Ndoa yangu inakaribia kuvunjika,msaada jamani

Ndoa yangu inakaribia kuvunjika,msaada jamani

Ni hivi hao madada sio wajinga ni wajanja sababu wao ni wamachame na wanawake wa kimachame wanajulikana sana kwa mchezo wao wa kuua waume zao wanapofanikiwa,hivyo wanajihadhari mapemaa wakijua kuwa na wewe unaweza ukamfanyia hivyo hvyo kaka yao halafu mtoto watoto hao wakarithi mali zake na mama yao.

ki ukweli hii mila ya kuua waume zao pindi watoto wakiume wakishazaliwa ndio naisikia leo kuwa ipo pia kwa wapare,ila wadau kama mtakubaliana na mimi siku zote lisemwalo lipo inawezekana ikawa ni mila yao ya ndani kwa ndani huko iliyfichwa wanayoijua wao/best preserved secret,mana wapare ni almost kabila moja na Wasambaa na wazigua na hawa pia wanamtindo wa wanawake wao kuwaua au kuwatengeneza waume zao.Sasa inawezekana kabisa kwamba hii mila iko huko kwa wapare labda haswa pale wanapoolewa na makabila tofauti labda huwa wanaitumia sana na hao dada zake mme wako wanaijua hii na ndio maana wanajihadhari mapema mana hawajui yaliymo moyoni mwako.Au inawezekana ikawa ni mila iliyokufa ya zamani ya wapare/dead custom ambayo nayo pia wanaijua mana mkae mkijua siku zote mchawi anamjua mchawi mwenzake na mwizi anamjua mwizi mwenzake siku zote,mana kama mtu ni muuaji basi utawaambia hata watoto wako fulani na fulani pia wanatabia ya kiuaji au ukoo fulani ni wa kiuaji ili wawe na tahadhari mapema
 
Mimi ni mpare na mume wangu ni mchaga (MMACHAME)....ndoa yetu ina miaka 6 na miaka yote tumeishi kwa furaha na upendo..Mumgu ametujalia watoto 2 mkubwa 5yrs wa kike mdogo 3 month wakiume...Toka nijifungue mtoto huyu wa kiume mume wangu amepunguza mapenzi na mimi na wala hampendi kabisha huyu mtoto,Nilipomuuliza anadai dada zake wamemweleza kuwa kuzaliwa kwa mtoto huyu ndio mwisho wa maisha yake,Eti mimi nitamuua sbb wapare wanatabia ya kuua waume zao punde wapatapo watoto wa kiume. Yn naumia sana roho kwani nilidhani mtoto angekua furaha kwa mume wangu kumbe amegeuka hofu kwake,Nifanyaje jamani

Hao dada zake hawako mbali na ukweli.
Nakumbuka miaka ya tisini(1990s) wanaume wenye kujiweza kifedha wengi ambao walioa wanawake wa kimachame walikuwa wanauawa na majambazi mara baada ya mtoto wao wa kiume kufikisha umri fulani.
Wachaga wasio wa machame walikuwa wanaamini kwamba mke wa kimachame akiwa na mtoto wa kiume aliyefikisha umri fulani, huwa anakodisha watu kumuua mumewe, akijua kwamba mwanae wa kiume atamsaidia kuendeleza hizo mali alizoacha mwanaume, na yeye atakuwa free kudili na watu tofautitofauti, kwa sababu huwa hawapendi kuwa chini ya mtu.

Kwa hiyo hao dada zake wanawa-judge wanawake wa makabila mengine kwa kuangalia tabia za mwanamke wa kimachame.
 
eeh dada wewe hayo wengi yameyakuta sio wewe tu mpare.
Kuna rafiki yangu wa kinyamwezi ameolewa na mchaga, alianza na wakike 2, akaja wakiume.
Shemeji zake, wifi zake wakambadilikia, na kumloga kwa sababu kamzalia kaka yao mtoto wa kiume, ndio walikuwa wanataka kumua wifi yao ili kaka yao awe hai.
Akivo sema huyo mwanamke wa kinyamwezi juu ya wachaga.


