Ndoto ya tenga imekuwa kweli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoto ya tenga imekuwa kweli!

Discussion in 'Sports' started by Shedafa, Jan 6, 2010.

 1. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ndoto ya Tenga kuitangaza TZ kwa njia ya mpira hatimaye imelipa, leo kwa mara ya kwanza BBC WORLD kipindi cha michezo kimetangaza habari za Tz kucheza na Ivory coast. Ingawa focus yao ilikuwa kwa Drogba lakini ndio wametutangaza hivyo, na kuweka high lights chache za mpira huo likiwepo goli tulilofungwa. Kwangu mimi imelipa, watu wamesikia habari zetu na kuona uwanja wetu.
   
 2. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii ni kazi ya Tenga au Maximo?
   
 3. E

  Edo JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Yap, ni kweli hata kwenye www.soccernet.com habari ilikuwepo front page. Ni mwanzo mwema !
   
 4. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu Shedafa,
  Kutangazwa huko, watu wamesikia habari zetu NZURI au udhaifu?
   
 5. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #5
  Jan 6, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Nadhani udhaifu maana tulifungwa. Sidhani kama walikua
  wanaongelea kuhusu Kilimanjaro au Serengeti.
   
 6. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  bongo suala la uwanja bado ni tatizo....
   
 7. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Uwanja una nini???
   
 8. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Dunia imetuona, kufungwa kwenye mechi za mpira wa miguu ni jambo la kawida na wakati mwingine ni ngekewa ya timu iliyoshinda. tukiangalia mchezo wa J3 wageni hawakucheza sana zaidi ya wenyeji ila bahati ilikuwa yao. Viva Maxmo, tenga ni mratibu tu
   
 9. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  http://www.chelseafc.com/page/LatestNews/0,,10268~1923534,00.html
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hamna mtu mwenye kazi yake hapa,TUSIDANGANYANE!...kikubwa na muhimu ni kwamba muda umefika wa sisi kufikia kwenye hiyo levo ndogo ya uchezaji
   
 11. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nimesema Tenga kwa sababu ndiye aliyewafuata Ivory Coast wakati wanacheza na Malawi kama niko sawa, aliwafuata kuwaomba waje wafanye mazoezi hapa kabla ya kwenda Angola. Kwa hiyo ujio wao si juhudi za Maximo, ingawa Maximo naye anastahili kupongezwa kwa sababu wasingekubali kuja kama kusingekuwa na sifa nzuri hata kama kiwanja ni kuzuri namna gani.
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,287
  Likes Received: 22,047
  Trophy Points: 280
  Taratibu taratibu na sisi tutakuja kuwa gumzo.
  Cha muhimu ni koboresha tu sera zetu ili soka letu likue
   
 13. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Tunastahili kuwapongeza kina tenga...msijifanye mmesahau enzi za kina al hajji....

  walikua kila siku ni migogoro na ndo mana walishindwa kuconcetrate na maendeleo

  ya soka. sasa hivi kucheza na timu zenye majina makubwa ni kawaida bongo.

  big up TENGA
   
 14. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  jamani tenga ametutangaza kwa lipi? nchi inatia aibu sana zambia,gabon,benin,togo, hizi ni nchi changa sana kwetu kiuchumi,leo zimeingia africa cup 2010 angola sasa leo utaweza kusema nini jua ya tenga na jopo lake la TFF.....mimi nataka wote wanausika na michezo hapa tz waondolewe madarakani na waingia watu wenye uwezo na sera za kutupeleka kwenye mashindano makubwa.kuhusu kocha wa taifa ni bora tuwe na kocha mzalendo ambaye anajua nchi yetu,atajua wapi anaweza kupata wachezaji.
   
 15. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Makubwa, ikiwa mtazamo wa uchumi tena ni kigezo itakuwa kazi!. Kwa hiyo Marekani si ndio angekuwa bingwa wa dunia kila siku, vipi uchumi wa Brazil kulinganisha na USA, UROPA na JAPAN?. Kwani mkuu, kabla ya Maximo alikuw kocha mzungu?. Je, kuna mtu alikuwa hata na hamu ya kuzungumzia Stars?.
   
 16. A

  Alpha JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Now we need to build 3 more quality stadiums, improve our public transportation, expand our airport, get more investment in Hotels, Get rid of the traffic jams, etc and we can host the African Cup of Nations ourselves. LOL! ;)

  I know.... i'm dreaming
   
 17. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Inshallah, nawe ndoto zako ziwe kweli kama Tenga!
   
Loading...