Ndugai bize na simu huku akiongoza bunge, ajabu kweli!

mosagane

Senior Member
Jul 24, 2012
122
25
Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo ameonekana kuwa bize na kuchati na simu yake ya mkononi huku akiwa anaongoza kikao cha bunge.

Ndugai ameonekana akitumia muda mwingi kubofya bofya simu yake bila kuwa makini na nini anachokiongoza.

Hii imekaaje wana JF, kiuwajibikani na unyeti wa kiti chenyewe?

Source: Channel 10 - habari saa1
 
Hoja ikiletwa kwa kujadiliwa kwa umakini mkubwa wanao chat na waliolala wote wanastuka na kusema....ndiooooooooo na kupiga meza.....wanarudi kusinziaa na ku chat!!mwisho wao umekaribia!!
 
Akina Komba, Wassira , Sitta na wengineo wako bize kulala bungeni......Ndugai nae busy na simu .....kazi tunayo watanzania......wanaounga mkono hoja waseme ndiyo.............ndiyoooooooooooooooooooooooooooooooo hao ni wale waliosinzia ndio huwa wanaitika bila hata kujua hoja inayoungwa mkono......waliosema ndio wameshinda daaaaaah !
 
Ingekua mi ni spika ningepiga marufuku simu bungeni au ziwe zimezimwa sasa bora hiyo.. Kuna mbunge alipigwa picha anasafisha viatu vyake bungeni.. Hiyo iliniacha hoi ilikua ni wakati wa kuchangia bajeti ya wizara ya kilimo na ushirika sasa kama alikua kaboreka si angetoroka ka wabunge wenzake walivyofanya
 
Sasa kama bunge lenyewe wanataka wafanye na mashindano ya ulimbwende yaani watafute madam bunge na jioni hii wameongeza wanataka wafanye na mapambano ya ngumi unategemea wanoandika hayo matangazo na kumtumia speaker ayasome wanakuwa wanawaza nini? Au unafikiri wanamfaham vipi speaker? Enzi za Sitta hakukuwa na upuuzi kama huo ila kwa sasa vuteni tu subira mtasikia mengi
 
Anathibitisha alichosema juzi kuwa baadhi ya wabunge huingia wakiwa tiiiiiiiiii!!
 
ni kwamba Ndugai anakuwa bize na mambo mengine kama wanao ongea ni wabunge wa CCM kwa sababu anajua wanaunga mkono kila kitu,ila kama wanao ongea ni wabunge wa CHADEMA huwa anakuwa msikivu na makini sana
 
labda anaulizwa maswali na watoto wake kwa nini hawajui idadi yao? watakuwa walikuwa wanahitaji majibu fasaha watakuwa wamechukizwa na kauli yake kwamba hajui idadi kamili ya wanawe kwa hiyo labda ndo sababu ya kuwa busy simu yake na vilevile mama za watoto watakuwa walikuwa wanataka majibu pia hahhahahahahahahahahahahahahahah
 
Anapewa miongozo na wadosi kupinga kujadiliwa kwa issue kama mgomo wa wa walimu.....majina ya mafisadi wabunge kutotajwa bungeni ndani ya kipindi cha bajeti,....kusupress oposition n.k

Baada ya Jembe Sitta kutolewa kwenye kiti, maspika wa wakati huu wanapelekwa pelekwa
 
Pengine alikuwa anachabo picha za xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx nani ajuae
 
Huyo kwanza jana kakiri ni mzinifu, hukumu yake ni kifo tu. Hafai kuongoza hata kidogo, wacha bunge, hata serikali ya mtaa.

Juzi nilimsikia Zungu alipokaa kwenye kiti anavyoongea kwa utaratibu na kunyeyekea. Ni mfano wa kuigwa.
 
alikuwa anapitia jf

aone mijadala ya huku

sometimes anafanya maamuzi baaada ya kuchabo jf

au ilikuwa ya tochi
 
Huyu Naibu Spika wiki iliyopita si alisema wabunge katika kikao cha jioni wengi wanakuwa hawako sawa? Sasa yeye mwenyewe anatumia Valour; FEGI au ulevi upi hadi awe Phone Operator wakati kikao kinaemdelea?

Hawa jamaa bungeni sasa wanakuwa kama wako kijiweni (sema kijiwe chenye class kiasi)..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom