Ndugu zangu watu wa CCM, ebu epukeni aibu hii.

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
546
Reaction score
1,114
Unaingiaje kwenye uchaguzi Mkuu wakati huo Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani ambaye ndo mpinzani wako mkuu yupo mahabusu, na kama haitoshi, chama kimefutiwa Ruzuku yake, kimezuiliwa kufanya shughuli zake za kisiasa, kimebanwa kila kona.

Katika mazingira hayo, hapo kuna uchaguzi gani? Unachagua nini kati ya nini?

Angalau zamani hata kama CHADEMA kitashindwa kwenye box la kura, kilikuwa kinashiriki uchaguzi. Kilikuwa hakiwekewi vikwazo vingi hivi mwaka wa uchaguzi.

Watu wa CCM, mtakuwa na amani gani kuingia kwenye uchaguzi Mkuu katika mazingira haya?

Jitafakarini kwanza kabla ya kuingia kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu katika mazingira haya.
 
Hivi mnatumia vigezo gani kuseme Chadema cha Kikuu cha upinzani kwa takwimu zipi?

Hivi chama kikuu cha upinzani kina Mbunge 1 wa kuchaguliwa na Wananchi.

Hamna aliyewazuia Chadema wasishiriki uchaguzi ni wao wenyewe walisema hawashiriki unataka wabembelezwe?
 
Katika power struggle kanuni inayotumika huwa inaitwa "ubaya juu ya ubaya" ama ukitaka kumuua nyani usimtazame usoni.

CCM linapokuja suala la kuyataka madaraka wako serious na hawana utu wala huruma.

Bila kuchapana na kuuana sahau kuhusu mabadiliko.
 
Wenyewe wanajiita viziwi
 
Si uingie barabarani wewe na familia yako wauiliwe kisha Chadema isonge mbele.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Kwa hiyo chako kikuu cha upinzani ni kipi!?
 
Tanzania hatuna mfumo wa vyama vingi. Tuna kiini macho tu. Kwa vipindi tafauti watawala wamekuwa wakichaguwa chama kipi wakipaishe.

NCCR, CUF, CHADEMA, ACT vyote vimetumika. Hivi vina chembe chembe za dalili za uhai. Ama CHAUMA inashangaza kwa kweli. Labda ni jaribio la kutimiza azma ya Magufuli ya kuuwa vyama vyote baada ya 2020.
 
Naunga mkono hoja kwa 100%.
 
Hawajali, kwenye akili zao wanaona ni sawa tu kwa kweli ni aibu kwa Taifa linalojinasibu kuwa ni la kidemokrasia
 
Wewe ni Mtanzania au Mrusi?
Maana, hakuna Mtanzania anayeishi hapa Tanzania anayeweza kusema hivyo.

Ni hatari sana Taifa kuwa na watu wa aina hii.
 
Wewe ni Mtanzania au Mrusi?
Maana, hakuna Mtanzania anayeishi hapa Tanzania anayeweza kusema hivyo.

Ni hatari sana Taifa kuwa na watu wa aina hii.
Toka lini umekuwa msemaji wa Watanzania.
 
Si uingie barabarani wewe na familia yako wauiliwe kisha Chadema isonge mbele.
Tusiombe tufike huko. Kwa akili fupi tulizo nazo Watanzania tunadhani moto ukiwaka utawaunguza CHADEMA tu kitu ambacho ni UJINGA tu wa kutochambua mambo kwa kina. Ndugu yangu, tukifika huko, waliomo na wasiokuwemo wote wataunguzwa na moto huo.

Tusiombee hata kidogo kufika huko, ni hatari.
 
Sasa si wajitangaze tu washindi? Badala ya kutumia kodi za wananchi ili kufanya maigizo ya uchaguzi
 
Tanzania bara chama kikuu cha upinzani ni CHADEMA. Kwa upande wa ZANZIBAR chama kikuu cha upinzani ni ACT wazalendo

Kusema Tanzania chama kikuu cha upinzani ni CHADEMA sio kweli
Wao ni bara tu

Wenzao chama kikuu cha upinzani ZANZIBAR wamekubali kuingia kwenye uchaguzi

Hawawezi subiri cha bara kinachoringa kuingia kwenye uchaguzi
 
Ujinga tupu ulichochora hapa
 
Bahati mbaya ndugu zako hawana haya...😜
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…