Ndugu wa Mbunge anaswa na shehena ya Cocaine, Heroine

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
na Mwandishi wetu



MFANYABIASHARA anayedaiwa kuwa ni kinara wa biashara ya dawa za kulevya nchini, amenaswa na shehena ya dawa za kulevya aina ya Heroine na Cocaine.

Mfanyabiashara huyo, ametajwa kwa jina moja la Asad na anadaiwa kuwa na uhusiano wa kindugu na mmoja kati wabunge maarufu nchini, mwenye asili ya Kiasia.

Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema kuwa mfanyabiashara huyo alinaswa na dawa hizo za kulevya nyumbani kwake, Mikocheni na kiasi kingine kilinaswa Kabuku, mkoani Tanga.
Mmoja wa maafisa wa polisi wanaohusika na kitengo cha kupambana na dawa za kulevya, aliliambia gazeti hili kuwa mfanyabiashara huyo alinaswa mkoani Arusha, akijaribu kuwatoroka polisi waliokuwa wakimsaka kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa habari hizo, mfanyabiashara huyo ambaye ni mmoja wa vigogo wa biashara hiyo amekuwa akisakwa na polisi kwa muda mrefu na kuwatoroka mara kwa mara.

“Amekamatwa na kiasi kikubwa cha Heroin Kabuku Tanga, alikamatwa pia na shehena nyingine ya dawa za kulevya aina ya Cocaine nyumbani kwake Mikocheni na mwenyewe amekutwa mjini Arusha akiwa kwenye harakati za kuwatoroka polisi,” kilisema chanzo chetu cha habari.
Akithibitisha kukamatwa kwa mihadarati hiyo, Kamanda wa Kikosi cha kupambana na dawa za kulevya, Godfrey Nzowa, alikiri kukamatwa kwa kigogo huyo.

Alisema mfanyabiashara huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho mjini Tanga kujibu tuhuma hizo.

Hata hivyo hakuwa tayari kueleza mahusiano ya kigogo huyo na mbunge mmoja maarufu nchini kwa madai kuwa taarifa zote zitapatikana mahakamani hapo. “Kweli tumemkamata na kiasi kikubwa cha mihadarati na kesho (leo) atafikishwa mahakamani mkoani Tanga. Taarifa zingine zote za uhusiano wake na mbunge uliyemtaja, mtazipata mahakamani hapo kesho,” alisema Kamanda Nzowa.
 
Kesi za madawa ni kiinimacho tu!
Mnajua kesi yoyote ya hivi iliyotolewa hukumu?...ha ha haaa!
Hapo watamwambia apime mwenyewe uzito wa kesi, na hivyo atajua awaacheache vipi!
 
Very poor journalism. Kama una uhakika na taarifa yako kwa nini jina lifichwe.

Ndugu yangu hizo ni habari nyeti most of good journalist hawapublish majina yao kama wanashika vitu kama hivyo hadi USA they do the same hawajipambi kwa Majina yao
 
still, it reflects poor journalism. Hivi ukiwa na jamaa wa mbunge inamaanisha nini? Amehusika au? Wale wanaofungwa hawana ndugu? Pia haielezi hata hayo mazingira ya kumkamata kiufasaha zaidi ya kusema walikuwa wakimtafuta. Inamaana wamsearch Dar baada ya kukamata na dawa nyinginr Tanga? Uandishi huu!
 
Kesi za madawa ni kiinimacho tu!
Mnajua kesi yoyote ya hivi iliyotolewa hukumu?...ha ha haaa!
Hapo watamwambia apime mwenyewe uzito wa kesi, na hivyo atajua awaacheache vipi!

Hivi huwa wanaambiwa wapime nini wenyewe?

Wapime mshiko?
 
Hakuna kesi hapo kwa maisha ya bongo tena ni ndugu ya mhe. Mbunge? jamaa hata kabatini kajalaa ashatolewa zamani!
 
ukiona nguli wa kihivyo kadakwa jua kahitilafiana na hao wazuia madawa wenyewe! manake ni DUGU MOJA!!! kwani zinaendaga wapi hizo coc na her wanazoklamata!!! DANGANYA TOOOTOOO
 
Kesi za madawa ni kiinimacho tu!<br />
Mnajua kesi yoyote ya hivi iliyotolewa hukumu?...ha ha haaa!<br />
Hapo watamwambia apime mwenyewe uzito wa kesi, na hivyo atajua awaacheache vipi!
<br />
<br />Uko sawa kabisa,nani anakumbuka ile kesi ya madawa yaliyokamatwa mbeya kwenye maiti na promotion ya kova kuletwa dar unganisha dots utapata jibu
 
Ndugu yangu hizo ni habari nyeti most of good journalist hawapublish majina yao kama wanashika vitu kama hivyo hadi USA they do the same hawajipambi kwa Majina yao
poor journalism babaa

KWani kuwa ndugu na kiongozi ni siri??
 
Hivi huyu Nzowa kwanza si ana kashfa huyu?Vipi ile tume waliyoiunda kuchunguza dhidi ya tuhuma za Mengi na mwanae kubambikiwa madawa ya kulevya?na waandishi wa habari wa bongo nao full magumashi kwani hawatupatii muendelezo wa matukio mbali mbali kwa kufuatilia mwisho wake hivyo haya mambo ni stori tu na hakuna lolote kuanzia aliyekamatwa hadi waliyekamata aka pilisi wakiongozwa na Nzowa mwenyewe:crying::crying:
 
wahalifu ni wahalifu tiu haijalishi ni ndugu wa mbunge au rais....
 
Too Many Loopholes... Hawafanyi background checks kwa Wabunge? kuona kama familia zao zina biashara gani au ni pesa mtindo mmoja?
 
Angekuwa ni ndungu wa mbunge wa chama cha upinzani tiyari habari leo,jambo leo,mtanzaniana vigazeti vingine vingeshadadia. Nakumbuka diwani wa Chadema kukamatwa na bunduki hayo magazeti yalivyo shangilia.
 
Back
Top Bottom