Ndoa zawagawa wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa zawagawa wabunge

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BAK, Nov 4, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,811
  Likes Received: 83,208
  Trophy Points: 280
  Ndoa zawagawa wabunge
  Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 4th November 2009 @ 09:14
  Habari Leo


  MBUNGE wa Kibakwe, George Simbachawene, amesema, kumzuia mtoto mwenye umri wa miaka 14 au 15 kuolewa kama yupo tayari kuhimili mikiki mikiki ya ndoa ni kumnyima haki yake ya msingi.

  Simbachawene amesema, si busara kumzuia mtoto kuolewa baada ya kuhitimu elimu ya msingi kwa kuwa si wote wenye malengo ya kuendelea na elimu.

  Mbunge huyo amesema, wapo watoto wenye umri wa miaka 16, ni mabinti wazuri wenye sifa za kuolewa. Kwa mujibu wa Mbunge huyo, jambo la msingi si kumzuia mtoto asiolewe, bali uthibitisho wa daktari kuwa anaweza kuingia kwenye taasisi hiyo.

  Simbachawene amesema, watoto wa kike wanakua haraka, hivyo wakiwa tayari kuolewa, wazazi washirikishwe ili wapate haki ya ndoa.

  Ameyasema hayo bungeni wakati anachangia muswada wa Sheria ya Mtoto wa mwaka 2009 unaohitimishwa leo.

  Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Lyimo, amesema, suala la umri wa kuolewa si la msingi kwa kuwa kuingia katika taasisi hiyo au kutoingia ni uamuzi wa mtu kwa kuzingatia mazingira husika.

  Mbunge wa Viti Maalum, Martha Mlata, amehoji, mtoto anayeolewa akiwa na umri wa miaka 14 au 15 anafuata nini huko?

  Kwa mujibu wa Mbunge huyo, kumruhusu mtoto mwenye umri huo aolewe ni sawa na kuruhusu watoto waoane.

  "Hivi unategemea nini akiwa leba… Ni ugonjwa huo kwamba anaenda kutibiwa?" amehoji Mbunge huyo wakati anachangia Muswada wa Sheria ya Mtoto wa mwaka 2009.

  "Mimi nakataa kabisa, na napinga sana" amesema Mbunge huyo na kupendekeza kuwa mtoto aolewe akifikisha umri wa miaka 18.

  Mbunge wa Viti Maalum, Diana Chilolo, amepinga kuruhusu watoto kuolewa na hasa wanapoolewa na wazee.


   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hivi bongo tuna statutory rape? Kama tunayo what is the legal age of reason?
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Having carnal knowledge of a woman below 18 yrs ni statutory rape..labda kama ni mkeo thats th eposition of the law as of now..- ( refer Sexual Offences Special Provisions Act 1998)

  15ysr ni minimum age for a woman to be married..and even below that with consent of parents/court - ( tizama Law of Marriage Act 1971)-

  too many contradictions .The marriageable age contradicts with the Education Act on compulsory primary eduction,with law of contract on entering into a contract....etc .... long debate...

  Age of majority is 18 as per Age of Majority Act.
   
 4. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Huyu Simbachawene hana lolote anataka mtoto wa kike kuolewa na miaka 15 wala si haki. Au kwa kuwa kaona jimboni mwake watoto wengi wameacha shule na kupata mimba ndio maana anatetea?
  Baada ya kuhimiza wazazi wasomeshe watoto zao wakike, yeye anataka wazazi wakubali. Kweli huyu mbunge yupo zaidi kwa maslahi yake binafsi.
   
Loading...