Uchaguzi 2020 Ndugu Tundu Antipas Lissu, mgombea bora wa urais kuwahi kutokea Tanzania

Real Patriotist

Senior Member
Feb 6, 2016
183
500
Habari kwenu waungwana.

Tangu nimekuwa nikifuatilia siasa za nchi hii kwa vipindi kadhaa vya chaguzi kuu. Hapa ni kwa kipindi ambapo sikuwepo ila kwa njia ya masimulizi ya kihistoria na vile vipindi ambavyo nimekuwa nikishuhudia kwa macho na masikio yangu hasa baada ya kuwa na uchaguzi wa vyama vingi 1995 hadi leo hii.

Nikiri kusema wazi kuwa, hapajatokea Mgombea wa Urais wa Tanzania mwenye uwezo wa ajabu kama alivyo huyu mwamba Tundu A Lissu.

Kwa wafuatiliaji wazuri sina haja ya kupoteza muda kuwataja wagombea wa urais kadhaa waliopata kuwepo na ambao wapo sasa kwenye kinyang'anyiro hiki cha 2020 na kama kuna mtu anapinga hili alete mgombea wake tumlinganishe na huyu mwamba.

Tundu ameonesha uwezo mkubwa sana katika kuzijua sheria za nchi na kimataifa hivyo ameshindikanika kuyumbishwa na propaganda za kisiasa za wanasiasa uchwara(wapinzani wake mf. Polepole na watu wake) kwa kweli wameshindwa kufua dafu hata kwa punje.

Tundu ameonesha uwezo mkubwa wa kutoa hoja zisizojibika kwa upande wa wapinzani wake. Mfano matumizi mabaya ya madaraka na uongozi usiofuata sheria wa CCM wakiongozwa na mgombea wao ambae ni rais anaemaloza muda wake.

Mathalani ujenzi wa uwanja wa ndege nyumbani kwao Chato, ununuzi wa ndege ambao haujafuata sheria za manunuzi, urasimishaji wa mbuga ya Burigi na kuhamisha wanyama, kupata wakandarasi wa miradi mikubwa ya umeme wa MNHEP na SGR zabuni zake hazieleweki na wakandarasi wamepatikanaje pamoja na kashfa ya kumtimua CAG kufuatia hoja ya kukosekana kwa maelezo ya matumizi ya pesa ya umma ya Tsh1.5t. Hoja hizi "konki" hakuna wa kuzijibu na hata kama zimejibiwa ni blah blah tu.

Lakini yeye kawa mahiri sana katika kujibu hoja za upande wao rejea mikutano ya waandishi wa habari aliyofanya Tundu Lissu na majibu yake mujarabu kabisa.

Ni mgombea anaeijua vizuri historia ya nchi hii kabla na baada ya uhuru na mifumo yake ya uongozi na sheria hivyo hawana chocho ya kumpoteza huyu mwamba na michezo yote michafu ya kisiasa anaijua na dawa yake anaonekana kaiandaa vyema na anapenda sana amani ndio maana anasisitiza juu ya haki itendeke kwa kila hatua ili uchaguzi ufanyike kwa utaratibu na mshindi atangazwe hakutakuwa na shida.

Ni mgombea anaeonekana kajipanga vyema kwa kila hatua ya uchaguzi, anakuambia tofauti yake yeye na wagombea wa vyama vya upinzani waliopita ni kuwa hawakuwa na mawakala wa kutosha nchi nzima ila yeye kajipanga vya kutosha hivyo atahakikisha kura zake zinalindwa na kutangazwa.

Sio mgombea mnyonge. Ni mtu anaejiamini sana na mpigania haki za wanyonge. Historia inambeba tangu akiwa ni wakili wa kawaida kabisa ametumia nafasi yake kupambania haki za wanyonge huko Tarime Nyamongo wanajua vizuri lakini hata akiwa mbunge amekuwa akiipambania nchi kwa kufuata sheria ili iepukane na kesi pamoja na hasara ya kulipa fidia. Amejitolea kwa uwezo wake na fani yake kupambania nchi na watu wake.

Ni mwalimu mzuri sana anayevutia kumsikiliza; fuatilia mikutano yake ya kampeni hakika hutoki mtupu ndio maana anajizolea mamia na maelfu ya wasikilizaji. Anahakikisha wananchi wa Tanzania wanaelewa sheria na kuzielewa haki zao ila kupambania haki zao kwa wanaowanyima.

