Naomba msaada wa kuinusuru ndoa yangu(Naona ipo ukingoni...
Mimi ni baba mwenye watoto wawili(7 & 4) Nipo kwenye ndoa mwaka wa 8 sasa...
Nimeanza kupata matatizo na mke wangu yapata mwaka sasa kuhusiana na TENDO Zima la mchezo wa kitandani..
Kwakweli nimeshindwa hata kumuelewa,ANANIKATALIA kufanya mapenzi kwa visingizio kibao(Mara anasikia usingiz sana,mara hajisikii,mara amechoka sana)..Yaani ndani ya huu mwaka sijawahi kufanya naye mapenzi kwa ridhaa yake bila kumlazimisha kwanguvu)..
Yaani imefika wakati nika amua kumsaidia kazi zoote za nyumbani(Kufua kupika na kadhalika) Ili mradi akifika nyumbani asifanye kazi yoyote ya kumchosha..LAIKINI haija saidia kitu..
ANASEMA HANA HAMU KABISA HATA MWAKA UNAWEZA KUPITA BILA KUFANYA MAPENZI(WALA HAONI TAABU)..
Mwanzoni alikuwa akifanya kazi mjini(Akiondoka alfajiri na kurudi Jioni sana)..Sasa nimemfungulia salon hapa hapa maeneo ya nyumbani(Yote hiyo ni kujaribu kumpunguzia uchovu anosema ndio unamfanya akose HAMU.. Lakini haijasaidia kitu..
Kusema ukweli hii hali imenichanganya sana..( Mimi si mtu wa kutoka wala sijawazia jambo hilo) Lakini nitaishije bila kupata haki yangu ya ndoa??? Na mke ninaye???!
JAMANI NAOMBA USHAURI HATA KAMA NI WA KITABIBU : MAAANA HATA KAMA ANATEMBEA NA MTU MWINGINE(HATEMBEI NAYE KILA SIKU) LAZIMA KUNA SABABU ZA KIAFYA ZINAZOMFANYA HAKOSE HAMU...
YERICKO NYERERE - Ahsante sana kwa ushauri wa kina...Na mapendekezo ya kufanya..Hakika nitajaribu kumtoa out ..out(Mimi si mtu wa kutoka out sana...."Mara chache sana)..Kuhusu lugha ya kumtoa nyoka pangoni( Nayo nitajaribu--Ila yeye huwa si mtu wa kunisikiliza hata kama namwimbia wimbo anasema namchosha)..!
Ahsantela personalities tutafanyaje? nipe mahali pa kuanzia kufanya personalities zi-match!!Nyie mna tatizo la kutofutiana personalities. Sasa hata kama unamuimbia anachokaje jamani? Ama unamuimbia myimbp za rose mhando zile za kurusha kichwa kama madogoli?
Zungumza nae taratibu akuamboe unamkera kwa nini. Lakini tahadhari, sio lazma ubadilike jumla ili utate tendo la ndoa. Baada ya hapo labda mue de hoapitali kama mlivyoshauriwa awali. Manale walau mara moja kwa mwezi angekutamani aisee.
Ahsantela personalities tutafanyaje? nipe mahali pa kuanzia kufanya personalities zi-match!!
Jaribu kumsoma mwenzio ujue ni vitu gani vinamfurahisha zaidi kusudi muendane. Angalia mziki anaosikiliza, labda ujadiliane nae pia. Kwani hamna nafasi ya kucheza pamoja? Mfano muulize anataka kuimbiwa wimbo gani na kama hauujui basi muimbe pamoja nk.
Ngoja kwanza, wakati ambapo unamsaidia kufua na kupika ili asichoke yeye anakuwa saluni. Ina maana wewe haufanyi kazi yoyote?
NYANI GABU - Ahsante kwa ushauri wako na angalizo( Natumia muda wangu mwingi kumuuliza namna gani anataka niwe au nifanye ili ajisikie,lakini sijafanikiwa) Suala la kunuka makwapa ua mwili sina tatizo hilo kabisa(Niapenda usafi na ninazingatia usafi wa mwili na mavazi.)
Usafi wa kinywa je?