Ndugu yetu yupo kwenye mtego nchi moja ya hapo Ulaya, tunamtoaje?

Kamongo

JF-Expert Member
Mar 20, 2009
1,956
2,072
Ushauri kwa Ndugu yetu Ambaye yupo masomoni nchi za Ulaya.
Ndefu Ila nafupisha kwa Kadri ya uwezo ......Bro.wangu Anasoma nchi moja hapo ulaya!
Huyu Ni brother Alienda Europe 2020..alienda kimasomo.
Katika Fani ya Afya hivyo Amefanikiwa kupata chuo kizuri na kuanza kuishi maisha ya hostel ...hivyo baadae Akaomba kazi kwenye hospital ya private kufanya part time Tena hususani mida ya usiku.
Siku moja akaja mwanamke mmoja wa kizungu anaumwa Katika kujielezea , Madaktari wa kizungu wakagundua hii Itakuwa Ni malaria Sasa bila Kuchukua vipimo wakampeleka kwa dokta wa kibongo maana hizi case kwao hawazijui Sana Kama Daktari anayetokea Kanda ya Africa Atakuwa na utalaamu zaidi na wenzetu wanaangalia uzoefu zaidi.
Dokta.Tumwite Charles...
Kufika kwa Charles akamsikiliza , akagundua wiki Kama moja nyuma alisafiri kwenda middle East na India pia hivyo akampima malaria akutwa nayo ..akawa ametafuta dawa akakosa zipo sindano tu! Hivyo akamwandikia sindano.
Akampa nurse wa kike awe Ana mpiga sindano Ila mama aka chagua dr.charles afanye Hilo Zoezi hata Kama kumlipa kwa muda Ziada atafanya hivyo.
Kweli Zoezi likaanza na dokta.. Charles akawa anampiga sindano yule mama wa kizungu...Tumwite Doris.
Siku siyo nyingi akapona.
Hivyo akawa anajulikana hata home kwa Huyo Doris
Hata mumewe Doris akawa anamjua dokta Charles.
Sasa Katika Harakati zile yule Doris alimuuliza Charles..unaishi wapi ?
Charles akamtajia Ila Ikawa Hizo hostel zipo mbali Sana na hospitali anayo fanyia kazi.
Hivyo Doris akamwambia kwanini usihamie maeneo ya Karbu ? Chale akasema hapa ni town Sana na Gharama zipo juu' istoshe mm nakaaa hostel hivyo nalipia kidogo Kama Dola 220 hivi kitu ambacho Ni affordable kwangu Ila hapa town Ni kuanzia Dola 1,000 hivi hivyo siyo Rafiki kwa uchumi wangu.
Doris akamwambia atamsaidia Asogee Karbu Ila sio kwa kumpa pesa Bali ampe vielelezo vya hayo malipo hapo hostel Kisha aongee na mumewe ili aweze kulipia kiasi hicho hicho kwenye moja ya apartment zao zilizopo maeneo ya Town.
Charles akakubali akampa kopi ya mkataba.
Siku chache yule mama ...Doris...akamletea Charles mkataba w Apartment mpya ndani ya Town.
Malipo Ni Dola 200( krona 2000 hivi) tu kwa Mwezi discount katoa hapo Dola 20 kila Mwezi.
Dhamani ya apartment pale Ni Dola 1,700 ( krona sek 17500) mpaka Dola 3,500 (krona sek.. 35,945) na wapangaji wapo wengi ndani ya gorofa 12.
Dokta Charles peke yake ndio Amepewa favor hiyo.
Mkataba Ni miaka 3 na Nusu.
Mkataba umenza January 2023.
Baada ya kuhamia Sasa ...Doris Anakuja home peke yake kuja kumsalimia Charles siku za wikendi ...
Sasa issue ipo japo Ni mwenye nyumba akija wapangaji wengine Hawa mjui Wala hata hawana time naye akija huyooo mpaka kwa Dokta Charles.
Watapiga storii wee, wataangalia movie then Doris anaondoka Kama Kuna Cha ziada hajanieleza.
Tatizo limekuja kuna mke wa baharia mmoja wa meli/pilot tuseme.. ameonesha Dalili zote za kumtaka Dokta Charles kwani anaweza kumblock kwenye parking bila sababu za msingi inabidi apande lift Hadi gorofa ya 8 kumgongea akitoka Sasa alivyo vaa Sasa lazima network isimame vilivyo..
Charles anapitia Mengi...tu
.. hajui awe rickboy au nn!
Akisema Ni Mambo ya bongo kimasihara anaweza tekwa atupwe hata baharini , pia shaba inaweza mhusu na yupo nchi za watu.
Gorofa ya tano Kuna mke wa afisa wa polisi naye amechukua namba yake Huyo mama nae Ni Askari
Dada anatuma jumbe za mahaba...Ila Dokta anaogopa kujibu kwaajili ya ushaidi anaogopa mumewe Anaweza kuona na ana chuma kikali huwa kina ningi'nia kiunoni Muda wote akimwona.... Hivyo bro Ni shida!! Tu Hana Raha sasa.
Yeye bro.anakaa Kama floor/ 7 hivi.
Any way ..... please Toa ushauri wa Afya hapa Ni ufikishe kwa Niaba Kwa brother Dokta Charles afanye Nini?
Mpira uko kwenu Wana jukwaaa.
........Ukizani hii Ni chai ongezea sukari maana hii Ni ya majani tupu! .Haina ladha.
Okay country code ya Dokta Charles hii hapa...+46
Ushauri wenu Ni muhimu na Kama unatambua hiyo code na umekaa huko elezea maenye yenye nyumba za Bei nafuu ' inaweza kumsaidia pia!!
Hiyo ni Chai ya kijiweni wazungu siku hizi wameshtuka,
 
Sasa si awale wote ?

Akila wote watakasilikiana wao kwa wao wala haina shida. Akila wawili tu itakuwa shida.

Mwisho wa siku mtu anakazi yake aachane na kulelewa na jimama.
 
Ndugu yangu hapo umedaganya kabisaa???Kama mtu ameanza Kozi hiyo ya MD mwaka 2020 leo hii 2023 huyo ni MD2 bado hata kwenda wodini harusiwi kabisa na kutibu bado ki kosa la jinai.
 
Pesa ya krona ni Sweden
+46 ni Sweden
Hivyo mta jiju wewe na huyo rafiki yako!
 
Back
Top Bottom