Aisee ni mengi ya kuandika lakini nisiwanyime nanyi mchangie juu ya ubora wa mgombea huyu ambaye mimi nimemuweka namba moja.

Wasalamu!
 

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
693
1,000
Nyerere alihitimisha kitabu chake cha UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA kwa shairi Ole wake Tanzania Tusipoisaidia nifanyalo nimeliweza kushauri na kuonya nimeishatoka kitini zaidi nifanye nini????

Watanzania tumepewa Hii Lulu ya Tundu Lisu tumchague na tumuombee kwa Mungu maombi ya kishindo.

Tumepata mgombea urais Bora sana kuwahi kutokea Tanzania na Africa kwa ujumla.Tusijefanya makosa tena y Kuchagua jiwe mwenye utawala wa.
UDikteta.
UKatili,umtekaji,kuminya uhuru wa kutoa maoni,kuzui mikutano ya kisiasa.

Tumchague huyu Mzalendo anayejali Raia wa Tanzania, Mpenda Haki maendeleo utuna Umoja wa watanzania.

Nyerere alitamani kuwa na nchi yenye vijana jasiri wasio na woga wenye kuhoji na kupiga vita uonevu sio vijana wa ndio mzee.

MCHAGUENI LISSSU 2020.
# NI YEYE
 

Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,429
2,000
Hakika ni Mgombea Bora .... Tena ni Kizazi cha BORN FREE (Baada ya Uhuru). Yaani anapambana watu zaidi ya 5 kwa wakati moja halafu anawagalagaza wote. Magufuli, Majaliwa, Samia, Pinda, Kikwete, Mzee Makamba na sasa Mahela aliyeongezeka kwenye team!!
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,086
2,000
Picha la kuogofya
IMG_20200918_200218.jpg
 

Mchokozi wa mambo

Senior Member
Mar 27, 2014
100
225
kwanini nani asiyewajua CHADEMA kuwa kwenye social media mpo kila kona kuhaha ili kuwakamata vijana maana ndo watumiaji wakubwa wa social media.

hii kampeni haitazaa matunda jiandaeni kwa mambo mengine ila Ikulu ni jambo gumu sana kumuangusha Magufuli.

najua wapo mtanikosoa lakini ndo uweli mchungu Lissu hatoboi na baada ya hapo ajiandae kuporomoka kisiasa maana CHADEMA ni mwiko kwa mtu mwingine kuwa maarufu zaidi ya MBOWE
 

Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
9,700
2,000
Habari kwenu waungwana.

Tangu nimekuwa nikifuatilia siasa za nchi hii kwa vipindi kadhaa vya chaguzi kuu. Hapa ni kwa kipindi ambapo sikuwepo ila kwa njia ya masimulizi ya kihistoria na vile vipindi ambavyo nimekuwa nikishuhudia kwa macho na masikio yangu hasa baada ya kuwa na uchaguzi wa vyama vingi 1995 hadi leo hii....
We akili zako sawa na za ng'ombe tu! kuna mtu alimfikia mrema idadi ya watu wewe?
 
Jul 1, 2020
43
125
Kwa kweli nakiri mmetulemea wiki hizi mbili, lakini sisi tuna maarifa mengi. Ngoja tuanze raundi ya tatu ndiyo mtajua sisi ni magwiji w siasa za Afrika!
 

MEXICANA

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
1,321
2,000
Ukiona watu wanatumia nguvu nyingi kumpamba mtu ujue hapo kuna ualakini.
Nchi hii haiwezi kutawaliwa na mbeligiji
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
10,538
2,000
Nikiri kusema wazi kuwa, hapajatokea Mgombea wa Urais wa Tanzania mwenye uwezo wa ajabu kama alivyo huyu mwamba Tundu A Lissu.

Hakika hilo halina ubishi baada ya kusoma makala yako bora na pia kufuatilia kampeni za Tundu Lissu TunduLissu2020

CHADEMA wamejipanga vizuri sana na ndiyo maana tunaona 'mawenge' kambi ya CCM Mpya mpaka Tume ya Uchaguzi na Vyombo Vingine wakikimbizana kujaribu kuzuia tufani kuu ya inayobeba kimbunga cha UHURU, HAKI na MAENDELEO YA WATU

Video: TUNDU LISSU ANAFANYA MDAHALO NA WAANDISHI MWANZA 26/09/2020
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom