Ndoa ndoano, nani tatizo?

Ndoa ndoano, nani tatizo?

Kwenye ndoa mwanaume ndo anaweza kuwa chanzo kikubwa hasa tabia za kuchepuka na kutotekeleza majukumu yake katika maisha ya kawaida.Mwanamke akiridhika na mumewe hawezi kuwa na tamaa wala tabia mbovu anamtii na kumheshimu mumewe anachoambiwa na kushauri
 
Tatizo kubwa ni maharusi baada ya kusema YES I DO na kumalizika honeymoon kwa jina maarufu mwezi asali, kila mtu anaanza kumuona mwenzie adui. Yale yote waliyokuwa wakiyafanya wakati wa uBF na uGF na hadi kuamua kufunga pingu za maisha TUPA KULEEEE kila mtu yuko busy na mambo yake, na marafiki zake. Hana time na mkewe/mumewe. Nimechoka, nina safari zangu etc ndiyo yanakuwa maneno ya kila siku ndani ya ndoa. Na badala ya kukaa chini na kuongea kila mtu anaanza kujenga hasira za kufa mtu dhidi ya mwenzie na uadui unazidi kujenga mizizi ndani ya ndoa.

Na siku hizi tena na social media mume/mke huyo mbio mitandaoni kwenda kumuanika mwenzie huyu hivi huyu vile na mara nyingi hata kabla ya kujaribu kuongea na mwenzie ili wawekane sawa na hivyo kuifurahia ndoa yao.



Tafiti nyingi zinaonesha kwamba wanaume wengi huingia kwenye ndoa bila ya kutarajia, wakati wanawake ni moja ya mipango yao ya maisha tangu wakiwa washichana wadogo. Kwenye ndoa wanawake wanakuwa na mipango tofauti sana na wanaume. Ukija stuka wote hawaitamani ndoa nyumba inakuwa kama jela vile.

Ni nani hasa kati ya mwanamke na mwanaume ambaye anasababisha hadi ndoa ionekane ni taasisi yenye dhahama nyingi kuliko raha?
 
Anatakiwa ajiongeze vipi. Au ile hoja kwamba wanawake wa siku hizi mnapenda Pesa na si wanaume wanaowaoa ina ukweli fulani?
Hapana mkuu,maisha ya ndoa ni zaidi ya pesa,
Mwanaume hatakama hana pesa lakin anaonesha kuijali familia,kushirikiana na mkewe ki mawazo,kuwa karibu na mkewe,inajenga upendo.
Lakin sasa unakuta mwanaume anatoka asbh kwenda kazini akirudi breki ya kwanza bar, utamuona hapo nyumbani saa 4usiku hapo ndo kawahi,na akifika hataki kujua familia imeshindaje wala kuna matatizo gani.
Unakuta mke anamatatizo kibao lakin wa kukaa kuzungumza nae hakuna,hapo si lazima apate hasira?
 
Mwanamke wa hivyo sijamuona labda jimama linaloishi na marioo ila kwa wanaume yapo, tatizo kidogo tu mke anataka hela atume kwao yaani kuoa ukoo maskini ni balaa la kujitakia
Unakuwa umeowa ukoo wote!
Yaani maandiko yanasema mwanamke ni kiumbe dhaifu
 
Wote wawili mwanaume na mwanamke wanachangia kuharibu ndoa yao. Hii ninaweza kuieleza kwa kutoelewa kwao ama kuelewa na kupuuzia falsafa ya KUACHA NA KUAMBATANA.
Kabla ya ndoa kila mmoja anakua na tabia na mienendo,mila na desturi,marafiki na vitu anavyovipenda na KUAMBATANA navyo.Sasa unapoingia katika ndoa sharti kila mmoja AACHE bahadhi ya vitu/watu/tabia zisizohitajika katika ndoa kisha AAMBATANE na vitu/mwenza/tabia zenye kuboresha ndoa.Jambo hili limekua kitanzi cha ndoa nyingi kwa zama hizi.
 
Wakunyeyekewa ni mungu.Mume anaheshimiwa.

Jibu langu ni mwanaume.
Sababu, wanaume wengi hawatumizi majukumu yao,wanaona wakishaoa wamemaliza km ni mke atamkuta tuhapo nyumbani,so hajiongezi kwa chochote.
Udhaifu wa mwanamke hauwezi kwisha, maana ni andiko.
Hakuna mwanamke asiye dhaifu, labda shemale
 
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba wanaume wengi huingia kwenye ndoa bila ya kutarajia, wakati wanawake ni moja ya mipango yao ya maisha tangu wakiwa washichana wadogo. Kwenye ndoa wanawake wanakuwa na mipango tofauti sana na wanaume.

Ni nani hasa kati ya mwanamke na mwanaume ambaye anasababisha hadi ndoa ionekane ni taasisi yenye dhahama nyingi kuliko raha?

PICHA KWANZA!
 
hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho.
 
Ndoa za Siku hiz tunavumiliana tuu Tukichokana TALAKA zinatolewaa ndoa zilikuwa zile za Enzi za Babu na Bibi wazaa wazaz wetu
 
Back
Top Bottom