Heshima kwenu wana JF nyote.
Ukweli nahitaji sana msaada wa mawazo yenu. Mimi nimeoa na nina watoto 2. Tatizo kubwa ni huyu mama-watoto wangu. Ukweli ananifanya niujutie uamuzi wangu wa kumwoa. Na hakika kama ningejua ndoa yangu ingekuwa hivi, kamwe nisingemuoa na pengine nisingeoa kabisa. Kwa miaka 8 yote nimeishi kwa kuvumilia tu lakini kero mtindo mmoja. Mwanamke mbishi,mwenye dharau, mgomvi, mwenye kupenda kushindana, hana shukurani na neno "samahani" ni mwiko kwake. Akikosa badala ya kuomba radhi utamsikia "kwani wewe hukoseagi?" Ni mchokozi, mjuaji na asiye na dogo na asiye na unyeyekevu kabisa. Hapendi tuongozane njiani na wakati mwingine anaanzisha ugomvi au ubishi barabarani. Anakosoa karibu kila ninachokifanya. Mfano nikileta mboga nyumbani utasikia "sasa ndio nyama gani umeleta?" tunapokwaruzana kwa maneno, anataka ninyamaze yeye aseme na awe wa mwisho kusema. Mimi ni mwalimu na yeye ana elimu ya drs la 7 ila ninapowafundisha wanangu nyumbani yeye hujifanya anajua zaidi yangu na kusema nawapotosha watoto akitaka niwafundishe anavyotaka yeye. Mara kadhaa nimewahi kumwambia kuwa asipojirekebisha nitamrudisha kwao lakini hunijibu kwa dharau ati "kwani ulinitoa kwenye mti?" Haya ni kwa uchache tu. Ana kero nyingi, nyingi, nyingi sana. Nimeshawahi kumwita dada yake akatukalisha na akamsema sana mdogo wake lakini alitulia wk 2 tu, kero zikarudi palepale. Japo nimefunga naye ndoa kanisani, hiyo sio kinga dhidi ya kummwaga. Nahofia tu malezi ya wanangu 2: mkubwa yuko drs la I na mdogo chekechea. Ukweli naumia sana na mwanamke harekebishiki. Nifanyeje jamani?