Lakini nimeskia wapare nao pia wanamchezo huwo, hawapendi kaka zao waoe kabila lingine.
Kuna rafiki yangu mmoja wa kipare alinilalamikia juu ya dada zake. Jamaa alitaka kuoa mkenya mkikuyu, akaja dada ake akamuambia hasimuoe sababu akiwa na mali atamua. Wale dada wakawa wanamuambia kaka yao ela zote apeleke nyumbani kwao upareni. Kesi za wachaga, wapare na wakikuyu zinatisha sana, tena sio za kibinadam kabisa.
Zinakatisha tamaa, ndio maana makabila mengine uogopa kuoa ama kuolewa na makabila hayo. Samaani sana dada kwa maneno yangu.
Watu wanao weka mali mbele na ubinadam nyuma lazma wafikiriane vibaya.

Kama mkristo nenda kwa mchungaji kamueleze hayo, alafu waitwe wote madada na mumeo, uwaulize kwanini wanakufikiria vibaya, na wakuambie mpare gani huyo aliewai kuua mumewe eti kwa vile kamzalia mume mtoto wa kiume. Waulize unatatizo gani walilo liona wao mpaka umuue kaka yao!!!
 
Mmeo anahisi huyo mtoto wa kiume sie wake wala sio jambo lingne jiulize wakati wa mimba hamkuwa na hata kaugomvi au safari ya kuwafanya muwe mbali?
 
haya unayoyaongea
umeyasikia ila huja proove kam ni kweli yanatokea.
nina kaka 1 na tupo dada 5 hatujawah hata kumuuliza wifi anaish vipi na
mumewe. sembuze kumtilia bifu??? bifu ni aina mtu na sio kabila.

ukisikia wadandia treni kwa mbele ndio hao na kama sie tunawauwa ,mbona hodi haziishi kuja kutuoa?
 
Ingekuwa mie ndo ningemwekea sumu kabisaa ajifilie mbali, asiniletee mie hadithi za dada zake ambao wanaona hedhi kama mie, kama anawaamini sana kila wanachosema, basi awaoe
 
Mtoto tu wa kiume? hapana hapo kuna jambo jingine. Una uhakika huyo ni mwanae au ulichomoa pengine? au umeshaanza kuwa na macho mawili?. Tafadhari wanajamvi mubaneni vizuri huyu asije kuwa anatumalizia bundle zetu kwa ujinga wake.

yaani!
nami nina maswali kama hayo.
Hiyo sababu ya mumewe kuwa mkorofi asiye na upendo haileti hata kdg.
 
pole sana dada sasa huyo mumeo alitaka uzae watoto wakike tu, duh imani zingine bana zinachosha. yaani mtu anamwazia mkewe kuwa atamwua Mwombe Mungu atakusaidia.
 
Ingekuwa mie ndo ningemwekea sumu kabisaa ajifilie mbali, asiniletee mie hadithi za dada zake ambao wanaona hedhi kama mie, kama anawaamini sana kila wanachosema, basi awaoe

na wewe dada zake wanakuondoa ukimwua kaka yao kwani hiyo michezo si ndio ilianzia kwao??
 
.dah wanaume wengine hopeless kabisa........

hopeless kivipi kwani wewe wa2 wakikuambia mume wako ananyonya damu za wa2 hautahacha kuogopa??
hao wa pare huo utakuwa ndio mchezo wao sasa unabisha nini we umeshaambiwa hiyo njia ina simba anakula wa2 sasa wewe utaacha kukaa mbali na hiyo njia kama wewe unaogopa kufa kwa nini yeye asiogope pia??
 
Mh, jamani unaweza kuolewa koo nyingine ukajuuuuuuuuuuuta kujifaham na kilichokutoa kwenu.
 
Back
Top Bottom