Mimi ni Mama wa watoto wawili, nimeolewa na ndoa yangu ina miaka mitano sasa, tatizo nikuwa sina mapenzi na mume wangu na sijui hata nifanye nini. Mume wangu ni mwanaume mzuri, ananipenda na anajali familia yangu pamoja na wanangu, kiandani yuko vizuri anauwezo wa kuniridhisha ingawa siridhiki kwani sipendi aniguse, sitamani kabisa kufanya mapenzi na mume wangu nafanya kama kazi na kuna wakati mwingine natamani hata achepuke ili kuwa na mwanamke mwingine ambaye ananisaidia majukumu ya tendo la ndoa na mimi nayeye tubaki kama wazazi tu.
Kabla ya kukutana na mume wangu nilikua na mpenzi wangu ambaye tulipendana sana na tulishatambulishana mpaka kwa ndugu walikua wanamjua ingawa ilikua badi haijawa rasmi. Lakini kabla ya kufunga ndoa alichepuka, nilimfumania baada ya kupigiwa simu na mchepuko wake kuwa una mimba yake, nilimuuliza hakukataa, tuligombana sana kwa hasira nikamtukana na hapo ndipo kibao kilinigeukia kwania liniambia nimekosea adabu hivyo akanipa muda wa kujifikiria kama nafaa kuwa mke wake au la. Tulitengana kama mwaka hivi kila nikimuomba msamaha alikua anakataa mpaka nikachoka.
Ndipo nilikutana na huyu mume wangu na kwakua alikua siriasi na ndoa hata hatukuchukua muda tukapanga na kuoana. Aliposikia nakaribia kuolewa alikuja kuniomba msamaha lakini nilikataa katakata ingawa bado nilikua nampenda, niliolewa nayeye alioa mwanamke mwingine si yule ambaye alikua kashamzalisha. Nilijaribu kumsahau kwa muda lakini ndoa yangu ikiwa na miaka mitatu alikuja na kuniambia kuwa amenikumbuka, hawezi kuishi bila mimi ananipenda na mimi ndiyo mwanamke wa maisha yake na kuchepuka ilikua ni shetani tu.
Kwakua nilikua kwenye ndoa sikutaka kumpa nafasi kwani mume wangu ni mtu mstaraabu, hajwahi nikosea na ananipa kila kitu. lakini kaka kadri siku zinavyoenda nahisi nachanganyikiwa, nashindwa kabisa kuendelea na maisha kwani ananitafuta, anaweza kukaa miwezi sita hajanitafuta lakini akinitafuta najikuta natamani hata kumuona, natamani kurudiana naye, sijawahi msaliti mume wangu lakini nilichat na X wangu najikuta najisikia vizuri kuliko kufanmya mapenzi na mume wangu, nimechanganyikiwa Kaka sina hisia na mume wangu kabisa naomba msaada wako nifanye nini? Kama utapost tafadhali ficha jina langu.
Sent using
Jamii Forums mobile app