Muro ni tatizo si tu kwa yeye peke yake, bali hata anaokaa nao kuwasimulia hadithi hizi.

Lema anazunguka kutwa nzima na flash. Jaman, mimi najiuliza, hivi hii ndiyo elimu tunayoipata? Hivi ni kweli kabisa Bw. Muro amesahau kuwa hata Rais wetu kipenzi anatembea na flash ambayo ndiyo imebeba ushahidi wa kulinda rasilimali zetu watanzania? Au wakati Mhe. Rais anaionesha flash ile yeye alikuwa Marekani anasoma? Sasa kinachonishangaza zaidi, kwenye hoja hii hii akaruka na kudandia kumsifia Mkuu wa Mkoa wa Arusha ati ndiye anayemsaidia kuletea wananchi maendeleo. Wallah ni vichekesho, hili nalo naomba nillieleze kwenye hoja zangu zinazofuata.

Kwamba kumbe kuzunguka na flash kwake yeye ni ujinga mkubwa, tena flash yenye kila aina ya ushahidi wa kile ambacho rais wetu kinamnyima usingizi ‘Rushwa’, bali kuleta tuzo na kuwaonesha watanzania kuwa yeye taifa linamtambua ndizo akili? Binafsi kwanza nimkumbushe tu kwamba, kuna vijana ambao wametambulika, acha kitaifa, kimataifa. Vijana kama kina Benjamini Fernandes, ni watanzania hawa. Lakini tuzo anazoringia, hata kina Diamond, kina Ali Kiba, kina 20%...wanazo kibao, tena zingine ni international awards, ni ujinga yeye ndiye kafanya kuliko huyu anayezunguka na flash.

Anamsifia Bw. Gambo kwa (i) kuhakikisha billion 476 zinapatikana kwa ajili ya maji, (ii) barabara kuanza kujengwa na TANROADS, (iii) ujenzi wa hospitali ya wilaya, (iv) kina mama 500 kunufaika na mikopo nafuu, na; (v) umeme. Jamani, hizi ndizo hoja za Bw. Muro aliyewahi kulisadia taifa kupambana na rushwa kule Bagamoyo, kijana ‘kidume kabisa’ kama anavyojiita na rekodi yake haijawahi kuvunjwa. Jaman, hivi Jerry anajua kuwa Mbuge hatoi fedha mfukoni, isipokuwa serikali ndiyo inayotoa? Na Gambo ni sehemu ya serikali na isitoshe hata yeye hatoi mfukoni. Vilevile, msomi huyu hajui kabisa yote hayo aliyoyaeleza kwenye sifa zake kwa Bw. Gambo kuwa ni haki za msingi za wananchi ambazo zilitakiwa zipatikane miaka 50 iliyopita tena bila kuomba. Kingine, naona anasifia namna kiongozi wa serikali anavyotoa mikopo. Kwamba kwake yeye, kitendo kile ni safi kabisa, lakini hataki kuuliza hata kidogo kuwa kiongozi huyo kapata wapi pesa za kukopesha na kununua mapikipiki? Muro ni kati ya vijana wenye IQ ndogo ila walidondokewa na zali kwenda kusoma nje.

Ameelezea kuwa kuna waraka wa Abibu Mchange, mauaji ya Igunga 2011, kifo cha Chaha Wangwe, Ndesamburo, Mlinzi wa DKT Slaa kutekwa…na makorokocho mengine. Nikatarajhia sasa atakuwa tayari kuishauri serikali yetu iite uchunguzi wa nje ulio huru ili wote hawa waje waumbuliwe, lakini kijana msomi anarudia kuonesha tuzo. Napata shida hata kumuelezea Muro, hivi ni elimu ya aina gani ndugu huyu aliipata?

Jerry Muro amepambana na ufisadi kwa kuandika juu ya mafisadi na hadi taifa likamtambua. Hivi vijana wenzangu, ukiagizwa leo watu waliopambana na rushwa utamfuata Muro? Hebu tuweni serious lau kidogo basi.

