Ndoa za siku hizi

washajiwekea wanawake wa kiafrika ni watumwa, sasa imekula kwao kizazi kingine hiki
 
Wee homeboy inabidi ubadilike. Achana na huo mchezo mchafu ni dhambi kwa MUNGU tena mbaya sana. Kisha mshauri na rafiki yako Fidel naye aache.

....lol, eti mchezo mchafu... waambie wewe labda watakusikiza,...ukiwatishia na dhambi hawataacha, waambie kuna UTI, ipo siku njia ya mkojo itaziba!

mbu unanifanya nitoke kwenye mada.......lakini mkiwa na watoto lazima 'muibie' fulani hivi kugusana. ......watoto wasijekuwafuma wakapofuka bure!

ndoa lazima kuwe na sacrifices kila upande. kubali kulalia upande wke pia wakati wengine ili na yeye asione tabu kulalia uande wako muda mwingi.

...na kweli, kuibia kutamu hata kama mshajihalalishia, chap chap kabla watoto hawajarudi shule, nk...:)
 
kinachonishangaza zaidi ni wanaume hawa hawa waliopo bongo sasa, wakati walipokuwa viwanja vya watu huko, walikuwa wakifanya mambo telee kusaidia wake/gf zao. leo wameikanyaga tz ndo wamekuwa hawawezi tena!

...hakuna mgao kule,...halafu si unajua tena hoover linaunguruma ukibonyeza kitufe tu, dishwasher nayo aaaah, washing mashine na dryer kama kawaida...

Sasa ukija Bongo utafute taulo la kupigia deki, maji yenyewe mgogoro,.. halafu mtu wewe wewe utoke na beseni lako la nguo ukaanike nguo uani kwenye kamba majirani wanakuchora ukianika sketi na chupi za mkeo? no way bana...

Kama wife anataka usaidizi hausigeli wapo, lakini watendewe utu!

washajiwekea wanawake wa kiafrika ni watumwa, sasa imekula kwao kizazi kingine hiki

...sio utumwa jamani, wajibu wenu tu.
 
kinachonishangaza zaidi ni wanaume hawa hawa waliopo bongo sasa, wakati walipokuwa viwanja vya watu huko, walikuwa wakifanya mambo telee kusaidia wake/gf zao. leo wameikanyaga tz ndo wamekuwa hawawezi tena!

Gaijin, kuna watu wanaobadilika kutokana na mazingira yanayowazunguka na wengine hawabadiliki kabisa. Kuna jamaa mmoja wa Ki-Zanzibari aliingia kwenye mahusiano na dada mmoja wa Ki-Norway wakati jamaa anasoma huko. Jamaa ilibidi avunje uhusiano mara moja baada ya kuwa anaamshwa asubuhi akamwandalie yule binti breakfast. Si unawajua Wazanzibari walivyo ma-mwinyi?
 
...upo sahihi hasa!

Tatizo ni kina mama wa kileo kujibweteka! ...wengine usipowatolea uvivu utakuta hata chupi za mkeo na boxers zako zinafuliwa na house girl!...

Muhimu baba mwenye nyumba kuhakikisha hako kabinti nako kanapata mahitaji yake muhimu ya kibinaadamu, ....!

Hapo sasa kwenye ubina-adam!
 
utanisahihisha kama nimekosea....
  • wanaotunza nyumba( usafi,mazingira, chumbani kwa mabosi) ni mahouse girl
  • wanaotunza watoto ni mahouse girl
  • wanaofuatilia maendeleo ya watoto ndio hao hao
  • wanaomtayarishia baba mahitaji(maji ya kuoga, chai..nk.) bila kulalama uchovu ni mahousegirl
  • bila housegirl chakula hakipo, kikiwepo basi kitachelewa na ladha hairidhishi
  • mpangilio wa chakula mama lazima apate ushauri wake....utasikia ...dada leo tunapika/tunakula nini?
Pamoja na mengineyo mengi
  • akirudi mama huyu bado atampelekesha house girl bila kujali
  • house girl huyu huyu hana uhuru wa kukaa meza moja kula chakula alichokiandaa mwenyewe akiwa na matajiri wake
  • kosa dogo mtaa wa pili watalisikia kwa kelele zitakazotolewa na bibie tajiri
  • akivaa vizuri pia nalo ni kosa endapo atasalimika kutuhumiwa mwizi
  • hana haki ya kupumzika wala kula gudi taimu n.k
  • ole wake acheke au atabasamu akiongea na baba then mama amuone kwa bahati mbaya...atakoma!
Baba mie, sijui wengine__ I find it rahisi kumuomba/kumtuma hg maji ya kunywa, kubrash viatu, maji ya kuoga, n.k kwani atavifanya bila kulalama au kukunja uso__usinielewe vibaya ( sijafika unakofikiria)...TATIZO ni nini hasa? aaaaagghhhh!!!
MMH, with all the due respect sir, hujamla kweli huyu? je hata kufikiria kumla ushafikiria? kama bado acha ndugu yangu just try kurekebisha mapungufu ya mkeo kwa utaratibu. btw vingine kama hivyo kwenye zambarau unaweza kufanya mwenyewe bila kuhitaji msaada wa dada.
Halafu hiyo bluee ndo naidiscourage kabisaaa, yani kama anafanya hivi ataniudhi sasa, kwani kufanya hivo watoto wanajifunza nini? mbaya sasa hiyo.
 
