Ndoa ya Kihistoria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa ya Kihistoria

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by EMT, Jun 20, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  WAZEE wawili wakazi wa Mji wa Namanyere wilayani Nkasi, mkoani Rukwa, wameandika historia ya pekee ndani na nje ya nchi kwa kufunga ndoa wakiwa na umri mkubwa kuliko kawaida. Wazee hao, Mathias Kisokota (94) na Uria Mwimanzi (80) walifunga ndoa hiyo ya kihistoria katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Antony, Parokia ya Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa. Ibada ya ndoa hiyo iliyofungwa jana, iliongozwa na mapadri wawili ambao ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Katindi na Twamba Peter.Ndoa hiyo ilivuta hisia za watu wengi kiasi cha kufurika katika kanisa hilo kwa lengo kushuhudia wazee hao wakifunga ndoa.

  Kabla ya Ibada hiyo kufanyika nyakati za saa tisa mchana, gumzo katika Mji wa Namanyere, Sumbawanga na Mpanda ilikuwa ni juu ya kufungwa kwa ndoa hiyo ambapo wakazi wa mjini humo walisikika wakieleza kuwa hii itakuwa historia kwa wazee kufunga ndoa wakiwa na umri mkubwa kiasi hicho. Wazee hao ambao wamefunga pingu za maisha kwa kuamua kuwa mwili mmoja kama maandiko ya vitabu vya dini yanavyoeleza, wana watoto wapatao 10 na wajukuu zaidi ya 50 ambapo walianza kuishi pamoja miaka 35 iliyopita baada ya kufariki mke wa kwanza aitwaye Agnes Kasinsila. Hata hivyo baada ya mzee Kasokota ambaye ni Mkatoliki kuanza maisha mapya Uria anayesali Kanisa la Moravian mpaka sasa, waliendelea kusali kama kawaida, lakini wakikosa baadhi ya huduma za kanisa.

  Katika mahubiri yake kanisani hapo, Padri Twamba alisema kuwa hiyo ni changamoto ya uwokovu hasa kwa vijana kubadilika kitabia na kutenda matendo mema na ya kumpendeza mwenyezi Mungu hasa kipindi hiki ambacho Jimbo Katoliki Sumbawanga linajiandaa kusherekea Jubilee ya miaka 125 tangu kuanzishwa kwake. "Hii ni changamoto ya uokovu hasa kwa vijana kubadilika kitabia na kutenda matendo mema ya kumpendeza Mungu..... ni faraja kwetu katika umri wa wazee hawa wameamua kufanga ndoa, tena kipindi ambacho tunajiandaa kusherekea Jubilee ya miaka 125 tangu kuanzishwa kwa jimbo letu," alisema Padri Twamba.

  Mjomba wa wazee hao ambaye ndiye msemaji wa familia hiyo, Filibert Lumbert alisema wazee hao pamoja na kwamba wameanza kupoteza baadhi ya kumbukumbu muhimu katika akili zao, lakini walisisitiza kila mara kwamba lazima wafunge ndoa kanisani ili waweze kupata huduma zote muhimu za kanisa kama ilivyo kwa Wakristo wengine hususani Wakatoliki. Huduma ambazo wamekuwa wakizikosa ni pamoja kupokea mwili wa Kristu (Sakramenti takatifu) na pia waliamini wakiendelea na maisha ya bila ndoa wanaweza kuzikwa nje ya makaburi ya Wakristo wakatoliki kitu ambacho si sahihi kwao. Hata hivyo ndoa ya wazee hao ambayo ilifana sana, sherehe zake hazikuishia kanisani badala yake zilikwenda hadi ukumbini ambako watu waliwapongeza kwa kuamua kufanya tendo hilo muhimu katika maisha ya wanadamu.

  Mwananchi
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Impessive!!! Nimejifunza mambo mawili muhimu ambayo kila mmoja aweza angalia kwa jicho lake..

  1. Nimejifunza kua kama mmekutana na mtu na mnapendana kweli sometimes it is better kujiangalia wenyewe wawili bila kujali kama dini inaruhusu au lah! Kwamba kuishi kwa amani na upendo kati ya wawili la muhimu ni makubaliano na mipangilio yenu. wameishi kwa mda wa miaka 35 pamoja... wamejaliwa kupata watoto na wajukuu, Mungu huyo huyo kawalinda, kawaneemesha kawabariki mpaka wamefikishana uzee na hatimae kuoana.
  2. Nimejifunza kua no matter una furaha na amani kiasi gani.. au umebarikiwa kiasi gani.. ni muhimu kua at the end of the day ukumbuke Mungu yupo na ujiandae safari ya kuenda kutana nae pale utapofariki.
  Hata hivyo wakichuliwa kama mfano kwa vijana, inakua kama kuwashawishi si lazima waoane na wenza wao ili kuishi pamoja ambayo kidini ni dhambi... hata hivyo we are living in this difficult world ambapo mambo sio black and white tu!

  Kwa kweli wamebarikiwa wastahili pongezi... angalau wana uhakika wa kufa na kuzikana...
   
 3. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hongera zao!
   
 4. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #4
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  True love waoooo
   
 5. v

  vivimama Member

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 6. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Sometimes tukio kama hili linakufanya ukae chini na utafakari maisha yako, upendo wa kweli unapatikana katika hali ya umri wowote, hawa wazee wangeweza kupuuzia na kuona kama washamaliza maisha yao ila wakaangalia na kuona yapaswa kuoana, kwa kweli inatia moyo kuonyesha unaweza furahia maisha katika umri wowote,Hongera zao Mungu awazidishie umri wa kuishi ili waendelee kufaidi raha ya ndoa yao
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  at that age, is it about love - living together au tendo la ndoa?
   
 8. Dinnah

  Dinnah JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mpaka raha
   
 9. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mmeona eh kwa hiyo watu wasijilaumu eti mie umri unaenda sijaolewa! Utakuja olewa tu hata kama ukifikia 90's
   
 10. CPU

  CPU JF Gold Member

  #10
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sasa kutana na kijana wa sasa mwenye miaka 32 ofisini kwetu, kila mdada anaekutana nae anamwambia " Nataka kukuoa, si unajua umri umeshaenda, nataka kukuoa dada, Hakya Mungu tena, wala sikuchezei . . . . Ukikubali tu tunaenda home kesho

  Au kutana na mdada wa miaka 29 akimwambia kila mwanaume anaemfuata "Utanioa, eeeeh??? Utanioa lakin??"
   
 11. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Yaah, hawa inabidi waingie vitabu vya Guiness records. Mungu awabariki sana.
   
 12. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  hatimaye wameamua kutubu dhambi zao za zinaa kanisani & uzeeni... nice move btw!
   
 13. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hongera.....nafikiri wanatafuta kuzikwa kwa heshima ya kanisa..

  Kwa taratibu za kiserikali, hawa ni mume na mke toka miaka 35 iliyopita..
  wana watoto 10...????

  Inabidi nikajifunze tena nini maana ya ndoa?
   
 14. j

  jumanne kabwela Member

  #14
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  love birds
   
 15. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #15
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  Katika this confused world ya sasa... maana ya ndoa inabadilika kila siku... Sometimes in a bad way.. saddening..
   
 16. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Discuss
   
 17. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #17
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Dear Gaga maana imebadilikia in this sense...

  Marriage zamani ilikua na maana a union between a man and a woman/a man and women
  kiasi kwamb watoto woote wataozaliwa kati ya hao wahusika watatambulika katika jamii
  kama watoto halali wa wanandoa hao. BAHATI MBAYA saana hii maana imebadilika saana
  katika maeneo mbali mbali ya ulimwengu...

  Sasa hivi kuna ndoa nyiiingi!!! Kuna ndoa za same sex marriage (gays and Lesbians..),
  kuna ndoa za mkataba mpaka mwaweza kubaliana hamna kuzaa, kuna ndoa za
  kupata tu Uraia, kuna ndoa kati ya wanawake na wanaume pia....

  Tokana na changes hizo hapo juu kupelekea aina kibao za ndoa (naamini bado wanajaribu vumbua nyingine...)
  Hapa dear tutasema kweli ndoa ni nini?? Kazi saana.. tunapofafanua NDOA, tutumie vigezo gani?? Vya DINI??
  Vya ulimwengu?? Vya kimagharibi?? (maana hawa ndo wabaya.. because they run the
  world basi kila lipitishwalo wanataka li apply koote.. i.e.. same sex marriage)

  Kazi kweli... Hivyo narudi tena kumsupport kaka hapo juu... kuna umuhimu wa kuangalia upya maana ya ndoa.
   
 18. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kweli hapo nimekuelewa ashadii,.... maana siku hizi kuna ndoa hadi za mikataba, maana ya ndoa imebadilika sana, kila mtu anaichukulia kivyake tu
   
 19. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #19
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Sijui tunaelekea wapi... nina wasi huko mbele wataruhusu hadi INCEST
  maana maadili yanakufa, unyama kujaa saana... Dah!
   
 20. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nilivutiwa sana na habari hii nillipoisikia inasomwa kwenye kipindi cha magazeti redioni asubuhi, hapa twaweza kuona kiapo kisicho hila wala mawaa kwakuwa kama ni uaminifu na au kufa kuzikana vitatimizwa na wawili hawa bila mashaka.

  Wamesubiri na hatimaye wametoa kiapo cha kweli mbele za Mungu wao, laiti ingekuwa tunamiliki uhai yaani tuna uhakika wa lini tutaitwa na Muumba, huu ungekuwa utaratibu mzuri kuliko tunavyofanya siku hizi na hizi unsustainable marriages!
   
Loading...