Ndoa za aina hii vipi,zinafaa??

mkuu ndoa ya kiserikali inaruhusu talaka(huvunjwa na mahakama), kwa hiyo kama unahitaji kuoa na kuacha basi funga ndoa kiserikali itakua rahisi kidogo kutimiza hiyo azma...
 
Nyani Ngabu sheria inatungwa kutokana na katiba,ni jambo gumu sheria kuwa tofauti na katiba

Ndo maana suala la mgombea binafsi wanataka liwepo kwenye katiba.Katiba iliyopo inazungumzia uwepo wa mgombea lakini sio binafsi.
Na kwenye ndoa ni hivyo pia,katiba inazungumzia ndoa lakini sio za mkataba.Kwa ufaham wangu ili sheria iruhusu ndoa za aina hii ni lazima jambo hilo lianzie kwenye katiba.
Inawezekana labda sielewi sahihi ndugu yangu,hebu nieleweshe!
 
Last edited by a moderator:
mkuu ndoa ya kiserikali inaruhusu talaka(huvunjwa na mahakama), kwa hiyo kama unahitaji kuoa na kuacha basi funga ndoa kiserikali itakua rahisi kidogo kutimiza hiyo azma...

Kuna tofauti kubwa kati ya ndoa hi na ndoa ninayoizungumzia mimi.
Ndoa ya mkataba haiitaji kwenda mahakamani ili ivunjwe,inajivunja yenyewe muda ukifika.Pia unakua unajua tangu mwanzo tarehe fulani nitakua huru,sio ghafla!
 
Mbona ndoa ya mkataba ipo tu na inatumika kwa watu wanaotaka,mkataba ni kati yenu wanandoa hivyo kama mnataka kufunga ndoa mnafanya mkataba wenu kabla ya kuoana na mara nyingi ndoa hizi ni zile wanazofunga watu serikalini.

Mh!Una uhakika?
 
Kweli kabisa Mtambuzi but kama kungekua na utaratibu wa mkataba wa muda fulani huoni kama huyo jamaa yako asingehitaji kutoa rushwa ili kuvunja ndoa?
Yaani angefunga tu ndoa ya muda ambao angekuwa masomoni kisha wakati anamaliza ndoa inakua imejivunja yenyewe bila haja ya kwenda mahakamani.
Unaonaje?
 
Last edited by a moderator:
Nisingesema kama sina uhakika,kama unataka kuwa na ndoa hiyo sema nikusaidie kuipata.

Sema hapa hadharani ili wale wanaotaka uwasaidie.
Najua hawawezi kusema ila wasaidie ili waweze kuanza mchakato!
 
Kuna tofauti kubwa kati ya ndoa hi na ndoa ninayoizungumzia mimi.
Ndoa ya mkataba haiitaji kwenda mahakamani ili ivunjwe,inajivunja yenyewe muda ukifika.Pia unakua unajua tangu mwanzo tarehe fulani nitakua huru,sio ghafla!

nimekuelewa sana azma yako mkuu na namna ya ndoa unayomaanisha.
Binafsi hii siwezi kuiita ni ndoa bali ni aina fulani ya ufuska hivi. Ninasema hivi kwa sababu ndoa ni agano la umilele, hakuna namna ukaunganisha nafsi mbili kwa kuwa tu tamaa ya kimwili au maslahi fulani yamewekwa mbele...
Kumbuka serikali kupitia sheria ya ndoa iliyopo katika katiba pia inampa nafasi Mungu na ndio maana wanaofunga ndoa bomani hula viapo kwa kushika vitabu vya Kiungu...
 
cacico hujawahi kucheat?
kuna mtu namvizia humu jf, ndio nataka tuanze rasmi kucheat! my 'secret admirer wangu' lolest! sina maana hiyo Eiyer, ila ni dhambi na kuendekeza zinaa, tujaribu kuzishinda tamaa za mwili, la sivyo ipo siku vitaombwa vibali vya kuingiza ndoa kati ta binadamu na punda kwenye katiba!
 
nimekuelewa sana azma yako mkuu na namna ya ndoa unayomaanisha.
Binafsi hii siwezi kuiita ni ndoa bali ni aina fulani ya ufuska hivi. Ninasema hivi kwa sababu ndoa ni agano la umilele, hakuna namna ukaunganisha nafsi mbili kwa kuwa tu tamaa ya kimwili au maslahi fulani yamewekwa mbele...
Kumbuka serikali kupitia sheria ya ndoa iliyopo katika katiba pia inampa nafasi Mungu na ndio maana wanaofunga ndoa bomani hula viapo kwa kushika vitabu vya Kiungu...
watu tunapenda kufanya yale yote yaliyo mabaya yahalalishwe!! ni tamaa tu za kishetani, ila tusiziruhusu zikatawala hivi!! mwisho watu watataka ndoa na di..l..do kwenye katiba! lolest!
 
watu8 unajua ndoa ina maana gani hasa?Inaonekana tafsiri yako ndo inayokufunga kwenye jambo hili,ukiamua kutoka kwenye hicho kiberiti utafunguka.

Ndoa ni mkataba ndio maana mnapewa "dokumenti" tofati ni namna sheria inavyoelekeza namna mkataba huo uwe!
 
Last edited by a moderator:
cacico ,umevunja mbavu zangu,ninamhisi huyo lazima atakuwa ni yule wa kule upareni kabisa . . . . .Lol!

Kiukweli ni kwamba tatizo letu uzinzi tunautafsiri kwa mujibu wa imani zetu.Hatuwezi kupata suluhu kuna watu wasio na dini na kuna dini tofauti pia,makundi yote haya yanatofautiana namna ya kutafsiri uzinzi.Hivyo tunapozungumzia uzinzi tunajifunga wenyewe.Lakini hawa wote ndo wanaocheat sijui hapa maana yake nini!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom