NDUMBARO VS MALINZI: Sababu za ugomvi wao zabainika

mhalisi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
1,181
Reaction score
322
Dar es Salaam.

Mwanasheria Damas Ndumbaro ametoboa siri ya ugomvi wake na rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuwa ni basi la Taifa Stars na urais.

"Kuna mambo mengi yamejificha nyuma ya mgogoro huu, lakini nadhani chuki yangu na Malinzi imechangiwa na mambo kadhaa," alisema Ndumbaro katika mazungumzo maalumu na gazeti hili.

"Sababu ya kwanza ni pale lilipokamatwa basi la TFF kwa deni ambalo nadhani linazidi Sh150 milioni. Malinzi alimpigia simu Silas Mwakibinga (aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi), akimwagiza kwamba bodi itoe pesa hizo kwa ajili ya kugomboa basi," alisema Ndumbaro.

"Mimi niligoma kwa sababu ni mmoja kati ya watu waliokuwa wanatia saini katika utoaji wa fedha hizo. Fedha zilizokuwapo pale ni za Yanga. Unajua mpaka leo Yanga hawajafika kuchukua pesa zao ambazo zipo katika udhamini wa Azam TV na sisi bado tumewawekea.

Nikamuuliza Mwakibinga, hawa Yanga kuna mtu mmoja anaweka ngumu pale, lakini vipi kama akiondoka ghafla leo? Kesho asubuhi watakuja kuzichukua, tutazipata wapi? Nikagoma.

"Mwakibinga alimweleza Malinzi azungumze nami, lakini akagoma, akasema ‘mimi siwezi kuzungumza na Ndumbaro.'"

Ndumbaro aliongeza kuwa sababu ya pili ilikuwa ni pale alipokataa wakaguzi waliochaguliwa na Malinzi wasiikague Bodi wa Ligi.

"Nadhani wakati anaanza kututafuta sisi (Bodi ya Ligi) akiamini kuwa labda tuna fedha nyingi, akatuma wakaguzi wake waje kutukagua. Aliituma Kampuni ya Price Waterhouse Coopers. Wakaja jamaa fulani pale wawili ni Wahaya (kabila la Malinzi), nikajua madhumuni yao yalikuwa nini," alisema Ndumbaro.

"Lakini, kwa mujibu wa katiba ya TFF, wakaguzi pekee wa TFF ndio wanaoruhusiwa kutukagua sisi, Bodi ya Ligi. Hapo Malinzi alikuwa anakaribia kuvunja katiba. Nikaona bora nimwokoe kwa kugomea wakaguzi wake."

Baada ya sababu hizo mbili, Ndumbaro anaamini kuwa sababu ya tatu ambayo ni kubwa zaidi ambayo pia ni ya msingi ni jinsi ambavyo Malinzi amedanganywa na wapambe wake kuwa anautaka urais katika uchaguzi ujao.

"Wapambe wake (Malinzi) wamemdanganya kuwa Friend's of Simba wanamwandaa Ndumbaro kuwa rais mpya wa TFF mara Malinzi atakapomaliza kipindi chake cha kwanza, kitu ambacho siyo kweli.

"Napenda nikutamkie, mimi sina ndoto hizo, sina mpango huo kabisa na Malinzi aelewe hivyo. Kifungo chake cha miaka saba kwangu kimelenga kuhakikisha kuwa anamaliza vipindi vyake vyote viwili kwa amani kabisa," alisema Ndumbaro."

Mwananchi

Kifungo cha miaka saba kimekaa kimkakati, huu udikteta Malinzi anajidanganya tu, father of all diktetas Mr Muhidin Ndolanga alitoka itakuwa yeye Malinzi!!
 
Huyu Ndumbaro kwa taratibu za mpira anatakiwa awe amefungiwa maisha, TFF inamlea tu Blatter watu kama hawa tungekuwa tumewasahau, kaleta migogoro Simba sasa anaona viongozi aliowaingiza kwa nguvu karibu washushe timu daraja sasa amegeukia mpira uharibike nchi nzima.tumuogope kama ukoma
 
Ndumbaro ana yake machafu mengi sana kayafanya kwenye soka letu la tanzania tangu awe wakala mpala sasa.
hayo mambo yake ya nyuma ya pazi hayo nayo yakitajwa pia itajulikana mbivu na mbichi maana anajiona muda wote yeye anaonewa tu.
 
