Ndoa za sasa zina misukosuko mingi kuliko za zamani

Unique Flower

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
12,714
24,891
Habari za wakati huu, sasa ndoa za kileo ni za hatari sana,

Tukiachana na zamani:
1. Ndoa za leo ni misukosuko. Wanaume wanaoa kitu kwa mtu badala ya yeye mwenyewe.

2. Mtu anaolewa na mtu kwa sababu fulani sio huyo mtu.

Sasa tuanze, wanaume wengi wanaoa mke kisa umbo, wadhifa, anajua kuhudumia, mweh sasa unakuta wameenda kanisani kuoana kumbe mtu hata hamjui lolote kuhusu mwenzake kiundani hujawahi ishi naye ujue madhaifu na mapenzi yake, akinuna hujui yupoje na jinsi yakumrudisha kwenye hali yake ya kawaida hujui. Mnaishia kupishana maelezo.

BAADA YA NDOA
Unakaa naye miezi mitatu mtu anaanza kujionyesha madhaifu yake. Unapewa pewa madimlight hadi unashangaa, maisha ndio haya ungemjua tokea zamani ungefanya maamuzi ila ulimpendea kalio, kazi yake, utafutaji wa maisha, akili yake au sauti yake unajikuta basi. Huwezani naye.

Ndoa nikupangilia kuweka final say i got her. Basi sasa baba yako or your mom angekuwa wewe unaruka ruka this way hutulii kwenye ndoa ungeenda mtambulisha mwenzako kwanani. Tulia ulishamkubalia tulia the same to you guys baba ako angekuwa anaogopa kupambania ndoto yake ungekuwa unaenda kumtambulisha wapi mwenzako.

Halafu ndoa isiyoendeshwa na maombi na sala na kumkabidhi Mungu akupe nguvu ya kuishi nao kwa akili hutoboi mwaka. Kwa mwanamke unatakiwa kumkabidhi Mungu akupe nguvu ya kuishi naye huyo mwanaume.

Maisha ya ndoa ukiyachukulia resi resi utazima haraka tulia penda kumuelewa unayeishi naye mpange jinsi ya kuishi mpate familia iliyobora. Acheni kutamani njee hiyo ni sumu.

USHIRIKIANO
Maisha ya ndoa magumu, sio marahisi inahitaji muelewa na mvumilivu, ili ukabiliane na maisha yenu. Jua jinsi ya kumfanya akusamehe, akupe ule ushirikiano mzuri umoe hata vizawadi zawadi ili upendwe tafuteni njia yakushirikiana kwa pamoja ili muishi kwa amani.

Ila watu wa sasa hawana huo muda wao ni free hawataki kujituma, kujitolea, kuwa wavumilivu, kujaliana na kuona mimi na majukumu na mtu nilimpromise i will be with him or her forever alidhani alikuwa anacheza rumba. Au alikuwa anaigiza filamu za kibongo kuwa ikisha filamu na rudi kuwa single na igiza tena na mwingine. Hakunaga huo ni uwongo.

Umeoa na ndio umeanza kuitwa baba unaanza majukumu no kwendra popote chali yangu. Sasa unategemewa sio kujitegemea unaanza kuweka hela mezani, unaanza jioni kutoa haki yako na nilazima. Sio ombi ukigoma unashatakiwa bomani.

Ndoa ni commitment na unajitolea. Your time, Your everything to her or him sio unajibu jibu rubbish ukiulizwa uko wapi utakuja home saa ngapi. Kama hutaki kutawaliwa kataa ndoa.

Acheni kumchezea Mungu, ndoa takatifu ni unamuita Mungu awe pamoja na nyie mume na mke sio kucheza cheza unapete unakamada, umezaa nje sio mara moja, you're full of shit, unakera ila wanawake wazamani wanavumilia ujinga ili watoto wapate familia.

MISUKO SUKO IPO NA MAJARIBU PIA

Hiyo ipo na ndio muda wa kumuita Mungu akusaidie huenda umeoa mwanadada kisu sasa hajatulia anadanga, au wewe hujatulia ukawapa wadada mimba, au ndio mke hapati mtoto, au wewe huna uwezo huo, au hamueshimiani so kupigana mnapigana sana bila hitimisho.

HITIMISHO
ukitaka ndoa yenye amani na utulivu acha kujiona, penda kujishusha, mke asivuke mpaka wake, na wewe usivuke na yako.
Heshimianeni kitu ambacho siku hizi hakuna.

Kama huna period unasemaje umechoka tokea uolewe hadi sasa, mwanaume utasemaje na kazi anafanya tokea aoe. Wewe huna haki ya kumkatalia mkeo unyumba labda uwe unaumwa ila lazima umpe na mwanamke huna ruksa yakumnyima mumewe haki zake za msingi. Hiyo umefunga sheria.

Mapenzi ni raha na ndoa ni raha zaidi, penda kujishusha pale ukiona ndio inaenda hiyo. Kuachana sio solution.
Kutatua madhaifu yenu ndio ndoa iliyobarikiwa.

Siku njema.
 
Bila shaka mtoa mada ni "KE"
Vilevile uko jukwaani kumsemea either rafiki ama kaka hata shemeji.
Any way NDOA ina chagizwa na mambo mengi.Mi Binafsi ndoa imenishinda kwa makosa yangu ama pia ya mwenzangu.
Ila kama muda na kodi ya meza nlijitahidi sanaaa mpaka nikawa na madeni ili mradi mwanamke ale Nyama na anywe maji safi.Inshort every things i gave her.
Okay kikubwa kwenye ndoa hata ujitoe ama ujitume vipi lazima utafika sehem utakwama tu.
Ndoa haina formula.
Mi nilibeba Wife na mtoto mpaka Serengeti bata la week nzima nikakata kama Mil 10.
Lakini nlionekana kama Rubish japo now anatamani sana arudi kwangu baada ya kugundua nimemuacha Jembe.
Ukija jukwaani njoo na Core point to you're Topic.
NDOA KWA KARNE HII NI MZIGO
 
Back
Top Bottom