Ndugai ALIKOSEA Vifungu Kumvurumusha Ndugulile Bungeni!

chuwaalbert

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
3,598
2,115
MBUNGE wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile, amesema kuwa licha ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vitatu Bungeni kwa ajili ya kuwatetea wananchi wa Kigamboni, ataendelea kupambana kuhakikisha haki inatendeka kwa wakazi wa Kigamboni. Mbunge huyo alisema hapingi kuanzishwa kwa mji mpya wa Kigamboni, bali anapinga taratibu zilizotumiwa na serikali kutekeleza mradi huo.
Amesema suala la uendelezaji wa Mji Mpya unatawaliwa na Sheria ya Mipango Miji Na.8 ya 2007 ambapo sheria hii inaelezea kwa ufasaha taratibu zinazopaswa kuchukuliwa tangu hatua ya kutangaza kwa mradi hadi utengenezaji wa mpango kamili.



Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria , mchakato huu unapaswa kushirikisha wananchi katika kila hatua. Aidha, kifungu 24 (2) kinatamka bayana kuwa Mamlaka ya Kupanga Mji (Planning Authority) inaweza kusimamisha uendelezaji na ujenzi kwenye eneo la mradi kwa kipindi kisichozidi miaka miwili ili kutoa nafasi ya kuandaa mpango kamili.

Katika hatua nyingine Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amedaiwa kukiuka Kanuni za Kudumu za Bunge kifungu (71) (2) (3) na (4) wakati alipomwadhibu Dk. Ndungulile, asihudhurie vikao vitatu mfululizo baada ya kushindwa kuthibitisha tuhuma kwamba madiwani wa Halmashauri ya Manispaa Temeke walihongwa ili kuukubali Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni.



Ndugai alitumia kifungu cha 73 (3) ambacho kinampa mamlaka ya kumwadhibu mbunge aliyeshindwa kuthibitisha tuhuma alizozitoa, huku pia akiwa amekaidi kufuta kauli yake kuhusiana na tuhuma hizo.



Baadhi ya wanasheria na wabunge waliozungumza na gazeti hili walisema Ndugai alitumia jazba katika kufikia uamuzi huo na hivyo kukiuka utaratibu mzima wa kanuni za Bunge unaotumika kushughulikia malalamiko ya mtu asiye mbunge.



Ndugai alipaswa kutumia kifungu cha 71(2) na (3) katika kushughulikia sakata hilo la Dk. Ndugulile na madiwani kwa kuwasilisha malalamiko hayo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kuyatafakari na kulishauri Bunge.



Chanzo:
Tanzania Daima Jumatano
 
Kila siku tunasema NDUNGAI ni Janga la Taifa... ni mtu wa kukurupuka ovyo ovyo tu.
 
Si unajua tena wanasimamia kauli yao ya KIDUMU CHAMA CHA MAGAMBA wakati hawajui kuwa KIDUMU kilishatoboka.
 
Back
Top Bottom