Ndoto ya Rais Samia kuifufua NARCO yaanza kutimia

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,032
Serikali imeiwezesha Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) Sh. bilioni 4.65 kununua vitendea kazi na ng'ombe wazazi ili kuboresha na kuongeza uzalishaji wa kampuni hiyo.

Hayo yamefahamika wakati wa ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega aliyoifanya katika Ranchi ya Kongwa wilayani Kongwa jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
"Wakati akizindua matreka mapya matano na kupokea ngo'mbe 1,000 kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa kampuni ya NARCO, Ulega alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha kampuni hiyo iweze kujiendesha kibiashara.

Alisema lengo la Rais Samia ni kuiimarisha NARCO kwa kuboresha miundombinu na vitendea kazi ili waweze kunenepesha ng'ombe, kuimarisha biashara ya nyama bora

ya Kongwana kuzalisha malisho ya mifugo kwa wingi na kuyauza ndani na nje ya nchi.

"Hivi sasa tumeshafika katika kiwango cha kuuza nie ya nchi nyama tani 12,000 na kUanzia mwaka Ulao na kuendelea tutatoka kwenye tani hizo na kutafuta tani 50,000 na ikiwezekana mpaka tani 100,000," alisema.

Pia, alisema katika mkakati wa kuifufua kampuni ya NARCO wataanzisha skimu za un-enepeshaji wa mifugo ili nyama itakayokuwa inazalishwa kutoka NARCO iwe na ubora wa kuiuza nje ya nchi.
"Tunakusudia kwamba mchango wa sekta ya mifugo vongezeke kutoka asilimia saba hadi kufikia asilimia zaidi ya 10, na hilo linawezekana kwa sababu rasilimali ya kutu-wezesha kufikia huko tunayo," alisisitiza.

Alisema, serikali ina mipango ya kuanzisha skimu za umwagiliaji wa malisho ili yaweze kuzalisha kwa wingi kwa ajill ya kuyauza ndani na nje ya nchi.

"Kama tunavyosafirisha mahindi kutoka maeneo mbalimbali na kuwapelekea wahitaji tunataka pia tuzalishe malisho kwa wingi na kuyasafirisha kuyapeleka kwa wahitaii waliopo ndani na nje ya nchi" alifafanua
 
Back
Top Bottom