Yaani kuna mdada niliwahi pishana naye sehemu kama mara 2 haraka haraka. Siku nyingine nikatafuta namba yake nikaipata. Huyo dada alinivutia nami nikasema ngoja nione kama swaga zangu zinalipa. Kwa hiyo nikawa nawasiliana naye vizuri bila shida. Tukapanga tukutane uso kwa uso week hii.
Leo nimempigia simu tukaongea kama saa nzima. Sehemu ya maongezi ilikuwa hivi:
Mimi: Mambo? Habari za jioni?
Yeye: Poa, nzuri tu, nipo huku nilikopanga, ila Ijumaa nitaenda home kuwasalimia. Na ijumaa ile nyingine naenda kwangu.
Mimi: Kwako wapi? Umeolewa?
Yeye: Hapana sijaolewa, ni Mbezi, nimejenga huko. Yaani sikutaka kabisa kukaa kwa watu, home wala kupanga, wakati nasoma nilisema nikimaliza tu masomo yangu ya sekondari lazima nijenge na kuhamia kwangu. Nina nyumba mbili, nyingine ipo Kigamboni.
Mimi: Hongera, wengine hata kiwanja bado hatuna. Umewezaje kujenga huku ukiwa bado mwanafunzi, tena wa sekondari?
Yeye: Mmmmh, wewe mbona mtu wa ajabu hujajenga wala huna kiwanja! Wakati nipo sekondari nilikuwa natumiwa pocket money, kwa hiyo nimesave ndio maana unaona nimejenga.
Mimi: Taratibu nitaenda hivyohivyo dada. Au wazazi wamekupa? Wamekujengea?
Yeye: Wala, ni kwa kusave pocket money tu, kwani hata kazi bado sina. Kwanza wewe mie tukikutana ndani ya dakika nitajua kila kitu kuhusu tabia yako, hicho ni kipawa nilicho nacho, wala sitabahatisha!
Mimi: Kunijua kwa kuonana tu mara ya kwanza, sio rahisi.
Yeye: Kwanza hata sasa hivi naweza kukutajia a,b,c ........., z, kuhusu tabia yako!
Mimi: Unawezaje kunijua tabia bila kuniona?
Itaendelea na nitakuwa nawaupdate what happened.