Tatizo la Simba linaanzia hapa

Tatizo la Simba linaanzia hapa

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
18,038
Reaction score
25,668
Nilikuwa namtetea sana Mangungu kwamba hana uwezo sababu katiba haimpi nguvu.
Baada ya marekebisho ya katiba amekaa kimya na kuqcha bodi ambayo haitambuliki iendelee kufanya maamuzi ikiwemo kuingia mkataba wa kutengeneza kadi wakati swala la kadi za wanachama linatakiwa kuwa chini yake.
Inawezeka wako kimya wakisubiri ligi iishe ndio waanze utekelezaji.
Leo nimebahatika kusikia mahojiano kati yake na hizi tv za mtandaoni ndio nimejua tatizo kubwa ni yeye.
Kila anapoongea anabaki kuisifia TFF na bodi ya ligi, anaulizwa kuhusu uwanja anasema wqnategemea kujenga uwanja wa kuchukua watu 8000, anapoulizwa kama idadi hiyo inaendana na mashabiki wa Simba anajibu kuna uwanja wa Mkapa unachukua watu elfu 60 pia TFF wanajenga uwanja utakaochukua watazamaji elfu 30 hivyo hamna haja ya Simba kujenga uwanja mkubwa.
Huyu amezidiwa maono hata na mzee Dalali darasa la nne la zamani, vilabu vikubwa kama Barcelona na Madrid wamepanua viwqnja vyao ili waingize mapato zaidi yeye anawaza Simba kucheza kwenye viwanja vya serikali na Tff au labda kwenda kucheza Zanzibar kuifurahisha serikali.
 
Watafuteni yanga baada ya miaka miwili muone hilo balaa, utajengwa uwanja huo haujawah kutokea tanzania

Meja samuyo
 
1778905225487.png

Nionyeshe Kenneth Mkapa na Godwin Aswile kwenye picha hiyo.
 
Sisi mashabiki wa simba tuna imani na mwenyekiti wetu Mangungu. Mwacheni afurahie mafanikio yake. Uwanja wa watu elfu 8 unatosha sanaa! Nani kama Mangungu? Hakunaaa!
 
Sasa mtu ni ccm na tena ameshakuwa mbunge unategemea atakuwa na akili timamu zaidi ya kusifia sifia tu
 
Back
Top Bottom