omtiti
JF-Expert Member
- Jun 19, 2019
- 1,022
- 1,590
IFIKE WAKATI MSIOJIELEWA, MJIELEWE!
Ukiipenda Demokrasia, pende na Sheria.
Ndugai Yuko Sahihi!
Na:George Kabadi.
==================================
Ni kosa kubwa kuiruhusu akili ya mwanasiasa ifanye kazi, kama mbaadala wa akili yako. Miaka ya hivi karibuni, limeibuka vimbi kubwa la watu wanaojiita wanaharakati kuwatetea watu wanaopenda kusemewa, matatizo yao na watu wengine.
:-Hili ni kosa kubwa katika kufikri.
»Katika ubinadamu wangu, natoa pole kwa MH Tundu Lissu, kwa utenguzi wa ubunge wake ulio-fanywa na kanuni na sheria za bunge.
»Katika sheria za nchi yangu, natoa pongezi kwa Spika Job Ndugai kwa kufuata demokrasia katika kutenda mambo kwa sheria, bila kutumia mihemuko ya ki-binadamu.
Najua ya kuwa fikra za watanzania wengi, hasa wanaoishi kwa fikra za bendera hawaezi kutambia matakwa ya sheria inasema nini katika hili.
Wengi tumejikita kusema nchi haina demokrasia, wakati demokrasia inapofuatwa hunalalamika, hakuna demokrasia. Je tunataka demokrasia ipi haswa ifuate?
Tutambue demokrasia huambatana na utekelezwaji wa sheria, bila kujali kakatwa nani!
:-Ujinga wa walio wengi hufikri nchi huongozwa kwa mihemko ya fikra za mtu binafsi.
»Rais:-Akitoa tamko vijana wa lumumba hulishadadia kana-kwamba ni sheria.
»Wapinzani:-Wakitoa tamko, vijana wa upinzani nao hulichukulia kama sheria.
Imefika wakati sasa, sheria ikifuatwa, tunalalamika.
Kutengulia kwa ubunge wa Tundu Lissu, ni tikwa la sheria.
Tuangalieni sheria inasema nini, tusiangalie Spika kasema nini!
Sheria ya nchi hii, haitungwi na Sipika Ndugai na mkewe, bali hutungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tusimulaumu Ndugai wakati yeye katekeleza matakwa ya sheria.
:-Uathirika wa kudharau sheria na kutii matamko ya viongozi, ni umekua kwa kasi. Ikiwa tumeamua kuishi kwa kutokufuata sheria, basi na tuishi wa kwa kufuata matamko ya viongozi wa vyama vya siasa, ambao matamko yao tunaona,ni bora kuliko sheria.
Sheria ni msumeno, tusiupangie msumeno sehemu ya kukata.
Kumlaumu Ndugai ni kukosa fikra mubadala!
#Acha Mawazo Mfinyanzi.
Kalamu Ya Mwebrania.
Na:George Kabadi.
0759 131 717