​Mpira wetu wenyewe hauna kiwango cha kutia matumaini, lakini zengwe miaka na miaka.
 
kwa jinsi nilivyokuwa namtegemea malinzi tangu ashinde kwa rushwa ya hela ndefu sana wkati ule wa bifu, sina hata sababu ya kumtetea kwasababu tangu aingie ndio soka la tz linazidi kushuka. bora hata Tenga. akina Tenga walifanya jitihada sana kumzuia huyu promota wa ngumi asiingie kuwa rais kwasababu walimjua lakini issue ilipenyezwa hadi bungeni, jamaa akachukua urais, lakini hakuna hata anachofanya. labda anarudisha kwanza garama alizotumia. hivi mbona bora Tenga mara mia nane? hivi malinzi amefanya nini tangu aingine madarakani? mbona ametuangusha sana? ndumbaro inawezekana akawa na sababu pamoja na kwamba yeye ndumbaro pia kama ana machafu yake yaanikeni hapa ili naye tumchambe.
 
Huyu NDUMBA vipi jamani!! mbona siku zote yeye amekuwa mtu wa kulalamika kuwa anaonewa!!!!
 
wana jamii ngoja niwatoe tongotongo juu ya jambo hili.
Kwanza mwogopeni sana ndumbaro huyu jamaa ni hatari sana

kwa soka la Tanzania
kwanza mimi naona MALINZI anamlea maana kwa mujibu wa kanuni za fifa mtu yeyote yule akiwa wakala wa fifa haruhusiwi kujishughulisha na masuala ya uongozi wa mpira na taasisi zake wala kuwa kiongozi kwewnye association yoyote ya tff.
amemwacha kama mjumbe wa bodi ya ligi,
amemwacha kama mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya simba
hizo sababu mbili tu zilitosha kumtosa toka kwenye system ya mpira,

kubwa zaidi amezuiwa kuwa wakala wa wachezaji na uongozi huu wa malinzi kutokana na sababu nilizozieleza hapo juu na kusababisha kitumbua chake kuingiwa na mchanga hivyo basi ndo maana anatapatapa.

Nakama sio masilahi binafsi kelele za nini ndo maana tff wamenyamaza kimya wanaona anapiga kelele.
ninayo mengi sana ila kwa leo yanatosha na ajiandae baadhi ya mikoa inajiandaa kumpeleka kwenye kamati ya maadili ikiomba afungiwe maisha hili linatokana na kutaka kuipindui serikali iliopo madalakani kwa kukusnya sahihi za wajumbe wa mkutano mkuu ili kumfujuza rais aliyechaguliwa kuiongoza tff kwa miaka minne.
 
Ndugu yangu huyu mtu ni hatari sana, nashukuru Ikizu umetutoa Tongotongo, huyu Ndumbaru alijilipa dola 10,000 kwenda kozi ya wiki moja tu Nairobi.amepewa nafasi ya kutia saini akaunti ya bodi kinyemela, kwani idhini ilipaswa kutoka ndani ya kamati ya utendaji ya TFF kwa mujibu wa utaratibu ndo maana unaona kachanganyikiwa baada ya kuona dili zao za kuibia bodi zimeshtukiwa.mwenzake kakimbia mapema kwani ana akili, huyu Ndumbarobpovu linamtoka kwa kuwa kazoea migogoro.tukumbuke wakati yupo TAZARA alikuwa anawatuma wafanyakazi washtaki na kukuza migogoro kisha anawapa dili jamaa zake kupiga pesa.Hana sehemu ya kupiga dili ndo maana povu linamtoka.
 
wana jamii ngoja niwatoe tongotongo juu ya jambo hili.
Kwanza mwogopeni sana ndumbaro huyu jamaa ni hatari sana

kwa soka la Tanzania
kwanza mimi naona MALINZI anamlea maana kwa mujibu wa kanuni za fifa mtu yeyote yule akiwa wakala wa fifa haruhusiwi kujishughulisha na masuala ya uongozi wa mpira na taasisi zake wala kuwa kiongozi kwewnye association yoyote ya tff.
amemwacha kama mjumbe wa bodi ya ligi,
amemwacha kama mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya simba
hizo sababu mbili tu zilitosha kumtosa toka kwenye system ya mpira,

kubwa zaidi amezuiwa kuwa wakala wa wachezaji na uongozi huu wa malinzi kutokana na sababu nilizozieleza hapo juu na kusababisha kitumbua chake kuingiwa na mchanga hivyo basi ndo maana anatapatapa.

