Ndoa za aina hii vipi,zinafaa??

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,702
Sijui au niseme sikumbuki kama jambo hili limewahi kujadiliwa hapa kwa mtazamo huu,kama tayari mnaweza kupotezea,kama bado tujaribu kuona kama lina manufaa kwetu
Nimepata wazo kuwa,katika mchakato wa kutafuta maoni ya katiba mpya mnaonaje kukawepo kipengele cha ndoa ya mkataba?(au kipo?Maana wengine hata katiba hatuijui achilia mbali kilichomo) . .Lol!
Nimewaza hilo kwa kuwa,kwa mtazamo wangu inaonekana hii mambo ya mpaka kifo kitutenganishe imewachosha wengi.
Ukitaka kuona ukweli huu angalia namna watu wanavyocheat si wanaume si wanawake ni vurugu mtindo mmoja.
Hata ndoa za mke zaidi ya mmoja nazo zimeshindwa kuondoa tatizo hili,huu ni ukweli.
Unakuta mtu ana wake wanne lakini ana nyumba ndogo 3!!!!
Hili ni tatizo.
Nawasilisha maoni,kuwepo na ndoa za mikataba,mnaoana kwa miezi mitatu,mnatafunana weeee,siku 90 zikiisha kila mtu na hamsini zake.Unang'oa kitu kipya au kama mzuka bado upo baina yenu,mnaenda ku-renew mkataba.
Nadhani hii itawapa fursa watu kubadili wenza mara nyingi watakavyo au vipi jamani?
Najua mnaweza kufikiri kuhusu dini na kudhani nimekuwa mpagani,lakini kabla hujanihukumu,fikiri kuwa wakati unamcheat mkeo/mumeo unakua unafanya hivyo kwa mujibu wa dini gani?
Sihalalishi kile dini inachoita dhambi bali wale wanaokubaliana na hii makitu wafanye kwa uhuru na uwazi!
 
Nadhani issue hapa si ndoa ya mkataba, bali ni aina ya kiapo kinachoapwa na wanandoa......!
 
Na kwanini unadhani hayatakiwi kuwepo?

Haya sasa...wengine wanataka katiba mpya ikataze lotion!

Katika hali iliyodhihirisha bado watu hawaelewi vizuri misingi ya Katiba kama Sheria Mama ya nchi, mwananchi mwingine alitaka ikataze kwa kuvitaja vipodozi vya kupaka 'losheni' zenye hatari kwa afya za wananchi, "Naomba Katiba ikataze kabisa ‘losheni' zenye kemikali za hatari zisiingie nchini, tena izitaje kabisa hizo losheni maana zinahatarisha maisha ya wananchi wanaotumia," alisema Charles Lubaza wa Peramiho.

Hata hivyo Mjumbe wa Tume, Ally Saleh alilazimika kufafanua kuwa, ikiwa hata losheni zitaingizwa katika Katiba kwa kutajwa kwa majina, basi Katiba hiyo haitabebeka.

Kaazi si kidogo.

Kutoka Wavuti
 
Nadhani issue hapa si ndoa ya mkataba, bali ni aina ya kiapo kinachoapwa na wanandoa......!

Nadhani hapa kuna ukweli fulani.
Lakini unadhani mtu anaweza kuapa kuishi nawe kwa miezi 6 halafu mahala anapoapa pawe ni kwenye nyumba ya ibada?
 
hili linahitaji marekebisho, kwani hata sheria za ndoa zilizopo hazikizi mahitaji ya raia,...najua utajiuliza nimejuaje?
usiwe mvivu pitia MARRIAGE ACT,2004 ambayo ndiyo imetokana na Katiba iliyopo sasa(1977)
 
Eheeeee utamu koleaa!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nyani Ngabu ,unadhani ndoa haina uhusiano na sheria?Hujui kuwa ndoa ipo kwa kuwa sheria inaruhusu na katiba ni sheria mama?

