ndoa yamtesa Dr. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ndoa yamtesa Dr. Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kabewa, Sep 1, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Kabewa

  Kabewa Member

  #1
  Sep 1, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa bado anateswa ‘ishu’ ya ndoa na sasa kila anapokwenda kujieleza, analazimika kutoa ufafanuzi kuhusu mke wake.

  Uchunguzi wa gazeti hili tangu vuguvugu za kempeni za Uchaguzi Mkuu 2010 zianze, umebaini kuwa Dk. Slaa amekuwa akiulizwa swali kuhusu ndoa yake kutokana na kuwepo na taarifa za mkanganyiko kuhusu mambo yake ya kifamilia.

  Imebainika kuwa swali kuu kwenda kwa Slaa ambalo limezua matawi mengi ni kile kinachojulikana na wengi kwamba mke wake, Rose Kamili ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, aliyewahi pia kushika nyadhifa kadhaa ikiwemo udiwani.

  Katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM, Rose aligombea ubunge lakini kura hazikutosha na kukawa na taarifa kwamba alitishia kuhamia CHADEMA kumfuata mumewe (Slaa).

  Jumamosi iliyopita kwenye Kipindi cha Jicho Letu Afrika cha Radio Clouds FM, Slaa alisema kuwa Rose kwa sasa si mke wake na kwamba mke wake mpya anaitwa Josephine Slaa.

  Slaa, akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho, George Njogopa alisema, suala la Rose lilizua mgogoro mkubwa lakini hatimaye waliachana na yeye kupata mke mwingine.

  “Ni demokrasia, sikuwa na sababu ya kumbana ndiyo maana nilimuacha aendelee na majukumu ya chama chake. Hata hivyo, ni vizuri watu wakatambua tofauti za ndani ya chama na familia,” alisema Slaa.

  Wakati akizungumza hivyo redioni, baadaye siku hiyo akiwa Uwanja wa Jangwani, Dar katika uzinduzi wa kampeni zake za urais, Slaa alilazimika kumpandisha mkewe jukwaani ili kutuliza ‘mzuka’ wa mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi.

  “Jamani ndiye mke wangu, anafanya kazi kubwa sana kunitunza na hasa katika kipindi ambacho nilikuwa nimeumia mkono,” alisema Slaa na kumtaka Josephine asimame ili awasalimu wapigakura.

  Hata hivyo, wapigakura walilalamika kwamba Josephine alisimama mbali, hivyo akaombwa kusogea karibu na kupunga mkono.

  Katika uchunguzi wetu, suala la ndoa ya Slaa limekuwa mjadala ndiyo maana amekuwa akilazimika kutoa ufafanuzi mara kwa mara ili jamii ijue ukweli kwamba yule wa zamani hayupo naye tena.

  Inafunuliwa kwamba jitihada za Slaa kutaka jamii ijue yeye hayupo na Rose badala yake amemuoa Josephine ni kutaka dhamira yake ya kupingana na Chama Cha Mapinduzi isitiliwe shaka na wapigakura wenye kiu ya mabadiliko

  Source Global publisher
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,920
  Likes Received: 12,112
  Trophy Points: 280
  Hata Kikwete inamtesa angalia signature yangu

  [​IMG]
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  [​IMG]


  [​IMG]
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Rose kamili si kada wa CCM, fuatilia mambo kwa karibu. Yuko Chedama na anagombea ubunge Hanang
   
 5. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kama upadri na ndoa vimemshinda, ataiweza serikali?! Sidhani
   
 6. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2010
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  CCM wawe makini na wasifurahie kwani wa kwao ndo mchafu zaidi na naamini watu wanatunza heshima ya cheo cha URAIS lakini siku paka atakapotoka kwenye pakacha watu hawataamini.
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  dah sijajua hii picha ni ya rose kamili au Eva
  Kama ni rose na Slaa kaacha mzigo basi niPM contact za huyu mwali ili nami nitangaze mgogoro na ndoa yangu, kama ni Eva basi kuna kila hali ya mtu kukwama kihalali hapo.
  Mie simo
   
 8. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,920
  Likes Received: 12,112
  Trophy Points: 280
  Ndoa nyingine hii hapa mwali siju ndiye yupi

  [​IMG]
   
 9. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Personal attacks sio nzuri...
  I don't recommend campaigning this way.
  Madhara yake huwa sio mazuri...

  Naomba mods waitoe hii, vitaanikwa vitu tusivyopaswa kuvisikia...
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hivi mkapa alikuwa na mke wakati anajiandaa kugombea...nasikia aliachiwa mke na pesa mbili mramba...maana alipaswa awe na mke...swali je mkapa aliweza kuwaongoza watanzania? ukilinganisha na huyu mwenye wake lukuki...
   
 11. minda

  minda JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  siyo kweli. hayo ni maisha binafsi ya WS na wala siyo siasa.
   
 12. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,920
  Likes Received: 12,112
  Trophy Points: 280
  Who is this and for whome

  [​IMG]
   
 13. Zungu la Unga

  Zungu la Unga Member

  #13
  Sep 1, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na hii nayo ni ndoa?
  jk-11.jpg jk-32.jpg jk-21.jpg
   
 14. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  One of the Slaa's concubines.
   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,920
  Likes Received: 12,112
  Trophy Points: 280
  Umekosa, nipe mji ila naomba Mods asije akafuta hii thread.
   
 16. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Naomba kukusahihisha kwa nia njema kabisa.
  Kwa mujibu wa Kanisa Katoliki, baada ya kupata Sakrament ya Ubatizo hadi Kipaimara; Sakrament inayofuata ni aidha ndoa au Daraja takatifu (Upadri, Usister, Brother). Uwezi kupata daraja la Upadri na hapo hapo ukafungiwa ndoa, vile vile huwezi kufunga ndoa na ukapata daraja la Upadri. Nachotaka kusema Rose Kamili ni mzazi mweziwe na Dr Slaa lakini hawajawahi kuwa na ndoa inayotambulika Kikanisa kwa kuwa Dr Slaa alishapata daraja la Upadri hawezi kufungiwa ndoa
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  EVA wa JMK....
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...