...hakuna mgao kule,...halafu si unajua tena hoover linaunguruma ukibonyeza kitufe tu, dishwasher nayo aaaah, washing mashine na dryer kama kawaida...

Sasa ukija Bongo utafute taulo la kupigia deki, maji yenyewe mgogoro,.. halafu mtu wewe wewe utoke na beseni lako la nguo ukaanike nguo uani kwenye kamba majirani wanakuchora ukianika sketi na chupi za mkeo? no way bana...

Kama wife anataka usaidizi hausigeli wapo, lakini watendewe utu!

...sio utumwa jamani, wajibu wenu tu.
yeah wajibu wetu indeed! na nyie wajibu wenu si kutafuta nyumba nzuri zenye hoovers na kuhakikisha ndani kuna dishwasher na washing mashine? au hapo unasemaje?
swala la utu kwa dada tuko pamoja kabisaa haina ubishi. kwa mtu yeyote mwenye akili dada anayeshinda na mwanao siku nzima we uko job lazima umtreat right otherwize usijelia siku moja.
 
sasa unalalama nini, kama vp fanya mwenyewe, unajua maji yalipo yawe ya kuoga, ya kunywa na nguo kunyoosha unaweza vilevile so fanya. unataka kufanyiwa na mkeo vyote hivyo bila kujali yeye pia katoka kazini kachoka kama wewe na kumsaidia hutaki. enzi za kutumikisha wanawake zishaisha, kama kazini tunaenda wote, na bado nina mzigo wa kubeba mimba na kuzaa na kutunza watoto na ninachangia family expenditures, why then should i still be your maid? Mi nafikiri ifikie mahali wanaume na nyie mbadilike, muone kusaidia kazi za nyumbani si kujidhalilisha, bali ni upendo kwa mkeo na msaada pia.kama ni mama wa nyumbani anaekaa home kusubiri utoke job ulete mahitaji ntakuelewa lakini kama ukiamka na yeye anaamka mnaenda wote job na kurudi, sioni kwa nini uwalaumu wanawake, play your part, they are people just like you.

Amin,Amin nakuambia kama unaona huo ni mzigo, napata hisia kuwa unajilaani kuumbwa mwanamke.Je,, ungependa kuwa mwanaume?
 
Amin,Amin nakuambia kama unaona huo ni mzigo, napata hisia kuwa unajilaani kuumbwa mwanamke.Je,, ungependa kuwa mwanaume?
sijasema ni mzigo na wala sijawahi kutaka kuwa mwanaume ila tu lazima mkubali kuwaheshimu na kuwathamini wanawake, they go through alot, some things you have no idea of, at least you should understand that and help them when necesary. period. ....and i am proud to be a woman, keep it in the records!:cool:
 
Kumbe ndo maana wewe Anopheles quadrimaculatus unashinda kwenye Jukwaa la mambo ya Kikubwa, Michezo na Mahusiano....Njoo kwenye siasa tunajadili Dowans kule!

...Noooooo wayyyyyyyyy!

nilishaachana na siasa za bongo bana, presha tupu... halafu Mheshimiwa Zitto kila nikimsoma data zake najipa depression za bure tu,...

yanini kujitoa raha bure?

Nyumbani kwangu najitegemea,...maji ya kisima na pump kwa mashine, nyumba natumia solar kwenye emergency kama hizi,...Presha ya nini bana?
 
good evening kwa wale wabongo wenzangu. i am out, wacha na mie nikacheki familia inaendaje lol!
 
enzi za kutumikisha wanawake zishaisha, kama kazini tunaenda wote, na bado nina mzigo wa kubeba mimba na kuzaa na kutunza watoto na ninachangia family expenditures, why then should i still be your maid?

sijasema ni mzigo na wala sijawahi kutaka kuwa mwanaume ila tu lazima mkubali kuwaheshimu na kuwathamini wanawake, they go through alot, some things you have no idea of, at least you should understand that and help them when necesary. period. ....and i am proud to be a woman, keep it in the records!:cool:

Ni hapo tu Carmel, labda sikuelewa.....

