Ndugai: Vyombo vya habari vinawabeba wapinzani

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,803
1,863
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema anakerwa na tabia ya vyombo vya habari nchini kuwakosoa viongozi wa CCM na Serikali tu na kuwabeba wa vyama vya upinzani hata wanapokosea.

Amesema, viongozi wapinzani ni viongozi wa serikali watarajiwa, hivyo vyombo vya habari vina wajibu wa kuwakosoa kama ilivyo kwa viongozi wa serikali na chama tawala badala ya kuwabeba hata katika mamo ya wazi.

Aliyasema hayo katoka maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari Duniani jana jijini Dar.

Alisema umekuwa ni utamaduni wa waandishi wa habari kuwabeba wapinzani huku viongozi wa CCM na serikali wakikosolewa kutokana na utendaji wao.

"Hakuna jambo lisilokuwa na mwisho :clap2: na leo tukiwabana hawa na kuwaacha wanaotarajiwa kuwa viongozi, sio haki, lazima vyombo vya habari viangalie pande zote na kukosoa", alisema.

Alivitaka vyombo vya habari kubadilika na kuwa na mapenzi na nchi yao badala ya kushabikia wanasiasa na vyama vyao, kwani wanahabari wana nafasi kubwa ya kujenga jamii ama kuibomoa kama watakubali kutumika vibaya.

Kuhusu mahusiano kati ya BUnge na vyombo vya habari, Ndugai alisema, kwa muda mrefu yameendelea kuwa mazuri na kuahidi kuyadumisha.

SOURCE: NIPASHE (pg. 08)
DATE: MAY 04, 2012
 
Magamba Wabadilike, wawe na matendo masafi halafu waone vyombo vya habari vitakuwa upande gani. Ukweli ni kwamba jambo lolote geni (liwe zuri au baya) hiyo ni habari. Matendo mabaya yanayofanywa na baadhi ya viongozi wetu ndio yamewafikisha hapo hao waliopo madarakani. Naibu spika nendeni mkajipange.
 
Naona ni kuweweseka mbona kila siku wapinzani wanalalamika kuhusu TBC1 je hilo analisemeaje?
 
anakimbiia kivuli chake huyu ,, hataweza kupingana na ukweli ina maana waandishi wadanganye ..? kama ccm wamehamwa watu waandike chdema ndio imehamwa?
huyu naye kashazoe siasa za kumtukuza ambazo zimeshapitwa na wakati
 
Yaani Waziri ashirikiane na Wahuni waanzishe kampuni za kihuni kwa ajili ya kutuibia, halafu rais aliyemteua yupo honeymoon Brazil wanabembe na Maximo, anataka vyombo vya habari viandike Waziri fulani ni Kiongozi bora na ni mfano wa kuigwa na bosi wake aliyemteua anastahili sifa!
 
Sina hakika kama alikimaanisha kweli alichokisema. Labda kama alimaanisha TBCCM kuwa inawabeba kina thithiemu SAWA!
 
Ni tatizo la kuzoea kupewa sifa kila siku, sasa mnapewa ukweli mnalalama!
 
Huyu Jamaa nafikiri anaongea bila kufikiria,

Kwanza yeye mwenyewe kwa asilimia kubwa hatendi haki bungeni sasa anategemea aandikwe vipi?
pili hawa anaowaita wapinzani tayari ni viongozi kwa taifa hili wanaongoza watu wengi sana hivyo sio kwamba wanaotarajiwa kuwa viongozi, hawa ni viongozi tayari, chukulia mtu kama Dr Slaa, Mbowe, Lipumba wewe unataka wawe viongozi mara ngapi?, Dr Slaa ni kiongozi wa watu wengi sana jamani!! tutazame uongozi kwa upana zaidi asifikiri kiongozi ni kuwa naibu spika tu.Narudia tena Dr Slaa ni kiongozi wetu akipotoka vyombo vya habari vitamwambia lakini haviwezi kumsingizia ikiwa bado hajapotoka.

Pia anatakiwa kukemea na vyombo vingine sio vya habari tu akemee Police, Mahakama, Usalama wa taifa na wengine wengi watende haki na sio kuegemea upande wa serikali tu.
 
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema anakerwa na tabia ya vyombo vya habari nchini kuwakosoa viongozi wa CCM na Serikali tu na kuwabeba wa vyama vya upinzani hata wanapokosea.

Amesema, viongozi wapinzani ni viongozi wa serikali watarajiwa, hivyo vyombo vya habari vina wajibu wa kuwakosoa kama ilivyo kwa viongozi wa serikali na chama tawala badala ya kuwabeba hata katika mamo ya wazi.

Aliyasema hayo katoka maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari Duniani jana jijini Dar.

Alisema umekuwa ni utamaduni wa waandishi wa habari kuwabeba wapinzani huku viongozi wa CCM na serikali wakikosolewa kutokana na utendaji wao.

"Hakuna jambo lisilokuwa na mwisho :clap2: na leo tukiwabana hawa na kuwaacha wanaotarajiwa kuwa viongozi, sio haki, lazima vyombo vya habari viangalie pande zote na kukosoa", alisema.

Alivitaka vyombo vya habari kubadilika na kuwa na mapenzi na nchi yao badala ya kushabikia wanasiasa na vyama vyao, kwani wanahabari wana nafasi kubwa ya kujenga jamii ama kuibomoa kama watakubali kutumika vibaya.

Kuhusu mahusiano kati ya BUnge na vyombo vya habari, Ndugai alisema, kwa muda mrefu yameendelea kuwa mazuri na kuahidi kuyadumisha.

SOURCE: NIPASHE (pg. 08)
DATE: MAY 04, 2012

hapo kwenye red bora umejitambua
 
kama wapinzani ndio wanasanua madili huko ndani selikalini wachuniwe tu na vyombo vya habari!! wasiwamulike!!!!!!!!! Kazi nzuri wanahabari
 
Ila posti nzito baba! uone kwamba vijana bado mchujo mzuri unahitajika kabla ya kuwa nyadhifa.Uspika unahitaji washauri wazuri, sasa wengi wakiwa na maskendo inakuwa ngumu
 
Vyombo vya habari haviwapendelei wapinzani ila vinaandika habari ambazo zitauza magazeti.

Uwe mpinzani uwe CCM ukipata kichwa cha habari kinasema "Slaa aisambaratisha CCM Arumeru" lazima ununue gazeti kujua kulikoni. Ukishanunua gazeti unakuta Slaa amefungua tawi la wakereketwa wa Chadema na kugawa kadi 15
 
Ndugai hakupaswa kabisa kuwa msemaji wa vyombo vya habari, wala kuvisema katika siku hii yenye jina la UHURU WA VYOMBO VYA HABARI. Hapa ni kama mtunza bustani kumsemea mpishi.

Zile enzi walizokuwa wanatamba na Magazeti yao ya Chama na RTD zimekwisha. Siku za Shamba la Wanyama (Tumsifu kiongozi wetu) zimekwisha. Wananchi wameamka na wamechoka kusifu, wamechoshwa na wapenda sifa. Yeye kama CCM aviagize tu vyombo vya habari vya CCM vitawasifu wanavyotaka wao, lakini sio kuvitaka vyombo vyengine HURU.

Pamoja na hayo, sekta ya habari sasa imekuwa biashara yenye upinzani. Watu wananunua habari wanayoipenda siyo wanayotakiwa waipende.
 
Aseme wamebebwa kwa lipi..
Mfano mzuri ni kesi ya mpendazoe/mahanga ambapo vyombo vya habari vilikuwa vinatoa habari za mwenendo wa kesi kwa kuegemea upande mmoja, kiasi kwamba kesi ambayo haikuwa na hoja kabisa kuonekana kwa jamii kwamba mahanga lazima ashindwe. Huu si upendeleo kwa upinzani?
 
Back
Top Bottom