Ndugu zangu tusiwaamini wanasiasa hata kidogo!!!

Ukwel mtupu

Member
Jan 30, 2014
40
8
Wakuu kwanza polen na majukumu ya kila siku, mimi ni mdau mkubwa wa siasa hasa baada ya uchaguz mkuu uliopita nilikuwa nafatilia sana siasa za vyama vyote chama tawala na vyama pinzani.

Mwaka 2010 kipind cha uchaguzi mkuu nilikuwa nimejielekeza zaid katika kufatilia hoja zilizokuwa zikitolewa na vyama pinzani hasa chadema kwa kuongea hoja za msingi ambazo zilikuwa zinagusa maisha ya watu kitu kilichopelekea chama hicho kupata umaarufu mkubwa na hivyo kujizolea kura nyingi

Waliokuwa wagombea wengi wa chama hiki ambao baadhi yao walihama kutoka chama tawala waliweza kuwashawishi wananchi kwa kueleza mapungufu, udhaifu na uovu wa chama tawala hali iliyowafanya wananchi kuwaamin na hivyo kuwachagua.

Cha ajabu kilichonifanya hadi niamue kuweka uzi huu hii leo ni kutokana na baadhi ya wanasiasa kuhama kutoka chama kimoja na kwenda kingine, cha ajabu na kuchekesha ni mtu huyo huyo aliyekuwa anakiponda chama kile ndiyo huyo huyo anahamia tena chama kilekile. Mfano mzuri nafikir wadau wa siasa mliona kilichotokea shinyanga siku ya jana na juzi kwacmadiwan wawili wa chadema kuamua kujiuzuru na hatimaye kurud ccm, kipind cha kampen za uchaguz wa 2010 nilkuwa shinyanga na nilbahatika kuhudhuria kampen za mmoja wa madiwan hao, kwa jins alivyokuwa ananad sera zake kwa kukiponda chama tawala usingeweza kuamin kuwa mtu huyu angeweza kurud kulekule alikokuwa anakuponda.

Swali la kujiuliza ni je kule alikokuwa anakuponda kwa kueleza kasoro zake leo hii kuna mabadiliko, je wahusika wamejirekebisha had kuamua kurud huko???Wahusika hawa walichangia kwa kias kikubwa chadema kupata kura nying sana had watu kuamin kuwa hata ubunge chadema ilishinda ila uchakachuaji ulifanyika leo hii watu haohao wanarud kulekule walikokuwa wanakuponda, nashindwa kuelewa katika mikutano yao watawaeleza nin wafuas wao waliowaamini, wanaweza wakawaeleza kuwa tulikokua hapafai, je huko walikoenda panafaa yale madhaifu waliyokuwa wanayaeleza yameisha???

Binafsi naweza kidogo kumwamin mwanasiasa anaetoka chama cha upinzan na kuamia chama kingne cha upinzan kwa kuamin labda chama alichokuwa kilkuwa na mapungufu yasiyoweza kurekebishika na hivyo kuamua kutafuta mbadala wake lakin si yule wa kurud upande aliyouona haumfai

Kwa kweli watanzania wenzangu bado tuna safari ndefu sana ya kupata wanasiasa wenye dhamira ya dhati kabisa katika kulikomboa taifa hili, vinginevyo tutajikuta tunahama vyama kila siku tukiamin huko tuendako ndiko kunafaa kumbe hakuna, pia tutajaza utitiri wa vyama pasipo mabadiliko yoyote.

Wanaanchi wanapanga foleni kutwa nzima kuwachagua leo hii mnawasaliti kwa kuwaacha njian huku mkiwapa majibu mepesi mepesi, wananchi wasipopiga kura mnawalaumu eti hawazijui haki zao mara hawajui demokrasia, demokrasia gani iliyojaa usaliti wa hali ya juu kiasi hicho???huyo huyo mwananchi leo anaenda kupiga kura kwa mara nyingine na hana iman kama huyo anaemchagua tena atamsaliti au la!!!

TUSIWAAMINI WANASIASA NDUGU ZANGU WAWE WA CHAMA TAWALA AU WA UPINZANI!!!
 
Kazi ipo kwa wanasiasa wetu!!!
 
Wanasiasa wengi ni wachumia tumbo... Wanaangalia upepo upi una harufu ya ankara, na hiki ndicho kiini cha usaliti. Tamaa na njaa vinawamaliza wanasiasa!
 
Back
Top Bottom