Nakama sio masilahi binafsi kelele za nini ndo maana tff wamenyamaza kimya wanaona anapiga kelele.
ninayo mengi sana ila kwa leo yanatosha na ajiandae baadhi ya mikoa inajiandaa kumpeleka kwenye kamati ya maadili ikiomba afungiwe maisha hili linatokana na kutaka kuipindui serikali iliopo madalakani kwa kukusnya sahihi za wajumbe wa mkutano mkuu ili kumfujuza rais aliyechaguliwa kuiongoza tff kwa miaka minne.

Nyie mnaokuja kumtetea Malinzi jipangeni kwanza,Ndumbaro kwa sasa sio wakala wa FIFA alishaacha uwakala.Mje kupangua hoja za ubadhirifu zinazohusu ubadhirifu hapo TFF.Malinzi alitoa ahadi nyingi sana lakini tangu ameingia hakuna matumaini kabisa
 
Kuacha uwakala jambo jingine, na kudai pesa akijifanya ni wakala huo ni wizi, kuhusu ubadhirifu kika kitu kinajieleza chenyewe amediriki hata kusema TFF imenunua magari hewa, wakati yapo.Kuhusu ubadhilifu anaoudai ni mkataba wa TBL, hivi kuwe na ubadhilifu na TBL na mkataba uendelee tu?acheni porojo TFF ni taasisi siyo mali ya mtu mmoja kuna viongozi lukuki wa kuchaguliwa, kuna waajiliwa makini.Hayo yanayozungumzwa ni poroja za vijiwe vya kahawa na wachumia tumbo.Hivi kuna mtu mpuuzi anaweza iba hela za taasisi kwa kujilipa kirahisi hivyo kama tunavyotaka kuaminishwa huo ni upuuzi na Ndumbaro anajua ana evidence, atapopelekwa maadili ni maisha.Tunachomuongelea yeye ni kujifanya alikuwa wakala wa mechi wakati hajawahi kuwa hata siku moja, yeye alikuwa wakala wa wachezaji, sasa huo utapeli tena wa maandishi aliyoandika mwenyewe wa kujifanya wakala aliyewaleta Bafana bafana ndiyo nauzungumzia.
 
kwa soka la Tanzania
kwanza mimi naona MALINZI anamlea maana kwa mujibu wa kanuni za fifa mtu yeyote yule akiwa wakala wa fifa haruhusiwi kujishughulisha na masuala ya uongozi wa mpira na taasisi zake wala kuwa kiongozi kwewnye association yoyote ya tff.
amemwacha kama mjumbe wa bodi ya ligi,
amemwacha kama mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya simba
hizo sababu mbili tu zilitosha kumtosa toka kwenye system ya mpira,

kubwa zaidi amezuiwa kuwa wakala wa wachezaji na uongozi huu wa malinzi kutokana na sababu nilizozieleza hapo juu na kusababisha kitumbua chake kuingiwa na mchanga hivyo basi ndo maana anatapatapa.

Nakama sio masilahi binafsi kelele za nini ndo maana tff wamenyamaza kimya wanaona anapiga kelele.
ninayo mengi sana ila kwa leo yanatosha na ajiandae baadhi ya mikoa inajiandaa kumpeleka kwenye kamati ya maadili ikiomba afungiwe maisha hili linatokana na kutaka kuipindui serikali iliopo madalakani kwa kukusnya sahihi za wajumbe wa mkutano mkuu ili kumfujuza rais aliyechaguliwa kuiongoza tff kwa miaka minne.

Binafsi sijui kanuni za FIFA kuhusu hayo maswala zikoje, lakini bado sikubaliani hili swala kulifanya ni la kisiasa katika vita ya Ndumbaro na Malinzi.

Hapa Malinzi na TFF wanatakiwa kujibu hizi hoja za ubadhilifu wa pesa. Tena naweza kusema tunashukuru huu ugomvi wao, kwani umetupa picha kubwa mno ya ubadhilifu mkubwa saana.

Mangeni ya ugomvi wao, hayanihusu kama mwananchi ripoti ya wakaguzi imebainisha haya madudu sasa kwa nini tunataka kuyafumbia yasijibiwe?
 
Hiyo ripoti ya wakaguzi ya mdomoni kwa nini wasiichapishe gazetini au wailete jamii forum, hivi unajua taratibu za ukaguzi ndugu yangu, wakaguzi wakikukagua kama kuna mapungufu wanakuambia kisha wanakupa muda wa kuwasilisha documents ili kuthibitisha kuhusu matumizi yako.hivi TBL wangekuta madudu yote hayo wangeendelea na mkataba, acheni uzushi, Ndoa ya TBL na TFF ipo imara kuliko maelezo.Mnadanganyana mtaani, Malinzi hawezi kujibu hoja za mtaan kama hizi yeye anawajibika kwa wajumbe wa mkutano mkuu huko ndiko anapaswa kujibu hoja siyo kwa mtu kama Ndumbaro, ambaye kaingizwa kichwa kichwa kwa kuongopewa, yeye atapelekwa maadili ataombwa athibitishe haya, asipothibitisha adhabu yake ni kutojihusisha na soka maisha, mtalia eeeh ila ndiyo itakuwa imekula kwake, kuna mtu anampotosha sana hajui ukweli lakini yeye anamuamini sana, kuna wakati aliropoka kuwa serikali inaibiwa kodi kwenye fomu ya mgao, alipoonyeshwa fomu ya mgao Ilivyo alipagawa na akakiri halikuwa hajaiona ila aliambiwa vibaya, sasa Yombayomba mtetee humu lakini muda si mrefu ataitwa na kuombwa uthibitisho, Saleh Ally hatakuwepo wala Yombayomba nakuhakikishia mtapagawa kwa sababu mnaamini sana uongo wake.
 
wana jamii ngoja niwatoe tongotongo juu ya jambo hili.
Kwanza mwogopeni sana ndumbaro huyu jamaa ni hatari sana

kwa soka la Tanzania
kwanza mimi naona MALINZI anamlea maana kwa mujibu wa kanuni za fifa mtu yeyote yule akiwa wakala wa fifa haruhusiwi kujishughulisha na masuala ya uongozi wa mpira na taasisi zake wala kuwa kiongozi kwewnye association yoyote ya tff.
amemwacha kama mjumbe wa bodi ya ligi,
amemwacha kama mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya simba
hizo sababu mbili tu zilitosha kumtosa toka kwenye system ya mpira,

kubwa zaidi amezuiwa kuwa wakala wa wachezaji na uongozi huu wa malinzi kutokana na sababu nilizozieleza hapo juu na kusababisha kitumbua chake kuingiwa na mchanga hivyo basi ndo maana anatapatapa.

Nakama sio masilahi binafsi kelele za nini ndo maana tff wamenyamaza kimya wanaona anapiga kelele.
ninayo mengi sana ila kwa leo yanatosha na ajiandae baadhi ya mikoa inajiandaa kumpeleka kwenye kamati ya maadili ikiomba afungiwe maisha hili linatokana na kutaka kuipindui serikali iliopo madalakani kwa kukusnya sahihi za wajumbe wa mkutano mkuu ili kumfujuza rais aliyechaguliwa kuiongoza tff kwa miaka minne.

Jinsi ulivyoanza kwa ahadi ya kututoa tongotongo nikajua unakuja na hoja.

Hebu tuache ushabiki, Dr Ndumbaro sasa sio wakala wa wachezaji wa FIFA, so, anaweza kuwa kiongozi.

Je Malinzi alihitaji hizo pesa kweli kutaka kukombolea mabasi au hakuhitaji na kama ndio sheria inamruhusu na Ndumbaro alifanya kosa kukataa?

Je ni kweli aliwatuma External Auditors kinyume cha katiba kukagua bodi ya ligi na alitaka kuivunja hiyo bodi?

Hoja yangu hapo ni kuwaomba mjenge hoja haswa mnaomtetea Malinzi maana msisahau hata TFF wenyewe wanatuchanganya, kwanini walikanusha kupokea rufaa ya Ndumbaro na wakakubali baada ya yeye kuitoa hadharani?.
 
Huyu Ndumbaro kwa taratibu za mpira anatakiwa awe amefungiwa maisha, TFF inamlea tu Blatter watu kama hawa tungekuwa tumewasahau, kaleta migogoro Simba sasa anaona viongozi aliowaingiza kwa nguvu karibu washushe timu daraja sasa amegeukia mpira uharibike nchi nzima.tumuogope kama ukoma

Binadamu huwa tunasahau haraka,

Tumeshasahau Malinzi alivyopambana pale alivyokatwa asigombee urais wa TFF kwa kukosa sifa? hadi FIFA wakasimamisha Uchaguzi wa TFF tena chupuchupu ilikuwa tufungiwe na FIFA maana serikali iliingilia kati? Pale Malinzi alikuwa anaupinga uongozi wa Tenga, lakini leo Malinzi hamtaki akosolewe? Who is he?

Malinzi ndiye aliyetaka kuivuruga Simba kwenye uchaguzi na sio Dr Ndumbaro nadhani pia hilo tunasahau.
 
Back
Top Bottom