Apo mwisho, nimenote na kufile, i guess I will need it at some point,,:rolleyes:
 
utanisahihisha kama nimekosea....
  • wanaotunza nyumba( usafi,mazingira, chumbani kwa mabosi) ni mahouse girl
  • wanaotunza watoto ni mahouse girl
  • wanaofuatilia maendeleo ya watoto ndio hao hao
  • wanaomtayarishia baba mahitaji(maji ya kuoga, chai..nk.) bila kulalama uchovu ni mahousegirl
  • bila housegirl chakula hakipo, kikiwepo basi kitachelewa na ladha hairidhishi
  • mpangilio wa chakula mama lazima apate ushauri wake....utasikia ...dada leo tunapika/tunakula nini?
Pamoja na mengineyo mengi
  • akirudi mama huyu bado atampelekesha house girl bila kujali
  • house girl huyu huyu hana uhuru wa kukaa meza moja kula chakula alichokiandaa mwenyewe akiwa na matajiri wake
  • kosa dogo mtaa wa pili watalisikia kwa kelele zitakazotolewa na bibie tajiri
  • akivaa vizuri pia nalo ni kosa endapo atasalimika kutuhumiwa mwizi
  • hana haki ya kupumzika wala kula gudi taimu n.k
  • ole wake acheke au atabasamu akiongea na baba then mama amuone kwa bahati mbaya...atakoma!
Baba mie, sijui wengine__ I find it rahisi kumuomba/kumtuma hg maji ya kunywa, kubrash viatu, maji ya kuoga, n.k kwani atavifanya bila kulalama au kukunja uso__usinielewe vibaya ( sijafika unakofikiria)...TATIZO ni nini hasa? aaaaagghhhh!!!

Then mmeo akitayarishiwa mahitaji ya n.k mke analalama, ka kila kitu housemaid anaandaa then akiamua kumalizia one day usigombe.
Kwa nyumba yangu hakutakuwa na housemaid kabsaa!!
 
Namdawa karibu sana jamvini yaani hapa watu tunajenga na kubomoa hoja karibu sana hujachelewa na hujapitwa na kitu mama mimi ndo Baba Mtakatifu mwenyewe kwa hapa jamvini kuna mashemasi said:
nashukuru sana Fidel naamini sijachelewa kwani nimewakuta wote mnaelimishana vema na kutia moyo.Naamini nami nitajifunza mengi asante sana wanajamii katika darasa hili nyeti na lenye changamoto nyingi.
 
Ndio maana ma HG huwa wanapandishwa vyeo, kisha wenyewe (Hakina mama) wanakuja juu,

somo zuri sana hili,
 
utanisahihisha kama nimekosea....
  • wanaotunza nyumba( usafi,mazingira, chumbani kwa mabosi) ni mahouse girl
  • wanaotunza watoto ni mahouse girl
  • wanaofuatilia maendeleo ya watoto ndio hao hao
  • wanaomtayarishia baba mahitaji(maji ya kuoga, chai..nk.) bila kulalama uchovu ni mahousegirl
  • bila housegirl chakula hakipo, kikiwepo basi kitachelewa na ladha hairidhishi
  • mpangilio wa chakula mama lazima apate ushauri wake....utasikia ...dada leo tunapika/tunakula nini?
Pamoja na mengineyo mengi
  • akirudi mama huyu bado atampelekesha house girl bila kujali
  • house girl huyu huyu hana uhuru wa kukaa meza moja kula chakula alichokiandaa mwenyewe akiwa na matajiri wake
  • kosa dogo mtaa wa pili watalisikia kwa kelele zitakazotolewa na bibie tajiri
  • akivaa vizuri pia nalo ni kosa endapo atasalimika kutuhumiwa mwizi
  • hana haki ya kupumzika wala kula gudi taimu n.k
  • ole wake acheke au atabasamu akiongea na baba then mama amuone kwa bahati mbaya...atakoma!
Baba mie, sijui wengine__ I find it rahisi kumuomba/kumtuma hg maji ya kunywa, kubrash viatu, maji ya kuoga, n.k kwani atavifanya bila kulalama au kukunja uso__usinielewe vibaya ( sijafika unakofikiria)...TATIZO ni nini hasa? aaaaagghhhh!!!

Lakini Kilambi hujasema katika hayo yote mwanaume (baba) anapaswa kufanya nini kwa ajili ya mkewe. Na katika 'ndoa za siku hizi' kama unavyodai, wanaume wanatimiza hayo majukumu 'ya baba', au ni kinamama tu ndio waliokiuka majukumu yao na kuwaachia mahausigeli?

Mie sijaoa naishi peke yangu, natunza usafi wa nyumba/chumba, najua ustaarabu wa mlo wangu nk. Sasa haya yatanishinda vipi nikioa? Nafikiri ni suala la makubaliano tu ya wanaohusika kwenye hiyo ndoa.
 
na hata wakati mwingine tunapata shida kusema aksante kwa housegirl, ye ndo kaandaa chakula, na anakusubiri umalize kula ili atoe vyombo, nguo kafua, kakunyooshea, maji kakuwekea bafuni/kaandaa bafu, ni nani wa kumshukuru kama si yeye? na ukisema shsante kisha mke akasikia ujue vita kati ya mke na dada, sasa najiuiza ni nani anaistahili hiyo shukrani au kusifu maandalizi? ndoa za leo tutegemee kudra za mungu kuzidumisha,
 
I am better than my wife. Huwa analia sana wakati wa kumegana, afu anamalizia kwa kushukuru: Thanks Chris, you are everything to me!. You are so sweet. Hahahaha!

kwani wewe huwa hugugumi? vilio vyenu vinatofautiana sauti tu. all the same
 
Back
Top Bottom