Ndugu lawama......mnao huko kwenu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugu lawama......mnao huko kwenu?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Saint Ivuga, Jul 30, 2011.

1. Saint Ivuga

Saint Ivuga JF-Expert Member

#1
Jul 30, 2011
Joined: Aug 21, 2008
Messages: 39,525
Likes Received: 19,945
Trophy Points: 280
Jamani hili neno ndugu lawama kila mtu anaweza kulitafsiri kivyake lakini kwa mimi ni wale ndugu ambao hawaridhiki hawataki kufanya kazi wao kutwa kucha ni kulalamika tu na kufuatilia mienendo yako..... ndugu unataka kumsomesha unamwambia nakulipia kila kitu kuanzia ada na mambo mengine anaenda shuleni anacheza cheza hadi anafukuzwa au anafeli,, wengine ambao ni wakubwa kwako ......wao kazi ni moja tu kupiga mizinga maro oo unaoa lini.... mara umeoa mke mbaya ... mara oo umenunua nini..mara utakuja kulogwa mara wengine wamekutafutia mganga wa kienyeji.. nani anawaambia kuwa kila mtu anaishi kwa nguvu za giza?........ jamani hawa ndugu lawama nadhani hata nyie mnao au wewe ni mmoja wapo
nawakilisha ,.....

2. The Boss

The Boss JF-Expert Member

#2
Jul 30, 2011
Joined: Aug 18, 2009
Messages: 37,822
Likes Received: 22,467
Trophy Points: 280
ukiamua hakuna ndugu wa kukubabaisha,hawathubutu

mimi nyumbani kwangu hakuna ndugu anaekuja bila taarifa.....

wala kuniletea shida yake bila kutafakari mara mbili

si entertain ujinga kabisa........

3. Saint Ivuga

Saint Ivuga JF-Expert Member

#3
Jul 30, 2011
Joined: Aug 21, 2008
Messages: 39,525
Likes Received: 19,945
Trophy Points: 280
hahahha...hapo sasa si ndio unatafuta ugomvi na ukoo mzima?@boss

4. The Boss

The Boss JF-Expert Member

#4
Jul 30, 2011
Joined: Aug 18, 2009
Messages: 37,822
Likes Received: 22,467
Trophy Points: 280
wewe chunguza kwenu utagundua ukoo
ukishakuchukulia mwehu hivi,hawakusumbui kabisa....

ni bora wakuone mwehu ili uishi kwa amani......

na mambo ya ndugu yalivyo...ni kuwa
kuna watu huwa wanapendwa na ndugu tu,hata kama hawana makubwa
ya kuwafanyia hao ndugu....
na kuna watu huwa hata ufanye nini,malalamiko hayaishi.....
so bora kukaa mbali na ndugu....

5. Viper

Viper JF-Expert Member

#5
Jul 30, 2011
Joined: Dec 21, 2007
Messages: 3,665
Likes Received: 44
Trophy Points: 145
mkuu hao hawakosekani... utawafanyia kila kitu , they will screw it up ! alafu wanaanza kukudondoshea lawama kibaoo! wanaboa ile mbaya! ndio maana sometimes nawa ignore ... ingawa wanapaka unaringa ...

6. Gaga

Gaga JF-Expert Member

#6
Jul 30, 2011
Joined: Jan 6, 2011
Messages: 4,565
Likes Received: 20
Trophy Points: 135
Mie napenda sana kusaidia ndugu zangu, huwa naona huruma sana lakini hawa ndugu ambao sio tumbo moja huwa na wivu sana aisee,hata umsaidie vipi ataleta za kuleta tu,huwez amini unampeleka ndugu ako nje kusoma unamuomba akija aje na aina fulani ya perfume anamtumia msg mama ake kulalamika, then anakosea inakuja kwako, ungekuwa wewe ungejisikiaje,unakaa kimya bila kulalamika anaamua kuja nayo, then kuondoka anakuja tena kuomba pesa,hii ipo sanasana unafanyaje coz roho mbaya huna unampa tu,ila sasa nahisi nimejifunza kitu fulani,hata ujifanye mwema kiasi gani bado watakutafuta wakuchomekee kidole mat,,,,,

7. The Boss

The Boss JF-Expert Member

#7
Jul 30, 2011
Joined: Aug 18, 2009
Messages: 37,822
Likes Received: 22,467
Trophy Points: 280
sasa si ukichomoe tu hiko kidole...au una enjoy?????? lol

8. Gagurito

Gagurito JF-Expert Member

#8
Jul 30, 2011
Joined: Feb 11, 2011
Messages: 5,610
Likes Received: 25
Trophy Points: 135
Ndugu wa namna hii wanauzi kweli, wao hata uwafanyie nin shukrani hawana, kukicha ni minong'ono na malalamiko yasiyo na tija. Hovyo sana hawa!

9. tindikalikali

tindikalikali JF-Expert Member

#9
Jul 30, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 4,883
Likes Received: 96
Trophy Points: 135

aaah hata huku kwetu wapo.

