Ndoa sio mbaya kama watu wengi wanavyofikiri

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,576
18,894
Tatizo la ndoa linaanzia kwenye watu wenyewe wanaoingia kwenye hiyo ndoa.Maranyingi tunakosea kwanza kwenye kuchagua mwanamke au mwanaume tunapenda kuangalia sifa za nje zaidi unakuta mwanaume ana mpenda mwanamke kwasababu ya umbo lake au sura bila hata kuangalia mambo mengine yatakayosaidia kuimarisha uhusiano wenu.

Mfano mzuri ni ndoa ya brother wangu, bro wangu baada ya kukaa miaka 5 ya uhusiano na mchumba wake ikabidi aamue kumuoa lakini akakutana na changamoto upande wa ndugu zetu walikuwa hawampendi mwanamke wake na sababu kuu ni huyo mwanamke kutojichanganya na ndugu wa familia yetu.

Kuna kipindi ndugu zetu wakawa wanamlisha mama yetu maneno ya kumchagua mwanamke wa bro ili tu ndoa ya bro isifanyike na bro amuwache huyo mwanadada bahati nzuri mama alikuwa stability akawakubalia bro na mwanamke wake wafunge ndoa.Bro wangu ana miaka 30 wakati mwanamke wake ana miaka 27 baada ya ndoa bro wangu alifukuzwa kazini kwa kesi ya kutengenezwa sababu kubwa ya kutengenezewa mazingira ya kufukuzwa kazi ni my bro alikuwa mchapakazi na pia alikuwa anapendwa na boss kuliko mtu yoyote pale kazini kwamaana nyingine alichukiwa kwa sababu ya wivu so akakaa miezi 10 bila kazi so mke wake ndo akawa ana hudumia hapo me nikiwepo cos bro aliniomba nikae kwake cos ni karibu na chuo ninachosoma pamoja na kukaa kwangu pale sijawahi kuona mke wa bro akimdharau bro au wakigombana maana Kuna wakati mwingine mke wake anampa hela akitoka na marafiki zake au wageni wakija ili kulinda heshima ya bro.

Ukiachana na hayo mke wake akamfungulia duka bro Ili angalau apate pakujishikiza maana bro alitafuta kazi kwenye hiyo miezi 10 bila hata kupata.Bahati nzuri mwaka Jana mwezi wa 11 bro akabahatika kupata kazi ya kuuza magari aliconnectiwa na mke wake na biashara ilikuwa inaendeshwa na mjomba wa mke wa bro.

NB: To be honest napenda Sana ndoa ya brother na mkewe wanaishi vizuri mpaka Raha kitu Cha msingi sisi wanaume tujifunze kuchagua wanawake sahihi wakuingia nao kwenye ndoa sio wanawake wote ni wapumbavu wapo ambao ni waerevu.
 
Juzi kati ulitoa mfano huu huu ila uliweka wahusika ni wazazi wako leo imekua ni bro wako upo vizuri
Sisi familia yetu hakuna mwenye tatizo la ndoa kuanzia wazazi wetu mpaka Kaka zetu labda me na mdogo wangu ndio tuharibu record nzuri ya familia maana sisi ndio pekee hatujafikia umri wa kuoa.
 
endelea kukariri dogo....watu wana ndoa but wanapiga PUNYETO kama mbwa wa polisi...
Jaribu siku kuingia kwenye ndoa na mtu sahihi ndo utajua utamu wa ndoa mbona Kuna ndoa Zina amani na zinaishi kwa upendo tatizo mnaangalia Sana ndoa za celebrities ambao most of them wanaishi kwa kuigiza na waleta ustar mpaka kwenye ndoa.
 
Jaribu siku kuingia kwenye ndoa na mtu sahihi ndo utajua utamu wa ndoa mbona Kuna ndoa Zina amani na zinaishi kwa upendo tatizo mnaangalia Sana ndoa za celebrities ambao most of them wanaishi kwa kuigiza na waleta ustar mpaka kwenye ndoa.
nyingi usanii......wakifika home kila mtu na room yake...chakula kila mmoja anapika kivyake.......wengi wanakufa na tai....sio kwamba nasema ndoa ni kitu kibaya hapana........ziko chache sana.....nyingine kuna mmoja ni mtumwa....kisa watoto.....tatazo wengi wa vijana wanafikiria ndoa ni kukazana tuu....NDOA NI LIFE......usipojipanga utapangwa.....na utakoma kupangwa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom