Ndoto Yake Iko Nje Ya Uwezo Wangu.

Ndoto Yake Iko Nje Ya Uwezo Wangu.

Tman900

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
969
Reaction score
3,065
Mi ni mtu wa kipato cha Kati, nimewaza saidia Vijana kadhaa,
Mmoja aliosoma DMI. Na alipo maliza Chuo tulipambana kumtafutia kazi.
Mambo yakawa Heri akapata kazi
Sasa Yuko kijana yeye alimaliza form 4 na Ana Division 3, Toka nimemfahamu kwa siku ya kwanza ktk hizi Familia Zetu za kawaida.
Alionyesha ndoto ya kazi anayoitaji, kipindi kile alikua Bado mdogo nikaamini ni utoto akikua atabadilika lakini Bado ameshikiria msimamo wake kua anataka kua Mwanajeshi.
Changamoto niloonayo, ni kua sina Hata njia ya kumsaidia huyo Mtoto kufikia malengo yake.
Nilijaribu kufanya research zangu Binafsi Ili nimsaidie kufikia malengo yake huyo dogo, Bado niliona hiyo njia haiana mafanikio.
Mwaka Jana alimaliza mkataba wa JkT kwa sasa Yuko home, nikajaribu kufanya kamchezo ka kumuingiza taratibu Ili apende Biashara, yaani Wala haonyeshi kuvutiwa na Biashara zaidi ya kutaka kua Mwanajeshi.
Jana tulitoka kwa matembezi tukiwa ktk matembezi nilimgusia juu ndoto zake kwa sasa anatamani kufanya kazi Gani, Bado alisema anataka kufanya kazi ya Jeshi ndio kazi anayoipenda, sikutaka kumkatisha tamaa. Nilitumia neno tu la hekima kua nitapanga siku Tuongea Vizuri kuhusu Maisha na mzunguko wa kazi.
Sasa nawaza namna ya kumbadilisha mtazamo wake na kazi anayoitaka, na ni njia Gani ya ushauri ni mbadilishe mtazamo wake kwa hiyo kazi anayoitaka kua ipo nje ya uwezo wangu kumsaidia.
 
Ndoto zinaishi kama alishapata mafunzo ya awali basi wampambanie afikie huko ,kama akipata mwenza wake ampambanie maisha nj haya haya tu.
 
Hakikisha kwanza ana elimu angalau ya advance. Akienda kuwa MP tu atajutia ndoto zake
 
Back
Top Bottom