Kupatwa kwa jua ni tukio la kisayansi ambalo hutokea sehemu tofauti duniani kila baada ya wastani wa miezi 18, lakini katika eneo moja linaweza kujirudia mara moja tu kila baada ya miaka 360 hadi 410.
Ingawa kupatwa kwa jua kunaelezeka kwa njia za kisayansi tukio hili pia lina maana kubwa ya kiroho kwa wengi. Katika mila na dini mbalimbali, kupatwa kwa jua kunachukuliwa kama ishara kutoka kwa nguvu za kimungu au onyo la kiroho.
Ndani ya Ukristo, mianga katika anga la mbingu inatumika kama dalili na majira kama ilivyoandikwa Mwanzo 1:14-15. Waumini hutumia matukio haya kama kipindi cha kujiandaa kiroho na kutafakari kuhusu majukumu yao mbele za Mungu.
Hivyo, ingawa kimsingi kupatwa kwa jua ni tukio linaloelezeka kisayansi, bado lina umuhimu wa kiroho kwa wengi. Ni sawa na fundi wa gari anayelijua gari lake ndani na nje; kulijua gari hilo kisayansi haimaanishi kuwa gari hilo halina muumbaji.
Always fikiria kwa jicho la pili.