Ndoa za zamani watu walikua wanaoana toka sehemu moja au kijiji kimoja.Na ili uoe/kuolewa kulikua na uchunguzi unafanywa kabla na baada ya kujiridhisha na tabia za waoanaji ndipo ndoa hufungwa. Siku hizi watu wanaoana hata bila kuchunguzana walio wengi wanaangalia vigezo kama mali na urembo. Kwa bahati mbaya mambo haya yamewatawala sana vijana na wanajikuta wameacha kuangalia mambo ya msingi.
Nakumbuka kuna kijana flani alituletea binti na akasema anaoa soon. Tulimuuliza kijana yule kwamba je ameshajiridhisha na tabia ya huyo anaetaka kumuoa basi bila kujiuliza kwanini tuliuliza vile yeye akatujibu na kusema huyo binti yuko safi sana. Hatukuacha kuendelea kumdadisi , tukamuuliza tena je ikitokea baada ya ndoa kibarua kikaota nyasi unafikiri huyo binti ataendelea kuishi na wewe, akajibu tena bila kufikiri na kusema yuko bomba sana.
Basi ndoa ile ilifungwa na sherehe ilikua nzuri mno. Baada ya miezi 2 yule dada alianza maisha ya kutembea nje ya ndoa na akawa jeuri kupita kiasi. Ndoa ile ilikua na migogoro mingi sana kumbe yule mdada alikua hajatulia bali wakati ule alivaa ngozi ya kondoo ili aolewe.
Mitandao inachangia kwa kiasi kidogo sana kwani wanaoitumia ni wachache mno ukilinganisha na wasioijua au wasiotumia. Ili kupunguza migogoro kwenye ndoa nafikiri itakua vema tukijikita ktk kutafuta vyanzo vya migogoro hiyo. Kuna sababu zingine kama kukosa uaminifu kwa wababa ambalo limekua jambo la kawaida sana.