Uchaguzi 2020 Ndugu Tundu Antipas Lissu, mgombea bora wa urais kuwahi kutokea Tanzania

hata ukianza kumsikiliza unavutiwa na hoja zake tofauti na uyo mwengine unaweza ukaanza kuona aibu wewe badala ya muongeaji....ni heli ata umsikilize yule wa ubwabwa na kuku kidogo utaongeza siku za kuwepo uhaini
 
They proved their midget upstairs that's why they opted gunning him as a short cut but nature n God proved them Short cut is always a wrong cut // njia ya kumuua ilishindwa na Mungu sembuse mahakama na sheria za kifedhuli?
Short cut is always long.
 
Habari kwenu waungwana.

Tangu nimekuwa nikifuatilia siasa za nchi hii kwa vipindi kadhaa vya chaguzi kuu. Hapa ni kwa kipindi ambapo sikuwepo ila kwa njia ya masimulizi ya kihistoria na vile vipindi ambavyo nimekuwa nikishuhudia kwa macho na masikio yangu hasa baada ya kuwa na uchaguzi wa vyama vingi 1995 hadi leo hii.

Nikiri kusema wazi kuwa, hapajatokea Mgombea wa Urais wa Tanzania mwenye uwezo wa ajabu kama alivyo huyu mwamba Tundu A Lissu.

Kwa wafuatiliaji wazuri sina haja ya kupoteza muda kuwataja wagombea wa urais kadhaa waliopata kuwepo na ambao wapo sasa kwenye kinyang'anyiro hiki cha 2020 na kama kuna mtu anapinga hili alete mgombea wake tumlinganishe na huyu mwamba.

Tundu ameonesha uwezo mkubwa sana katika kuzijua sheria za nchi na kimataifa hivyo ameshindikanika kuyumbishwa na propaganda za kisiasa za wanasiasa uchwara(wapinzani wake mf. Polepole na watu wake) kwa kweli wameshindwa kufua dafu hata kwa punje.

Tundu ameonesha uwezo mkubwa wa kutoa hoja zisizojibika kwa upande wa wapinzani wake. Mfano matumizi mabaya ya madaraka na uongozi usiofuata sheria wa CCM wakiongozwa na mgombea wao ambae ni rais anaemaloza muda wake.

Mathalani ujenzi wa uwanja wa ndege nyumbani kwao Chato, ununuzi wa ndege ambao haujafuata sheria za manunuzi, urasimishaji wa mbuga ya Burigi na kuhamisha wanyama, kupata wakandarasi wa miradi mikubwa ya umeme wa MNHEP na SGR zabuni zake hazieleweki na wakandarasi wamepatikanaje pamoja na kashfa ya kumtimua CAG kufuatia hoja ya kukosekana kwa maelezo ya matumizi ya pesa ya umma ya Tsh1.5t. Hoja hizi "konki" hakuna wa kuzijibu na hata kama zimejibiwa ni blah blah tu.

Lakini yeye kawa mahiri sana katika kujibu hoja za upande wao rejea mikutano ya waandishi wa habari aliyofanya Tundu Lissu na majibu yake mujarabu kabisa.

Ni mgombea anaeijua vizuri historia ya nchi hii kabla na baada ya uhuru na mifumo yake ya uongozi na sheria hivyo hawana chocho ya kumpoteza huyu mwamba na michezo yote michafu ya kisiasa anaijua na dawa yake anaonekana kaiandaa vyema na anapenda sana amani ndio maana anasisitiza juu ya haki itendeke kwa kila hatua ili uchaguzi ufanyike kwa utaratibu na mshindi atangazwe hakutakuwa na shida.

Ni mgombea anaeonekana kajipanga vyema kwa kila hatua ya uchaguzi, anakuambia tofauti yake yeye na wagombea wa vyama vya upinzani waliopita ni kuwa hawakuwa na mawakala wa kutosha nchi nzima ila yeye kajipanga vya kutosha hivyo atahakikisha kura zake zinalindwa na kutangazwa.

Sio mgombea mnyonge. Ni mtu anaejiamini sana na mpigania haki za wanyonge. Historia inambeba tangu akiwa ni wakili wa kawaida kabisa ametumia nafasi yake kupambania haki za wanyonge huko Tarime Nyamongo wanajua vizuri lakini hata akiwa mbunge amekuwa akiipambania nchi kwa kufuata sheria ili iepukane na kesi pamoja na hasara ya kulipa fidia. Amejitolea kwa uwezo wake na fani yake kupambania nchi na watu wake.

Ni mwalimu mzuri sana anayevutia kumsikiliza; fuatilia mikutano yake ya kampeni hakika hutoki mtupu ndio maana anajizolea mamia na maelfu ya wasikilizaji. Anahakikisha wananchi wa Tanzania wanaelewa sheria na kuzielewa haki zao ila kupambania haki zao kwa wanaowanyima.

Aisee ni mengi ya kuandika lakini nisiwanyime nanyi mchangie juu ya ubora wa mgombea huyu ambaye mimi nimemuweka namba moja.

Wasalamu!
Nisawa kabisa kauli hii si mpya maskioni mwetu, hivyo hata mtakae mleta tena 2025 atakua bora kuwahi kutokea
 
Back
Top Bottom