Shamali ndugu yangu, alichokifanya jamaa yako si sahihi. Na hii hupelekea kuwaumiza zaidi watoto wasio na hatia. Ni ubinafsi wa hali ya juu kwa mume kuamua kuzaa nje kwa matatizo ya uzazi ya mke wake. Je, ingalikuwa ni yeye mume mwenye matatizo, angelikubali mkewe kudungwa mimba nje kwa siri na kumzalia watoto wawili wasio wake ki-baiolojia? Unaweza kukuta jamaa kashauriwa na washkaji kijiweni kuwa "lazima utoe copy" lakini matokeo yake ndoa yake halali iko matatani. Ni kwanini jamii inategemea mke akubaliane tu kuchukuwa watoto wasio wake na waliozaliwa kwa usiri nje ya ndoa? Nadhani ndoa ni zaidi ya watoto ingawa watoto ni sehemu kubwa ya ndoa. Mungu ana wakati wake wa kumzawadia mtu watoto kwa hiyo wanadamu tusitafute short-cut na justification kwa uzinzi wetu. Mwisho mnawaharibu watoto malaika wa Mungu bure kwa kuwachanganya manake hawajui wapi wanastahili kuwapo.