Jacob Kalangula
New Member
- May 3, 2012
- 4
- 1
Nyombo vya habar viko sawa ni mtazamo wake tu huo.
Always media afflict the confortable(SSM) and comfort the afflicted( Watanzania wonyonge)
Nyombo vya habar viko sawa ni mtazamo wake tu huo.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema anakerwa na tabia ya vyombo vya habari nchini kuwakosoa viongozi wa CCM na Serikali tu na kuwabeba wa vyama vya upinzani hata wanapokosea.
Amesema, viongozi wapinzani ni viongozi wa serikali watarajiwa, hivyo vyombo vya habari vina wajibu wa kuwakosoa kama ilivyo kwa viongozi wa serikali na chama tawala badala ya kuwabeba hata katika mamo ya wazi.
Aliyasema hayo katoka maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari Duniani jana jijini Dar.
Alisema umekuwa ni utamaduni wa waandishi wa habari kuwabeba wapinzani huku viongozi wa CCM na serikali wakikosolewa kutokana na utendaji wao.
"Hakuna jambo lisilokuwa na mwisho :clap2: na leo tukiwabana hawa na kuwaacha wanaotarajiwa kuwa viongozi, sio haki, lazima vyombo vya habari viangalie pande zote na kukosoa", alisema.
Alivitaka vyombo vya habari kubadilika na kuwa na mapenzi na nchi yao badala ya kushabikia wanasiasa na vyama vyao, kwani wanahabari wana nafasi kubwa ya kujenga jamii ama kuibomoa kama watakubali kutumika vibaya.
Kuhusu mahusiano kati ya BUnge na vyombo vya habari, Ndugai alisema, kwa muda mrefu yameendelea kuwa mazuri na kuahidi kuyadumisha.
SOURCE: NIPASHE (pg. 08)
DATE: MAY 04, 2012
Huyu Jamaa nafikiri anaongea bila kufikiria,
Kwanza yeye mwenyewe kwa asilimia kubwa hatendi haki bungeni sasa anategemea aandikwe vipi?
pili hawa anaowaita wapinzani tayari ni viongozi kwa taifa hili wanaongoza watu wengi sana hivyo sio kwamba wanaotarajiwa kuwa viongozi, hawa ni viongozi tayari, chukulia mtu kama Dr Slaa, Mbowe, Lipumba wewe unataka wawe viongozi mara ngapi?, Dr Slaa ni kiongozi wa watu wengi sana jamani!! tutazame uongozi kwa upana zaidi asifikiri kiongozi ni kuwa naibu spika tu.Narudia tena Dr Slaa ni kiongozi wetu akipotoka vyombo vya habari vitamwambia lakini haviwezi kumsingizia ikiwa bado hajapotoka.
Pia anatakiwa kukemea na vyombo vingine sio vya habari tu akemee Police, Mahakama, Usalama wa taifa na wengine wengi watende haki na sio kuegemea upande wa serikali tu.
Magamba Wabadilike, wawe na matendo masafi halafu waone vyombo vya habari vitakuwa upande gani. Ukweli ni kwamba jambo lolote geni (liwe zuri au baya) hiyo ni habari. Matendo mabaya yanayofanywa na baadhi ya viongozi wetu ndio yamewafikisha hapo hao waliopo madarakani. Naibu spika nendeni mkajipange.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema anakerwa na tabia ya vyombo vya habari nchini kuwakosoa viongozi wa CCM na Serikali tu na kuwabeba wa vyama vya upinzani hata wanapokosea.
Amesema, viongozi wapinzani ni viongozi wa serikali watarajiwa, hivyo vyombo vya habari vina wajibu wa kuwakosoa kama ilivyo kwa viongozi wa serikali na chama tawala badala ya kuwabeba hata katika mamo ya wazi.
Aliyasema hayo katoka maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari Duniani jana jijini Dar.
Alisema umekuwa ni utamaduni wa waandishi wa habari kuwabeba wapinzani huku viongozi wa CCM na serikali wakikosolewa kutokana na utendaji wao.
"Hakuna jambo lisilokuwa na mwisho :clap2: na leo tukiwabana hawa na kuwaacha wanaotarajiwa kuwa viongozi, sio haki, lazima vyombo vya habari viangalie pande zote na kukosoa", alisema.
Alivitaka vyombo vya habari kubadilika na kuwa na mapenzi na nchi yao badala ya kushabikia wanasiasa na vyama vyao, kwani wanahabari wana nafasi kubwa ya kujenga jamii ama kuibomoa kama watakubali kutumika vibaya.
Kuhusu mahusiano kati ya BUnge na vyombo vya habari, Ndugai alisema, kwa muda mrefu yameendelea kuwa mazuri na kuahidi kuyadumisha.
SOURCE: NIPASHE (pg. 08)
DATE: MAY 04, 2012
Naona ni kuweweseka mbona kila siku wapinzani wanalalamika kuhusu TBC1 je hilo analisemeaje?