Bila shaka haina masharti sana maana kuna jamaa yangu leo hii ameenda ofisi za RITA kuulizia taratibu za kupata cheti cha ndoa. Afisa msajiri akamwambia anatakiwa aende na mkewe huku wote kwa pamoja wawe na copy za vitambulisho vyao wanalipia ada ya kuandikisha ndoa kisha matangazo yanawekwa kwenye mbao za matangazo kwa siku 21 baada ya halo wanaenda kuchukua cheti
Kama kutakuwa na jingine wadau wataongezea
Ndoa ya serikali kama zilivyo ndoa nyingine zinazofungwa hapoa Tanzania kama vile za madhehebu ya kidini, zinazofungwa kimila zote zinzsimzmiwa na sheria ya ndoa ya mwaka 1971. Baadhi ya masharti muhimu ni pamoja na
1.Ndoa ni lazima itangazwe kwa siku 21
2. Siku ya kufunga ni lazima wanandoa waende na mashahidi wao
3. Ndoa lazima iwe kati ya mwanaume na mwanamke wenye umri iliokubaliwa kisheria
4. Siku ya kufunga ndoa wanandoa watakula kiapo na kusaini vyeti vya ndoa
5. Masharti mengine ni kama yalivyo fafanuliwa kwenye sheria ya ndoa ya 1971
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.