Joseph Roman Selasini (MB): Naibu Spika; Kufuru uliyofanya dhidi ya Ukristo haivumiliki

Picha ni edited

Mkuu mbona unaleta photoshop hapa Jf

Unatengeneza picha yako na kuedit

Shameless, Jipange upya umechemka

Mwambie aliyekutuma ashindwe
Nimeamua kuweka picha hii baada ya kumwona Makamu mwenyekiti wa Chadema Kanda Ya Kaskazini Kaka yangu Joseph Selasini Mbunge wa Rombo akihusishanisha tukio iliyofanyika Mbeya ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakifanya Igizo la kubeba jeneza yenye bendera ya chadema ikiwa na msalaba.
Jambo lililomfanya Kaka Joseph Selasini kuhusisha tukio ilo la Mbeya na kudhalilisha Ukristo kwakuwa ilihudhuria na Naibu Spika Dr Tulia Akson.
Ndugu yangu Selasini katika andiko lake iliyobandikwa kwenye kurasa la social media ya Chadema kanda ya Kaskazini amelaumu sana Naibu Spika kushiriki kudhalilisha Ukristo kutokana na tukio Ilo.
Nikiri kuwa kaka yangu Joseph Selasini nimefahamiana naye muda mrefu wakati huo akiwa Katibu wa Vijana Taifa wa NccrMageuzi mwenyekiti wake akiwa Msafiri Mtemelwa ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu mkuu wa Act Wazalendo.
Miye nikiwa ccm mwaka 1994 yeye na wenzanke akina Mosena Nyambabe, james Mbatia, Hemed Sabula, Evod Mmanda, akina Chitanda wakiwa NccrMageuzi sisi tulikuwa wadogo zao ktk siasa akina mbatia wakiwa Udsm sisi Ndiyo tunamaliza sekondari ukweli Selasini ni mwanasiasa mwenye Jaziba asiyetumia akili hata kidogo.
Nirudi kwenye picha hii hapa chini
Ili tukio iliyotokea katika kata ya Iyela mkoani Mbeya kwenye maandamano mwaka 2013/2014 na kupokelewa na aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema DR Wilbroad Peter Silaa na aliyekuwa mwenyekiti wa Bavicha Taifa Tanzania Mh John Heche katika Ile vuguvugu ya akina Samson Mwigamba na Zitto Kabwe.
Kipindi icho kaka Joseph Selasini alikuwa Mbunge chadema lakini hakuona kama ni Udhalilishaji wa Ukiristo Leo kwakuwa imefanywa na mtu wasiyempenda anataka kuchonganisha Imani ya Ukristo na siasa zetu.
Ni vyema sisi wafuatiliaji wa mambo ya siasa kukemea tabia hii ya viongozi wa chadema kutaka kuonyesha Umma kuwa wanaonewa hata kama hayo mambo wameanzisha wenyewe.View attachment 1213819
 
Unachotetea ni kipi? Kwa nafasi aliyonayo Tulia hakupaswa kushiriki kwenye ule upuuzi! Amekuwa muhuni siku hizi kisa ubunge 2020!
 
Na hii Nini,hivi machadema Yana akili gani hayana heshima hata kwa bosi wao. Chadema achenj siasa za hovyo msitufanye tuwapuuze zaidi
tapatalk_1569204398209.jpeg
 
Huyu Selasini naye hata ukiristo haujui. Ameongea kana kwamba Wakristo Msalaba ni Mungu wao. Wakristo tunaamini Ukombozi Wa Yesu Kristo kwa kufa kwake msalabani hatuuabudu Msalaba. Alichokifanya Selasini ni kutaka kuiombea CHADEMA huruma ya Wakristo kwa kutaka kuwaaminisha kuwa Tulia amekosea. Wakriso nao siyo wajinga kiasi hicho na walimuelewa sana Dkt. Tulia
 
Ina maana Chadema mnaukana msalaba au jeneza maana hivyo ni vitu viwili tofauti.

Ila yawezekana huyo Tulia aliutumia msalaba bila kujua atendalo labda ni msabato au mpagani .......akitubu asamehewe bure!
Ni Wasabato wa aina gani wasioielewa falsafa ya Msalaba?
 
Mhe Tulia Akson: Naibu Spika kwa hili sintanyamaza. Umekwenda mbali sana.
Kwa dhihaka hii dhidi ya msalaba sitatulia. Eti unaizika Chadema Mbeya. Kwa kutumia msalaba na akinamama wakilia Kinyakyusa. Dhihaka yako kwa CHADEMA sitaizungumzia hapa, ila najua wazi kwamba umma unakushangaa baada ya kuona jinsi unavyofanya vitendo vifanywavyo na wale waliolewa madaraka kupitiliza.

Tulia:
Umeidharau na kuidhalilisha alama ya msingi ktk Ukristu. Umekufuru umebeza na kuutukana msalaba.

Wewe ni Mkristu unajua Wakristu tunaamini msalaba kama alama au ishara ya ukombozi wetu dhidi ya dhambi na mauti.
Ni chombo muhimu cha imani ktk Ukristo.
Utengenezwe kwa dhahabu au chuma. Uwe wa mbao, matete au majani. Popote unapotumika hata kama ni dhaifu kiasi gani Mkristu anakumbuka msalaba wa Bwana Yesu. Anakumbuka mateso ya Mkombozi na damu ya thamani kuu iliyomwagwa kwa ajili yetu na ulimwengu mzima.

Dr Tulia Ackson Mwansasu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umekosea *"omba radhi kwa Wakristu na toba kwa Mungu"* kabla laana ya Mungu haijakushukia pamoja na chama chako na wote mlioshiriki.

Huwezi kuutafuta ubunge kwa kuwatukana wakristu. Kwa kudhihaki wanachokiamini. Huo ni ushahidi wa kukosa mvuto na kijiingiza kwenye kuabudu maigizo ya kipumbavu. Sikutegemea hili kwako kwa usomi wako na kwa cheo ulicho nacho.

Toka hadharani uombe toba usamehewe. Vinginevyo Wakristu wote watakuinukia kuutetea Msalaba wa Kristo. Tulipobatizwa tuliapa kuitetea imani. Tutafunga tutaomba ili majeshi ya mbinguni yashughulike na dhihaka hii.
Kwa hili hatutasita wala hatuogopi wasiojulikana. "Kwa hili kufa ni faida."
Chezeeni vyote sio imani na heshima ya Wakristu ktk msalaba kwa kuwa bila msalaba yaani " mateso, kifo cha msalaba na hatimae ufufuko, hakuna Ukristu."

*_“alifutilia mbali ile hati ya deni iliyokuwa inatukabili na masharti yake, na kuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani. Huko Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake.”_* Wakolosai 2:14-15 BHN

Joseph Roman Selasini (MB)
Huyu anaye mdhihaki Mungu, Amedhoofu kiafya, kiimani na kisiasa. Tayari hasira za Mungu ziko juu yake!
 
Nchi hii ina wapumbavu wengi,usomi ni geresha tu...nashangaa mnashtushwa na hili, kwani hili limezidi ujinga na ukandamizaji wanaofanya bungeni kama viongozi?
 
Acha upuuzi. Ni mara ngapi Chadema wamefanya matukio kama haya? Mnachotakiwa kuhangaikabnacho ni kuzuia kifo cha chama chenu badala ya kuhangaika na Dr. Tulia
Mhe Tulia Akson: Naibu Spika kwa hili sintanyamaza. Umekwenda mbali sana.
Kwa dhihaka hii dhidi ya msalaba sitatulia. Eti unaizika Chadema Mbeya. Kwa kutumia msalaba na akinamama wakilia Kinyakyusa. Dhihaka yako kwa CHADEMA sitaizungumzia hapa, ila najua wazi kwamba umma unakushangaa baada ya kuona jinsi unavyofanya vitendo vifanywavyo na wale waliolewa madaraka kupitiliza.

Tulia:
Umeidharau na kuidhalilisha alama ya msingi ktk Ukristu. Umekufuru umebeza na kuutukana msalaba.

Wewe ni Mkristu unajua Wakristu tunaamini msalaba kama alama au ishara ya ukombozi wetu dhidi ya dhambi na mauti.
Ni chombo muhimu cha imani ktk Ukristo.
Utengenezwe kwa dhahabu au chuma. Uwe wa mbao, matete au majani. Popote unapotumika hata kama ni dhaifu kiasi gani Mkristu anakumbuka msalaba wa Bwana Yesu. Anakumbuka mateso ya Mkombozi na damu ya thamani kuu iliyomwagwa kwa ajili yetu na ulimwengu mzima.

Dr Tulia Ackson Mwansasu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umekosea *"omba radhi kwa Wakristu na toba kwa Mungu"* kabla laana ya Mungu haijakushukia pamoja na chama chako na wote mlioshiriki.

