Ndugu yangu ameamka asubuhi na matope miguuni

Ndugu yangu ameamka asubuhi na matope miguuni

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
2,938
Reaction score
517
Kuna ndugu yangu anaishi nyumbani kwangu. Jana Jumapili alipoamka asubuhi sana ili ajiandae kwenda kusali Kanisani lakini cha ajabu alikuta miguu yake ina matope kibao tena akiwa amechoka balaa. akaja kunijulisha huku akiwa na matope kibao kwa kweli nilipigwa na butwaa na ikabidi tumpeleke Kanisani kuombewa.

Wakuu nakuja kwenu kama kuna mwenye idea na mambo haya na chanzo chake nini hasa?

Karibuni..
 
Alioga kabla ya kulala kweli? Na usiku wa kuamkia jumapili alitokea wap? Manake huu msimu ni wa mvua so matope yapo sana huko mabara barani.

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Chanzo chake ni mvua zinazoendelea kunyesha! Kwani ulivyompeleka kuombewa ulihisi ni nini?
 
Alioga kabla ya kulala kweli? Na usiku wa kuamkia jumapili alitokea wap? Manake huu msimu ni wa mvua so matope yapo sana huko mabara barani.

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums

mkuu huyu mtu jioni hakutoka nje kashinda ndani
 
kuna ndugu yangu anaishi nyumbani kwangu. jana jumapili alipoamka asubuh sana hili ajiandae kwenda kusali kanisani lakini cha ajabu alikuta miguu yake ina matope kibao tena akiwa amechoka balaa. akaja kunijulisha uku akiwa na matope kibao kwa kweli nilipigwa na butwaa na ikabidi tumpeleke kanisani kuombewa. wakuu nakuja kwenu kama kuna mwenye idea na mambo haya na chanzo chake nini hasa? karibuni.

Kulala bila kutubu, kuomba rehema na kujiweka katika uwepo wa MUNGU na kujifunika kwa damu YA YESU KRISTO WA NAZARETI ALIYE HAI NDIO CHANZO cha kujiweka karibu na wanachawi hakuna kingine.
 
Ni chapombe usikute ile mvua ya Jana kakesha Njia panda bar na kwenu Huko ni mabondeni.
 
Inavyoonekana Kuna mchawi nyumba yake ilikumbwa na mafuriko sasa alikuja kumchukua usiku kwenda kumsaidia mchawi kuhamisha vitu , ILA inavyoonekana walichelewa Sana inabidi amrudishe bila kunawa miguu
 
Wwweweee !!!!!acha kututania....unauliza nini wakati ulienda kwenye maombi kabla ya kuja huku....kwa nini usimpeleke Muhimbili kwenye kile kitengo cha Sakatrik.....yaani kawa kichaa na kujipaka matope.Kwa ufupi hiyo ni sayansi ya kienyeji na huyo kijana amefanyiwa test tu .... mengine yatamfuata wanasayansi hao wakiona yu mtupu.Ushauri kwa sasa ni shida saana maana Ramli chonganishi zimepigwa marufuku.plan B awache mambo yake ya u bishoo hapo mtaani au sivyo atajikuta amelala nje.
 
Au ulihisi walikua wanamfyatulisha matofali usiku?
 
COSTECH .......inashughulikia watafiti na wana sayansi.....tumeni watafiti katika hili...lipo kila siku
 
Nikuhabarishe....kuna wengine kazi yao ni kuja kula kwako tu.Unaweza pika ugali wa unha kilo3 msishibe watu wa 3..baba.mama na mtoto wa miaka6.na kila ukiongeza unga na wao wanaongezeka.Yaani munakula nao bila ya kuwaona.Lakini kama umefuga mbwa au paka huwa wanawaona na hupiga kelele.pia njiwa wanasaidia.
 
Unanifanya nichekee
 
Wewe tinga COSTECH watume watafiti na wana sayansi... mbona kule Rufiji wanasayansi wanapovuka mto kwenda ngambo ya pili kufanya utafiti ni lazima wapate kibali cha wenyewe ili viboko na mamba wasimamishwe kuwadhuru.
 
Back
Top Bottom