Uchaguzi 2020 Ndugu Tundu Antipas Lissu, mgombea bora wa urais kuwahi kutokea Tanzania

Habari kwenu waungwana.

Tangu nimekuwa nikifuatilia siasa za nchi hii kwa vipindi kadhaa vya chaguzi kuu. Hapa ni kwa kipindi ambapo sikuwepo ila kwa njia ya masimulizi ya kihistoria na vile vipindi ambavyo nimekuwa nikishuhudia kwa macho na masikio yangu hasa baada ya kuwa na uchaguzi wa vyama vingi 1995 hadi leo hii.

Nikiri kusema wazi kuwa, hapajatokea Mgombea wa Urais wa Tanzania mwenye uwezo wa ajabu kama alivyo huyu mwamba Tundu A Lissu.

Kwa wafuatiliaji wazuri sina haja ya kupoteza muda kuwataja wagombea wa urais kadhaa waliopata kuwepo na ambao wapo sasa kwenye kinyang'anyiro hiki cha 2020 na kama kuna mtu anapinga hili alete mgombea wake tumlinganishe na huyu mwamba.

Tundu ameonesha uwezo mkubwa sana katika kuzijua sheria za nchi na kimataifa hivyo ameshindikanika kuyumbishwa na propaganda za kisiasa za wanasiasa uchwara(wapinzani wake mf. Polepole na watu wake) kwa kweli wameshindwa kufua dafu hata kwa punje.

Tundu ameonesha uwezo mkubwa wa kutoa hoja zisizojibika kwa upande wa wapinzani wake. Mfano matumizi mabaya ya madaraka na uongozi usiofuata sheria wa CCM wakiongozwa na mgombea wao ambae ni rais anaemaloza muda wake.

Mathalani ujenzi wa uwanja wa ndege nyumbani kwao Chato, ununuzi wa ndege ambao haujafuata sheria za manunuzi, urasimishaji wa mbuga ya Burigi na kuhamisha wanyama, kupata wakandarasi wa miradi mikubwa ya umeme wa MNHEP na SGR zabuni zake hazieleweki na wakandarasi wamepatikanaje pamoja na kashfa ya kumtimua CAG kufuatia hoja ya kukosekana kwa maelezo ya matumizi ya pesa ya umma ya Tsh1.5t. Hoja hizi "konki" hakuna wa kuzijibu na hata kama zimejibiwa ni blah blah tu.

Lakini yeye kawa mahiri sana katika kujibu hoja za upande wao rejea mikutano ya waandishi wa habari aliyofanya Tundu Lissu na majibu yake mujarabu kabisa.

Ni mgombea anaeijua vizuri historia ya nchi hii kabla na baada ya uhuru na mifumo yake ya uongozi na sheria hivyo hawana chocho ya kumpoteza huyu mwamba na michezo yote michafu ya kisiasa anaijua na dawa yake anaonekana kaiandaa vyema na anapenda sana amani ndio maana anasisitiza juu ya haki itendeke kwa kila hatua ili uchaguzi ufanyike kwa utaratibu na mshindi atangazwe hakutakuwa na shida.

Ni mgombea anaeonekana kajipanga vyema kwa kila hatua ya uchaguzi, anakuambia tofauti yake yeye na wagombea wa vyama vya upinzani waliopita ni kuwa hawakuwa na mawakala wa kutosha nchi nzima ila yeye kajipanga vya kutosha hivyo atahakikisha kura zake zinalindwa na kutangazwa.

Sio mgombea mnyonge. Ni mtu anaejiamini sana na mpigania haki za wanyonge. Historia inambeba tangu akiwa ni wakili wa kawaida kabisa ametumia nafasi yake kupambania haki za wanyonge huko Tarime Nyamongo wanajua vizuri lakini hata akiwa mbunge amekuwa akiipambania nchi kwa kufuata sheria ili iepukane na kesi pamoja na hasara ya kulipa fidia. Amejitolea kwa uwezo wake na fani yake kupambania nchi na watu wake.

Ni mwalimu mzuri sana anayevutia kumsikiliza; fuatilia mikutano yake ya kampeni hakika hutoki mtupu ndio maana anajizolea mamia na maelfu ya wasikilizaji. Anahakikisha wananchi wa Tanzania wanaelewa sheria na kuzielewa haki zao ila kupambania haki zao kwa wanaowanyima.

Aisee ni mengi ya kuandika lakini nisiwanyime nanyi mchangie juu ya ubora wa mgombea huyu ambaye mimi nimemuweka namba moja.

Wasalamu!
Ccm mwaka huu wanalo,huyu mwamba ni no nyingine,sio lile zezeta Edo lilishinda badala ya kudai haki yake likasema linamwachia Mungu,Mungu yuko busy na mambo ya muhimu ya kufanya ..
 