Huwezi kuutafuta ubunge kwa kuwatukana wakristu. Kwa kudhihaki wanachokiamini. Huo ni ushahidi wa kukosa mvuto na kijiingiza kwenye kuabudu maigizo ya kipumbavu. Sikutegemea hili kwako kwa usomi wako na kwa cheo ulicho nacho.

Toka hadharani uombe toba usamehewe. Vinginevyo Wakristu wote watakuinukia kuutetea Msalaba wa Kristo. Tulipobatizwa tuliapa kuitetea imani. Tutafunga tutaomba ili majeshi ya mbinguni yashughulike na dhihaka hii.
Kwa hili hatutasita wala hatuogopi wasiojulikana. "Kwa hili kufa ni faida."
Chezeeni vyote sio imani na heshima ya Wakristu ktk msalaba kwa kuwa bila msalaba yaani " mateso, kifo cha msalaba na hatimae ufufuko, hakuna Ukristu."

*_“alifutilia mbali ile hati ya deni iliyokuwa inatukabili na masharti yake, na kuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani. Huko Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake.”_* Wakolosai 2:14-15 BHN

Joseph Roman Selasini (MB)
 
Huyu Selasini naye hata ukiristo haujui. Ameongea kana kwamba Wakristo Msalaba ni Mungu wao. Wakristo tunaamini Ukombozi Wa Yesu Kristo kwa kufa kwake msalabani hatuuabudu Msalaba. Alichokifanya Selasini ni kutaka kuiombea CHADEMA huruma ya Wakristo kwa kutaka kuwaaminisha kuwa Tulia amekosea. Wakriso nao siyo wajinga kiasi hicho na walimuelewa sana Dkt. Tulia
Ni mpangilio wa maneno tu ila wote mnaongelea kitu kimoja. Hakuna Ukristu bila msalaba. Bila msalaba ni Islam, hinduism, bahai, na atheism. Tofauti kati ya dhehebu na dhehebu kwa wakristu ni namna wanavyo utumia msalaba.

Jiulize kuna alama ya kwanza ya kanisa unapotembea barabarani ni nini?
 
Vipi na wale wanaokwenda na majeneza pamoja na misalaba kwenye mechi ya watani wa jadi simba na yanga?

Kiongozi wa ngazi yake sio wa kuiga maovu/ujinga . Anategemewa kukosoa na kuelimisha
 
Tulia Ackson ana sura mbaya sana kama mamba, angalao angejitahidi awe na tabia nzuri kuficha hilo lisura lake libaya!
 
Tamaa ya ubunge wa Mbeya mjini na kutokukubalika kumemfanya aingie kwenye ushirikina na uchawi bila aibu mchana kweupe, ubunge unatafutwa jamani.
 
Mimi nilijua kaenda kuhani msiba wa Chadema!! pale hakuna msiba wala nini? Duh kweli Tulia uenda akili zimeanza kumluka. Acha tu Mungu atajitetea mwenyewe.
Laana na mapigo lazima yamfuate Tulia na wanaCCM wa Mbeya au popote walioshabikia ule uhuni wa kudhihaki imani ya kikristo. Ajali iliyotokea jana Mbeya na kuua wanaCCM wa Mbeya huenda ni kionjo tu cha mapigo zaidi yatakayofuata.
 
Wa kumsahe ni Mungu sio sisi!!
Ina maana Chadema mnaukana msalaba au jeneza maana hivyo ni vitu viwili tofauti.

Ila yawezekana huyo Tulia aliutumia msalaba bila kujua atendalo labda ni msabato au mpagani .......akitubu asamehewe bure!
 
Siungi mkono ile drama iliyofanywa pale.
Lakini kuna uhusiano wowote uliopo kati ya msalaba na ukristo?
Naombeni majibu wajuvi wa hili.
 
Umekuja Kumtetea Watu Wanacholalamikia Ni Cheo Alichonacho Kama Spika Kufanya Mambo Ya Kiuni Kama Watoto Wa Udsm Au Wanywa Viroba Mtaani"
Sio kweli,Hoja ni kadhihaki.Hizo za cheo cha speaker unaleta Wewe. Ni siasa uchwara tu na zisizo na mwelekeo ndio maana leo hili la Speaker ni Agenda. Wale ni wafuasi, ulitala speaker akatae?
 
Back
Top Bottom