Lema aanze na wale madada wawili wanaohusika na mapenzi ya jinsia moja. Walioko kwenye chama chake. Vilevile Lema aanze kwanza kumuangalia kiongozi wake kwa kuzaa na mwanachama wake. Hapa ningependa sana Bw. Muro kwa faida ya watanzania athibitishe (i) kuwa kina dada wale wanafanya mapenzi ya jinsia moja, na (ii) kiongozi wa Lema kuzaa mtot na mwanachama wake. Akishakwisha kuthibitisha hili, kwa uthibitisho bainifu, basi afanye pia jitihada za kupata takwimu na mienendo iliyomo ndani ya chama kingine ambacho bila shaka, pamoja na kuwa anakana kuwa mwanasiasa, ndicho anachokiamini zaidi. Akishamaliza, arudi tena kwenye hoja ya msingi sasa, je kwa nini anaandika mambo ya uchochezi, na si rovyorovyo zingine.

Nadhani hata kama Muro ni shashimamishi, hapaswi kupuuzwa. Binafsi nimekaa siku nyingi sana nikijaribu kutaka kuwa na shani juu ya nani hasa ndiye Bashite, kumbe watanzania, Bashite ni Bw. Makonda, mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam. Nimeshtushwa aliposema kwamba wapinzani wamekazana tu na Makonda, eti oh Bashite, Bashite, Bashite…ala! Kumbe Bashite ndiye Makonda. Binafsi kwa hili nampa heko ndugu yangu, mtanzania mwenzangu na kijana mwenzangu, kijana msomi huyu, na hata kama atapewa tuzo kwa hili, nadhani ni halali.

Maneno kadindi yenye sheshe ndani yake hayana mashiko kabisa kwa mujibu wa tuhuma alizonazo. Nafikiri jeshi la polisi sasa lina sehemu nzuri kabisa ya kuanza kufuatilia matukio juu ya watu wasiojulikana, yawezekana Bw. Muro atakuwa anawafahamu wengi tu. Hiyo aliyoonesha kwenye karatasi akisema kuwa ndiye Makala yake orijinali itazamwe upya na ahojiwe kwa weledi wa kiintelijensia na hakika watapata mwanzo mzuri.
 
Sijawahi shawishika kuwa Murro ni mwandishi,japo kasomea uandishi! Elimu so makaratasi ya tuzo! Ni maarifa uliyopata mafunzoni na unavyoyatumia. Murro ni kapi!

Tangu akiwa msemaji( mropokaji nadhani sahihi zaidi),sikuwahi msikia akitoa taarifa yenye "akili".Waliomfungia walikuwa sahihi. Nitashangaa kama TFF wasio na taaluma ya upelelezi waliona kasoro wakachukua, hatua sembuse polisi na Sirro wanaojinasibu?
 
Mkuu, hiki kichakula kimetumwa na wakubwa kuja huku kubwata, pengine kilivyomaliza press kilienda kuripoti kwa kubwa lao mr bichwa.
 
Polisi haina ubavu wa kumhoji au kumchunguza Muro kwani wanajua fika kina nani wako nyuma yake....
Ugumu wa Organized crime kama hizi wanazofanyiwa wapinzani ni vigumu kwa polisi kufuatilia kwani master plan wake wanamjua na ndiye aloshika mpini....
Kwavile wao bado wanapenda ajira yao watabaki kubabaisha...japo kila mwenye akili anajua " nani ni wahusika" na sasa wanamtumia Jerry Muro ktk kutapatapa !!!
 
Police nao waonyeshe uhodari wao hawawezi kuacha udambwidambwi wa wazi hivi kuhusu watu wasiojulikana ukapita kirahisi tuu Jerry muro ahojiwe pls
 
Samahani, huyu Muro ndio yule ambaye akiwa bar na wadada anapenda kuongelea na kusifia ulaji wa tigo??? Ndiyo huyu rafiki yake Le mutuzz na makondakta???
Kama ni yeye basi hana credibility hata ya kumkemea James delicious.

Anyways, hivi kajaribu kujibu hoja za chadema kama nani vile??? Au ndo makamu slowslow??
 
Mmesahau huyo kijana hana kazi, alikua analenga uteuzi bahati mbaya hayumo. Huyu kijana alitaka kiki wikend nzima imuongelee, baht mbaya magu hapangiwi, kamwaga baraza leoleo
 
Huyo kijana analipwa nadhani kwa kazi hiyo ambayo inamuunganisha kwenye uadui na kundi kubwa la watu pasi yeye kujua
 
Back
Top Bottom