Wadau, kutokana na kushamiri kwa makanisa mengi hapa nchini na hata mengine kuongozwa na wachungaji (wanavyojipachika vyeo) ambao hawajaoa ili hali wao ndiyo wakubwa wa makanisa hayo.
Jeh! Ni nani atamfungisha ndoa endapo atataka kuoa?
Au anajifungisha mwenyewe ndoa? Kumbuka ndy kwanza kaanzisha kanisa...
Mbonea bwana huyu akitaka kuoa lazima afungishwe na mchungaji mwingine ..ingawa anaweza kuwa ni wa kanisa hilo hilo sehemu nyingine ..Ila hawa nao wana hatari
Ukiuliza wanasema wanaupako na karama yao ni kutangaza neno la mungu...
kweli hizi ni siku za mwisho na ni nyakati za hatari
Njaa jamani ndio inayo leta haya yote,maana nakumbuka enzi hizo mchungaji habarikiwi kuwa mchungaji mpaka awe amefunga ndoa,siku hizi ni vurugu tupu,mtu akiweza kutafsiri mistari miwili ya bibilia anajiita mchungaji,hawa jamaa ndoa zao huwa wanawaalika wachungaji wenzie kumfungisha ndoa
Kuvunga ndoa sio tatizo. Ninadhani hayo makanisa ya wanaojiita wachungaji wapo wengi, anaweza akampa madaraka mwenzake amfungishe ndoa.