Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
Ndovu waliopoteza miguu baada ya kukanyaga vilipuzi katika mpaka wa Myanmar na Thailand wamewekewa miguu bandia inayowasaidia kusimama na kutembea.
-
Ndovu mmoja aliyepoteza mguu mmoja baada ya kukanyaga kilipuzi katika mpaka wa Myanmar na Thailand amewekewa mguu bandia.
Mosha alikuwa na umri wa miezi saba alipopoteza mguu wake.
Watunzaji wanyama katika hifadhi ya Lampang wanasema alikabiliwa na matatizo ya kiafya kutokana na kukosa mguu.
Rafikiye Mosha, Motola, pia ameundiwa mguu bandia.
Motola alijeruhiwa na kilipuzi alipokuwa akifanyishwa kazi na wakataji miti msituni 1999.
Hajaweza kuutumia vyema mguu wake kutokana na hali ya majeraha aliyoyapata.
Shirika la Asian Elephant Foundation linasema wengi wa ndovu wanaotumiwa na wakataji miti msituni hujeruhiwa na vilipuzi.
Leo Motola na Mosha wanaweza kusimama na kutembea bila matatizo.