Ndondi: NKANE v/s KIBWANA - Mapungufu mengine kitengo cha Saikolojia Yanga

kinje ketile

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Posts
5,363
Reaction score
10,101
Kitengo cha 'Sheria' pale Yanga huko nyuma kilijidhihirisha kuwa na mapungufu makubwa ya weledi.

Bwana Patrick Simon ndiye aliyekuwa mkuu Wa Kitengo alifeli sana Kwenye kesi nyingi za Yanga mpaka siku za karibuni akaamua ang'atuke.Ipo Mifano kama Kesi za Kina Morrison kule CAS na rufaa ya Yanga CAS dhidi ya bodi ya Ligi zote Yanga ilikula mwereka na kuangukia pua, mpaka Mama Samia alipoingilia kati kuiokoa Yanga.

Sasa kitendo Cha Kuwaruhusu hawa Madogo Wa Soka Nkane na Kibwana kuzichapa 'live' kinaonyesha lipo eneo lingine pale Yanga halipo Vizuri... Eneo la Saikolojia.

Vijana hawa wa 'Soka' ambao ndio damu changa pale Yanga maana Wengine wengi ni Wazee inaonyesha hawakupata kabisa Ushauri wowote Wa Kisaikolojia walipokuwa Wanaliendea hilo pambano.

Watu wanajiuliza pale Yanga kipo Kitengo hicho cha Saikolojia? Kama Kipo kina wataalamu wa Saikolojia? Hakuna ushauri Wowote walioutoa kwenda kwa vijana hawa?

Kwa kweli sio kwa kile tulichokishuhudia ulingoni.!
 
kama kuna namna iliwafanya wapate pesa, sioni tatizo maana kama ni kuumia unaweza, kuumia hata ukiwa unatembea peke yako tu.

pia, sifikirii kama tatizo ni saikolojia, ila wao wametumia fursa vyema kwa jinsi ambavyo timu yao iko on fire.

Ni kutaka kutafuta trend, ambako bland, ndio hubeba yote hayo. ingekuwa kila supastaa anayefanya shughuli nyingi ana tatizo au management yake ina tatizo, wacheza kikapu wale kina michael Jordan wasingeitangaza Nike huko marekani na kuvuta mkwanja mnono.
 
Kitengo cha 'Sheria' pale Yanga huko nyuma kilijidhihirisha kuwa na mapungufu makubwa ya weledi.

Bwana Patrick Simon ndiye aliyekuwa mkuu Wa Kitengo alifeli sana Kwenye kesi nyingi za Yanga mpaka siku za karibuni akaamua ang'atuke.Ipo Mifano kama Kesi za Kina Morrison kule CAS na rufaa ya Yanga CAS dhidi ya bodi ya Ligi zote Yanga ilikula mwereka na kuangukia pua, mpaka Mama Samia alipoingilia kati kuiokoa Yanga.

Sasa kitendo Cha Kuwaruhusu hawa Madogo Wa Soka Nkane na Kibwana kuzichapa 'live' kinaonyesha lipo eneo lingine pale Yanga halipo Vizuri... Eneo la Saikolojia.

Vijana hawa wa 'Soka' ambao ndio damu changa pale Yanga maana Wengine wengi ni Wazee inaonyesha hawakupata kabisa Ushauri wowote Wa Kisaikolojia walipokuwa Wanaliendea hilo pambano.

Watu wanajiuliza pale Yanga kipo Kitengo hicho cha Saikolojia? Kama Kipo kina wataalamu wa Saikolojia? Hakuna ushauri Wowote walioutoa kwenda kwa vijana hawa?

Kwa kweli sio kwa kile tulichokishuhudia ulingoni.!
YANGA BINGWA!
 
Nilivyoona ile mikwala na vijembe mawazo yakanituma kuwa Walikuwa na Lengo la kuhamasisha...heee kumbe wanavurumishiana mikonde kweli.

Siku ingine wafanyiwe Ushauri nasaha.
 
Walicho kifanya kina utafouti gani na wachezaji wanapo enda kucheza mechi za hisani kipindi cha pre season? au ndio una dhihilisha u mbumbumbu wako?
NB; huwezi kufanya hayo kama timu yako haina makombe
Wanafanya wachezaji wa timu ndogo ndogo kwny Rank za CAF hazisomeki..zinazoishia makundi...muda wanao wa kutosha
 
Nilivyoona ile mikwala na vijembe mawazo yakanituma kuwa Walikuwa na Lengo la kuhamasisha...heee kumbe wanavurumishiana mikonde kweli.

Siku ingine wafanyiwe Ushauri nasaha.
Mi mwenyewe nilibakia nimeduwaa mana nilijua lengo lao ni kuhamasisha pia. Hee nikaona makonde mwanzo mwisho.

Na bahati walivyorusha ile taulo mana ambacho kingefuata pale ilikuwa ni ngumi za ukweli ukweli.
 
Back
Top Bottom