Mapolisi wanapigwa vifungu vya sheria huko kanda ya ziwa wanatulia na mabomu yao kama maji kwenye mtungi!
Adi jamaa wanaona wivu! Akuna kitu kizuri kama kuna jambo ambalo ulikuwa hulijuwi ukapata mtu wa kukufundisha hakika Lissu ni bonge la mwalim Mungu ampe kila la kheri
 
Laiti Kama kipindi cha Lowasa upinzani wangekuwa na mgombea imara na machachari Kama TL, CCM ingemtangulia Mkapa kabulini. Hata hivyo, CCM itamfuata Mkapa very soon. Lowasa kumbe alikuwa zoofu taaabani.
 
kwanini nani asiyewajua CHADEMA kuwa kwenye social media mpo kila kona kuhaha ili kuwakamata vijana maana ndo watumiaji wakubwa wa social media.

hii kampeni haitazaa matunda jiandaeni kwa mambo mengine ila Ikulu ni jambo gumu sana kumuangusha Magufuli.

najua wapo mtanikosoa lakini ndo uweli mchungu Lissu hatoboi na baada ya hapo ajiandae kuporomoka kisiasa maana CHADEMA ni mwiko kwa mtu mwingine kuwa maarufu zaidi ya MBOWE
We unaumwa nini... wewe na baba ako nani wakwanza kuijua jamii forum?
 
TUNDU ANTHIPAS MUGHWAI LISSU Ni TUNU kwa Taifa hili .

Ni mzalendo wa dhati kweli kweli kwa maneno na vitendo

Hana chembe ya unafiki ,ujeuri ,ujuaji ,kiburi,kisasi,ubabe .

Anakupa darsa murua unamkubali unalainika na kusema "ama kwa hakika hapa MUNGU aliumba kiumbe chema sana"

Msomi asie ma doa ana mtetexi kweli wa wanyonge kwa maneno na vitendo (bishaaa)

Kama ambavyo katika soka tunamshuru MUNGU kutuletea na kuona kipaji Cha MESSI .Hata katika Sisi watz tunamshuru MUNGU kutuletea TUNDU lissu

Viva lissu Viva TANZANIA.
 
kwanini nani asiyewajua CHADEMA kuwa kwenye social media mpo kila kona kuhaha ili kuwakamata vijana maana ndo watumiaji wakubwa wa social media.

hii kampeni haitazaa matunda jiandaeni kwa mambo mengine ila Ikulu ni jambo gumu sana kumuangusha Magufuli.

najua wapo mtanikosoa lakini ndo uweli mchungu Lissu hatoboi na baada ya hapo ajiandae kuporomoka kisiasa maana CHADEMA ni mwiko kwa mtu mwingine kuwa maarufu zaidi ya MBOWE
hutaki sasa, ccmu wale wabashite mtandaoni sijui walipotelea wapi,ccm wengi mabumbumbu tu hawajui kutumia media vizuri zaidi ya kufuatilia clips za Amberuty
 
Lissu mnafiki mkubwa huyu, limevaa kanzu huku linachuki kubwa na waislam
Kuna mnafiki kama huyo wa kwenu anayesema maendeleo hayana vyama halafu wakati huo huo anasema msiponichagua maendeleo mtayasikia? Pumzi imekata ndio maana mnawaya waya tu. Mnaitisha press mnaongea utumbo (polepole) halafu mnalituma robot lenu (mahera) lije kuanika ujinga wake hadharani wakati mliongelea chumbani. Safari hii mmegusa live current.
 
Hakika ni Mgombea Bora .... Tena ni Kizazi cha BORN FREE (Baada ya Uhuru). Yaani anapambana watu zaidi ya 5 kwa wakati moja halafu anawagalagaza wote. Magufuli, Majaliwa, Samia, Pinda, Kikwete, Mzee Makamba na sasa Mahela aliyeongezeka kwenye team!!
Ni YEYE
 
kwanini nani asiyewajua CHADEMA kuwa kwenye social media mpo kila kona kuhaha ili kuwakamata vijana maana ndo watumiaji wakubwa wa social media.

hii kampeni haitazaa matunda jiandaeni kwa mambo mengine ila Ikulu ni jambo gumu sana kumuangusha Magufuli.

najua wapo mtanikosoa lakini ndo uweli mchungu Lissu hatoboi na baada ya hapo ajiandae kuporomoka kisiasa maana CHADEMA ni mwiko kwa mtu mwingine kuwa maarufu zaidi ya MBOWE
KINACHONISHANGAZA TUNDU HASEMII KABISA SWALA LA USHOGA WAKATI ANATUHUMAA KUWA KATUMWA KUPIGIA UPATU USHOGA
 
kwanini nani asiyewajua CHADEMA kuwa kwenye social media mpo kila kona kuhaha ili kuwakamata vijana maana ndo watumiaji wakubwa wa social media.

hii kampeni haitazaa matunda jiandaeni kwa mambo mengine ila Ikulu ni jambo gumu sana kumuangusha Magufuli.

najua wapo mtanikosoa lakini ndo uweli mchungu Lissu hatoboi na baada ya hapo ajiandae kuporomoka kisiasa maana CHADEMA ni mwiko kwa mtu mwingine kuwa maarufu zaidi ya MBOWE
Pole sana mkuu maana naona umeandika kwa uchungu sana, upinzani uko kwenye damu. Sasa na nyie mnaenda kuwa wapinzani, nina uhakika hata miaka miwili hamfiki kabla chama chenu hakijafa. Tuliwaambia kuwa jiwe hafai kuwa hata kiongozi wa familia lakini mkabisha, sasa mnavuna mlichopanda

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom