maharage ya ukweni
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 1,493
- 3,382
Asalaam aleykum!
Habari za asubuhi!Wanabodi leo naendelea kuelezea mfululizo wa ndoto ambazo zinamuhusu kiongozi wetu ambazo tatu zimeshakamilika bado moja ambayo sijui itakamilika lini.Leo ntaelezea moja ambayo imekamilika na ile moja ambayo haijakamilka,wataalamu wenye elimu ya kutafasili ndoto watanielewesha kama itakua tofauti na ninavyofikiri maana kama ninavyosema kwamba mimi sina elimu ya kutafasiri ndoto lakini ndoto ninazoota hutokea kweli.
Kuna siku niliota natembea kwenye eneo fulani ambalo kwa shughuli za serikali ni kubwa kimadaraka,nikawa natembea huku na kule nashangaa shangaa nikawa naona maeneo fulani ambayo ni ya kupumzikia na kukawa kuna mtu fulani ambaye nilikua simuoni lakini yeye ndiye alikua ananielezea maeneo tofauti ikiwemo sehemu ambayo hua kiongozi mkuu pamoja na wasaidizi wake wanafanya mikutano.
Moja ya sehemu ambayo alinieleza ni sehemu ambayo nyerere alikua anafanya mikutano yake,sehumu aliyokua anatumia kupumzika tena kuna sehemu fulani kuna mandhali kama bwawa la kuogelea.Pia nikaoneshwa sehemu fulani ambayo wabunge waliitumia kufanya shughuli zao ambapo kuna sehemu nikawa ninaambiwa walitumia kufanya kikao cha jambo fulani la kutunga muongozo fulani wa sheria ambazo zilitumika katika kuendesha serikali.
Lakini nikafika sehemu fulani ambapo kuna mlango lakini huo mlango haukushikiliwa na ukuta wa matofali ila niliona mlango umesima pembeni yake kuna uzio wa senyenge zile zenye matobo makubwa makumba ambapo unaona upande wa pili.Kabla ya kuupita ule mlango nikatizama kwa juu nikaona maandishi yanasomeka MAGUFULI,nikawa najiuliza MAGUFULI ndio nini?Basi ikanibidi nigeuze kichwa changu chini juu nisome labda kile kibao kimejigeuza kwabahati mbaya juu chini lakini yale maandishi yakawa hayaleti maana na maana ikabaki ile ile ya jina MAGUFULI na wala sikujua hili jina kwenye kibao juu ya ule mlango linaashiria nini.
Ikabidi nipite niende upande wa pili na maadhali niliyokua naiona katika ile sehemu ilikua ni ya ikulu kwani huaga nikipita kwa nje kuna maeneo yanafanana sana katika ile ndoto.Baadae niliota ndoto fulani fupi wala siikumbuki ambayo ndio ilimalizia usingizi kabla ya kuamka.Hii ndoto niliota kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais,wabunge na madiwani na kabla Rais hajapitishwa na chama kuwa mgombea wa Rais kupitia chama chake
Ifuatayo ni ndoto ambayo haijakamilika na sijui itakamilika lini na mimi wala sipendi ikamilike kwakutoke kama ilivyotokea kwenye ndoto tatu kati ya zile nne nilizoota kumuhusu kiongozi wetu.Kuna siku nililala nikaota Rais wetu anaumwa ugonjwa mbaya sana ambao unahusiana ubongo pamoja na akili tena ugojwa wenyewe ni wa kiswahili.Kutokana na ugojwa huo hatoweza kuongoza hivyo hakuweza kuendelea kua Rais.Niliota hivi nimetokea njia fulani hivi mbele nikamuona Rais nje ya vijumba fulani vya nyasi vimechoka sana ambavyo watu wanaoishi kwenye vijumba hivyo ni mafukara wa kutupa.
Pembe alikua mke wake anamsaidia kumuhudumia kwani hakua hata na uwezo wa kutembea vizuri,nikawa nasikitika sana kwajinsi ambavyo anaumwa kiasi mpaka kutembea inabidi asaidiwe lakini pembeni nikawa nasikia watu wanazungumza maneno ya kumkashifu mojawapo ya neno nililosikia ni mtu anasema "tatizo anajifanya mjuani sana wakati mwenzake aliyepita alikua anafanya hivi na vile lakini yeye anafanya anavyojua yeye".Akaendelea kusema mwenzake alikua anasaidiwa na mzee fulani na kina fulani lakini yeye anafanya utadhani anaweza kila kitu.
Baada ya kupita kwenye vibanda kama viwili hivi vya nyasi ambavyo Rais alikua anauguzwa kwakupatiwa baadhi ya huduma wakiwa nje pamoja na kusaidiwa wakati wa kutembea.Mbele nikaona nyumba ambayo haijaisha kujengwa yaani kuna ishara ilikua inaonyesha kwamba ile nyumba ni nyumba iliyokua inajengwa na Rais lakini ujenzi umesimama kutokana na kuumwa kwake kwani yeye ndio alikua msimamizi mkuu wa nyumba ile pamoja na eneo lote lianalozunguka ile nyumba.Nikawa naishangaa ile nyumba ambapo niliona kuna baadhi ya kuta hazijafika juu usawa wa kuuzeka bati na vile vyumba ambavyo vimefikia usawa wa kuezeka bati havijaezekwa bati.
Moyoni nikawa nasema ndio basi tena hapa watakuja watu wengine watauza mpaka eneo linalozunguka hiki kiwanja,baada ya hapo ndoto hii ikaisha nikaendelea kulala na baada ya mda nikaamka na kuelekea chooni kujisaidia na kurudi tena kulala.
Baada ya kutafakali hii ndoto nikapata maana ya kwamba mbeleni kiongozi wetu atapata tatizo la afya na kushindwa kuliongoza taifa hivyo kutafanyaka uchaguzi mwingine wa Rais ili kumpata Rais mwingine atakayeliongoza taifa.Na hili linaweza kutokea katika kipindi ambacho muda wake wa uongozi bado haujaisha,mwenye tafasili nyingine ya hii ndoto naomba anisaidie.
CC;FREEDOM TOMMORROW