Sijaona mantiki ya wewe kuhusianisha nilichoshauri na maoni ya huyo alietaka katiba ikataze lotion!
 
Last edited by a moderator:
Koh koh! Sikubali wala sikatai hoja yako mkuu.

But nafikiri kinachotakiwa kufanyika ni kuhuisha(updating) sheria ya ndoa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nyani Ngabu ,unadhani ndoa haina uhusiano na sheria?Hujui kuwa ndoa ipo kwa kuwa sheria inaruhusu na katiba ni sheria mama?

Sijaona mantiki ya wewe kuhusianisha nilichoshauri na maoni ya huyo alietaka katiba ikataze lotion!
 
Last edited by a moderator:
uzinzi at work! hiyo yote ni tamaa! kuwa na mke/mume mmoja inatosha sana hasaaa kipindi hiki chenye maradhi mengi tu yatokanayo na uzinzi!
 
hili linahitaji marekebisho, kwani hata sheria za ndoa zilizopo hazikizi mahitaji ya raia,...najua utajiuliza nimejuaje?
usiwe mvivu pitia MARRIAGE ACT,2004 ambayo ndiyo imetokana na Katiba iliyopo sasa(1977)

Nyani Ngabu ,umeiona hii?
Nadhani itakusaidia kuondoa fikra kuwa mambo ya ndoa hayahusiani na katiba!
 
Last edited by a moderator:
Nyani Ngabu ,unadhani ndoa haina uhusiano na sheria?Hujui kuwa ndoa ipo kwa kuwa sheria inaruhusu na katiba ni sheria mama?

Sijaona mantiki ya wewe kuhusianisha nilichoshauri na maoni ya huyo alietaka katiba ikataze lotion!

Mantiki ni kwamba katiba haiwezi kutaja kila kitu.

Kuna mja hapo kasema sheria iliyopo labda inawezaa kuwa updated (na hii inaweza kufanywa bila kukinzana na tayari kilichomo kwenye katiba ya sasa).
 
Nyani Ngabu ,umeiona hii?
Nadhani itakusaidia kuondoa fikra kuwa mambo ya ndoa hayahusiani na katiba!

Sasa kwa nini hiyo sheria ya ndoa isifanyiwe nyongeza bila hata kugusa katiba?

Maana katiba tayari inatoa muongozo, na sheria zinazoongoza ndoa zipo tayari.

Hakuna mantiki wala haja ya katiba mpya kuzungumzia mambo ya ndoa za mikataba.
 
Mbona ndoa ya mkataba ipo tu na inatumika kwa watu wanaotaka,mkataba ni kati yenu wanandoa hivyo kama mnataka kufunga ndoa mnafanya mkataba wenu kabla ya kuoana na mara nyingi ndoa hizi ni zile wanazofunga watu serikalini.
 
Nadhani hapa kuna ukweli fulani.
Lakini unadhani mtu anaweza kuapa kuishi nawe kwa miezi 6 halafu mahala anapoapa pawe ni kwenye nyumba ya ibada?

Huko kwenye nyumba za ibada simo, kwa kuwa dini za siku hizi zimekumbwa na mkengeuko mkubwa kwa sababu ziko kibiashara na kimaslahi zaidi... Nadhani zile almaarufu kama za Bomani zinaweza kuwa na utaratibu mzuri wa kiapo ambacho kitaendana na matakwa ya wanandoa.

Kwa mfano kwenye miaka ya mwanzoni mwa 1990 nimewahi kuwa shahidi wa Ndoa ya bandia ya jamaa mmoja ambaye alitaka kwenda nje ya nchi nadhani kusoma lakini sharti ili apate nafasi hiyo ilitakiwa awe ameowa, hivyo tulipanga na mdada mmoja akakatiwa mshiko akakubali kufunga ndoa na baada ya kwenda nje na kupata alichotaka ndugu zake huku wakafanya michakato ile ndoa ikavunjwa mahakamani kwa rushwa na maisha yakaendelea na yule binti akaolewa na sasa ana familia yake
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom