Ndugu zangu wananichukia

Pole sana , ila jifunze kitu kimoja usikae na hasira rohoni au kuendelea kuwaza sana. chukulia positive way kuwa hizo ni challenges za maisha , na tambua kila ugumu unapotokea katika kutafuta solution ndo hapo unapozidi kupata experience ya maisha. Ondoa kinyongo ili usiendelee kuumia mwenyewe pia samehe na anza upya kivyako ila usikatishe mahusiano kwa mama na dada yako haya yatapita ,, na trust me ukishamove on.. baadaye dhamira itawasuta na kuanza kujirudi either kwa kuomba msamaha direct au indirect .
Kumbuka Hakuna jipya chini ya jua yanatokea sana kwenye family nyingi .ila muhimu kukabiliana nayo na kuyashinda
 
Asanteni kwa ushauri na faraja,Mungu awabariki
 
ubinadamu kazi sana. pole sana kwa matatizo
 
Pole sana mkuu ila fahamu tu kwamba wewe ni chanzo chanzo cha yote unayopitia. in Short Learn From Your Mistakes and move Forward
 

Miss jay pole,,,,ila kama uneshagundua ilo basi si watu wazur hawapend uendelee,,,cha msingi kuanzia leo sitisha kuwashirikisha ktk jambo lolote la mafanikio yako

Panga mipango yako mwenyewe fanya maendeleo yako in ur own full stop

Ushirikiano wako kwao utakuwa ni wa kawaida tu wa kindugu kama mawazo,, labda mama anaumwa dada , vikao vya familia, michango kama kuna tatizo basi lakini masuala ya kuwapa ela kwa ajiri ya maendeleo wakufanyie acha sasa ivi utakuwa maskini pliiiz

Ndugu lawama hujui huo msemo una maanisha nini

Ni ngumu saana kumuhukumu ndugu yako coz blood is thiker than water but njia sahihi ni.iyo niliokuambia piga kazi kimpango wako full stop
 

Afu kuwa makini dadangu icho kiwanja wanaweza kukiuza fanya mpango ukiuze ukajenge uko ulipo pliiz,,,na uthithubutu kufanya nao mipango ya maendeleo mshukuru mungu kwa kuweza kukuonesha.ilo
 

Wewe ndio nguzo kuu hapo ndio maana unaumizwa mama.
Usikate tamaa jenga hata mji ulipo ni asset yako, sio wote wanapata mama na dada wenye hekima na upendo wa kweli hasa katika mambo ya pesa.
Pole jipe moyo, Mungu ameshakutoa mbali sasa simama ufanye yako achana na ndugu hela pekee ya kuwapa ni ile unampa mama ya matumizi lkn mipango yako ya pesa isije ikakuweka katika ugomvi na laana.
 
Pole sana ila inaonekana hujifunzi, baada ya kuibiwa mzigo wa lak nane na mil moja ungejua type ya watu unaowaamini. Bora ufanye kazi na watu baki,mnaandikishiana so hata maswala ya kudaiana kisheria hayatakuumiza kwanza watu baki wengi ni waaminifu. Mi mzee wangu alienda kusoma nje enzi hizo, mama akabaki hali ngumu tena enzi za duka la Kaya...Mzee akipata senti anatuma vitu kwa baba mdogo akijua hapo yupo salama wakati mkewe anahangaika na watoto. Baada ya miaka miwili anarudi, mdogo wake kumbe kafilimba kila alichotumiwa na hata mkewe hakupata kitu. Ndugu ni wazuri lakini ndio chanzo cha umaskini hasa ukiwaendekeza. Simama on ur own.Ukipata visent unamtumia mama lakini sio akufanyie kazi zako. Your dad is watching over u from heaven
 
Ni pm tuongee vizuri coz unaweza pata matatizo ya kisaikolojia.

mijamaa inayopenda kulelewa utaijua tu.pm majaliwa au huna lolote mario wewe kama una ushauri umwage hapa.unataka na wewe kumdhurumu dada wa watu
 
Pole Sana Miss J
Waswahili wanasema Ni heri ya rafiki kuliko ndugu, we Ni fighter mzuri Sana msamehe mama kwa yote wala usimkasirikie, fanya mambo yako bila kuwashilikisha tafuta eneo jingine hapo ulipo fanya maendeleo yako. Mungu atakulipia tu
 
Sasa bila shaka umejifunza anza kujenga mwenyewe..! Huo ndio ukubwa kuwa makini..!
 
Dogo changamka.... wife material hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harusi yako nakupa go ahead...

nisaidie babu kunibembelezea maana fighters wakikaa meza moja lazima kodi ya bandarini ionekane
 

Umeolewa?
 
Pole sana mpendwa Miss Jay kwa yote yaliyokufika. Vikwazo kwa binadamu ni sehemu ya maisha na vikwazo hivyo ni lazima vitokee kwani vikwazo hivyo ni sehemu ya mtihani wa maisha yako ya hapa duniani. Ukifungua Biblia kwenye kitabu cha Mathayo 18:8-9 neno la Mungu linatuambia "Kama mkono au mguu wako ukikukosesha, ukate na kuutupa mbali nawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima bila mkono au mguu, kuliko kutupwa katika moto wa milele ukiwa na mikono miwili na miguu yako miwili. Na kama jicho lako likikukosesha, ling'oe na kulitupa mbali nawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa chongo, kuliko kutupwa katika moto wa Jehanamu ukiwa na macho yako yote mawili."

Mungu anapotaja viungo hivyo katika biblia hamaanishi viungo kama mawazo yetu yanavyodhani bali anamaanisha vikwazo katika maisha. Anamaanisha kama ukiwa na kitu au mtu ambaye/ambacho anakuwa/kinakuwa kikwazo katika maisha yako kwa namna moja au nyingine basi ni heri ukatengana na mtu huyo au ukachana kabisa na hicho kitu kuliko kung'ang'ania kuwa na kitu au mtu ambaye/ambacho ni kikwazo na mwisho wa siku ukaishia kutenda mambo ambayo ni chukizo mbele za Mungu.

Naamini maneno haya Matakatifu ya Mungu yatakusaidia kwa namna moja au nyingine kutatua matatizo yanayokusibu.
 
Last edited by a moderator:
Asanteni kwa ushauri na faraja,Mungu awabariki

Pole sana. Hii ya kwako si ya kwanza, wengi imewakuta. Kuna fundi mmoja mwaminifu hadi namuogopa, anakaa kwenye bonge la jumba alilojengewa na mhanga kama wewe. Yeye baada ya kurudi alishangaa kukuta nyumba imejengwa vizuri kuliko alivyotarajia.

Akampa tena tenda ya kujenga kiwanja kingine. Alivyorudi na kuuona uaminifu wa fundi, alimkabidhi fundi funguo za nyumba na hati pale pale. So fundi muaminifu ni proud owner wa nyumba ambayo ya Kaunga ni cha mtoto.

Usiache kuwapenda ndugu zako, hatuchagui ndugu lakini anza mwanzo usiogope kudhulumiwa. Kujenga ulipo sawa lakini kama hutakaa sana na ni mkoa wa pembezoni utahangaika kuja kuuza baadaye. Jichange pesa ukij likizo unafanya kitu, halafu unasubiri tena. It can be done
 
Sasa kijana unakasirika nn, wewe shukuru mungu kakuonyesha mapema! Assume uliwapa hizo hela ila usiwe na stress ndogo ndogo na anza kupambana! Kwa umri wako na hasira za maisha ulizonazo! 2years utakuwa umefunika mashimo yote yanayotakiwa kufunikwa na utaishi raha mustarehe
 

Samahani mpendwa PesaNdogo naomba nikurekebishe kidogo. Asset ni mali yoyote ambayo inaweza kuzalisha na kumuingizia mtu kipato. Nyumba ya kuishi huwezi kuiita asset kwa sababu nyumba haimuingizii mmiliki wa nyumba hiyo kipato unless nyumba hiyo iwe ya biashara yaani iwe ya kupangisha, hapo ndio utaiita hiyo nyumba kuwa ni asset.
 
Last edited by a moderator:

Nadhani unajua moja ya sifa za asset ni depreciation, nyumba ina sifa hiyo wakati ardhi alipoiweka inapanda thamani with time. Mtoa mada hajasema ni nyumba ya nini. Sijasoma biashara/uhasibu ila najua nyumba ni asset (non - current asset) ndo maana huwekwa dhamana akapata mkopo /mtaji.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…