10. Gaga

Gaga JF-Expert Member

#10
Jul 30, 2011
Joined: Jan 6, 2011
Messages: 4,565
Likes Received: 20
Trophy Points: 135

wengine tumeumbwa na huruma yaani mie nina matukio na ndugu zangu mpaka aibu, unajua sie ni mayatima yaani mie na jamaa tangu miaka mingi tu kwa hiyo tunajua kabisa ni lazima kusaidia ndugu, yaani hata usipomsaidia atakuja kwako kula kila siku,kuna wakati unajikausha lakini inabidi tu ujitutumue

11. The Boss

The Boss JF-Expert Member

#11
Jul 30, 2011
Joined: Aug 18, 2009
Messages: 37,822
Likes Received: 22,467
Trophy Points: 280
trust me
utakapokuwa na shida
utashangaa wale ambao hujawahi kuwasaidia
wanavyojitolea kukusaidia
utashangaa wale unaofikiri ndio wakusaidie
watakavyo kaa pembeni....
life bwana....

12. tindikalikali

tindikalikali JF-Expert Member

#12
Jul 30, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 4,883
Likes Received: 96
Trophy Points: 135
mh mada imenigusa bandugu, kwani nahisi naelekea huko kwenye kutupiwa lawama zisizo na msingi. Nikikumbuka maisha yangu ya shule, ni wachache walioweza kunisaidia tena wale wenye uwezo kiduchu, kuna waliokuwa mbali nami sikujali nikakomaa na shule, nashukuru Mungu sikuwahi feli hata siku moja. Hivi majuzi nime-graduate, toka waliposikia nipo chuo kikuu salamu zikaanza na wengine wakijisifu, "huyu mwanangu kabisa", tisa kumi sasa wameanza kunihubiria et nisioe mapema, kwani sitowasaidia na maneno mengine mengi.

13. Saint Ivuga

Saint Ivuga JF-Expert Member

#13
Jul 30, 2011
Joined: Aug 21, 2008
Messages: 39,525
Likes Received: 19,945
Trophy Points: 280
Gaga pole sana mtu wangu.. hapo nimekupata manake unaweza kukuta baadhi ya hao ndugu wengine walikusaidiaga wakati unasoma sasa watoto wao nao wanakuamgalia huna jinsi ..najua sana hii situation

14. Likwanda

Likwanda JF-Expert Member

#14
Jul 30, 2011
Joined: Jun 16, 2011
Messages: 3,854
Likes Received: 45
Trophy Points: 145
Vituko vya ndugu ni vingi sana, ila tunatakiwa kuwavumilia na kuwaambia makosa yao kwa umakini sana. Simuungi mkono ndugu yangu Boss, maana kuna leo na kesho, mtu unaweza kuwanyanyasa ndugu zako kutokana na visa vyao baadaye wakawa msaada mkubwa kwako hivyo tuvumiliane maana binadamu wote si sawa.

15. p

pori Member

#15
Jul 30, 2011
Joined: Mar 12, 2010
Messages: 86
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Asante sana Boss maana hilo nalo neno! mijitu mingine yaani ndugu asilogwe kuwa na ka-cheo au uwezo fulani, inakuwa nongwa! asubuhi sana mapema wako majumbani mwa watu hata aibu hawana. ukiangalia wana viungo timilifu mwilini lak hawaishi kuomba omba. hawa ndio wale wanadiriki kupokonya mali zoote endapo mwenza mmoja anaaga dunia. wakati wa karne hii si wa kutegemeana kwa percent 100 kwa mia kwa ndugu. dawa yao ni hiyo tu ya kuwatimua

16. Gaga

Gaga JF-Expert Member

#16
Jul 30, 2011
Joined: Jan 6, 2011
Messages: 4,565
Likes Received: 20
Trophy Points: 135

Nashukuru Mungu nimesoma kwa pesa zetu yaani shule nimeanzia certificate nikiwa nishaolewa hakuna wa kujiitutumua kanisomesha.ila karibu najikwamua, sasa karibia najivua gamba ndugu jama ni huwa wanarudisha sana maendeleo ya familia ila tunafanyaje,ukikumbuka kwenu wazazi nao walikuwa wanaishi na ndugu, kuna binamu yangu nimejua sio dada yangu kabisa wakati niko form one

17. Saint Ivuga

Saint Ivuga JF-Expert Member

#17
Jul 30, 2011
Joined: Aug 21, 2008
Messages: 39,525
Likes Received: 19,945
Trophy Points: 280
mkuu hii dawa mbona naona kama ni kali sana?si unajua kuna leo na kesho?

18. FiQ

FiQ JF-Expert Member

#18
Jul 30, 2011
Joined: Feb 11, 2011
Messages: 479
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
kuna ndugu na ndugu jaman, ndugu wa tumbo moja mm cwez kumuacha no matter nina na mali kiasi gani bt still nakumbuka magumu tuliyopitia.

Mf. Inaweza kutokea umepata matatizo makubwa na una hali mbaya kifedha mpaka kiafya ndugu wengine wanaweza kuku kimbia bt ndugu wa tumbo moja he/she can't. Am talk frm ma own experience.

19. Saint Ivuga

Saint Ivuga JF-Expert Member

#19
Jul 31, 2011
Joined: Aug 21, 2008
Messages: 39,525
Likes Received: 19,945
Trophy Points: 280
offcourse ndugu wa tumbo moja hata ukimuacha lazima nafsi ikusute tu....

20. Desidii

Desidii JF-Expert Member

#20
Jul 31, 2011
Joined: Oct 2, 2007
Messages: 1,212
Likes Received: 5
Trophy Points: 135
Ha ha ha wapo sana unawasaidia wakati unazo ngoja uishiwe hao hao ndo wanaanza si alikuwa anaringa mwone alivokonda gari kauza, nyumba kauza hana kitu...kweli ndugu lawama

Loading...