Ndugai hajaeleweka kwa watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugai hajaeleweka kwa watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Martoism, Aug 12, 2012.

 1. Martoism

  Martoism Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh, Rev. Peter Simon Msigwa mbunge wa Iringa mjini hivi majuzi kwa umahiri na umakini mkubwa akiwasilisha maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni kwenye hotuba ya wizara ya maliasili na utalii alieleza kwa mifano hai jinsi serikali ya awamu ya nne almaarufu "Magambaz government" ilivyoshindwa kusimamia, kutunza, kuendeleza na kuvuna utajiri wa maliasili zetu kwa ustawi na maendeleo ya jamii nzima ya watanzania. Huku mh, Msigwa akiongozwa na nukuu za viongozi mashuhuri duniani kama Churchil wa U.k , hayati baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanganyika na wanazuoni maarufu kama kawaida yake kwa kuwa Msigwa mara nyingi huwa hazungumzi na hadhara yeyote bila nukuu, Gafla Lukuvi (mb Isimani) akakasirishwa na udhaifu wa serikali yake ulivyokuwa ukianikwa wazi wazi akaomba kiti (Ndugai mb wa kongwa na Naibu spika) amzuie Msigwa kuendelea kuianika serikali , bila kificho huku akijaa jazba na hasira kali Ndugai aliiagiza serikali iwaonyeshe kambi ya upinzani kuwa si dhaifu, si legelege , haiwatumikii matajiri, haijazidiwa nguvu wala haishirikiani na majangili . Tujiulize sote hivi Ndugai anatuona watznia ni vipofu hatuoni?
   
Loading...