Pasiwepo ndoa hizo kwa sababu mizinguo.jambo la msingi mtu asioneshe kama anamtaka fulani kindoa kwani hilo litamfanya anaetakiwa kujipamba vizuri kitabia na kuigiza ili amvute yule mtu.
Mwanaume winda kimya kimya utapata mnyama sahihi umtakae,usiwe na kelele kutafuta mchumba.eti mtu unakaa na mwanamke na mwanamke anajua kwamba hapa nachunguzwa ili kama nafaa niolewe.hivi mwanamke gani ataonesha tabia chafu hapo? Atakuigizia mpaka ukome na ukiingia kingi kuoa umekwisha.
Ndoa anaeweza kuidumisha ni mwanamke.
Mwanamke akiwa malaya kwa mumewe na kuwa mtundu na asiwe kidomodomo mwanaume hatakubali kumuacha mwanamke huyo.
Mwanaume akiwa mstaarabu asiyenuna nuna na kuwa mkali basi mwanamke atafurahi.
Ndoa ili idumu kila mwanandoa anatakiwa atathmini ni tabia zipi ambazo mara nyingi huvunja mahusiano basi waziepuke.
Ndoa haitaki maigizo ishini nyinyi kama nyinyi.
Mimi na mke wangu tunaweza kukaa ndani siku nzima humo tunapiga stori tu za hapa na pale na kucheka tunasahau hasa kama mtu na mumewe tunakuwa marafiki,kwa mke wangu nakuwa huru kupiga kila aina ya stori.
Namchokoza makusudi na kumsumbua.kuna wakati mwanamke sio atakumbuka mazuri na utulivu wako,bali wakati ungine hukumbuka vituko na viuchokozi wako
Habari za kupiga stori za kupendana tu kila mda uongo bwana.ndoa inatakiwa asilimia 70 ni urafiki na zinazobaki ni mtu na mkewe.
Mume kumsaidia mke kazi huo ni urafiki ukivaa vazi la mume utakaaje jikoni bwana,ila ukivaa vazi la urafiki utakaa nae jikoni na mkasaidiana kupika.ila tunaona watu na marafiki zao wanavyosaidiana,kwa nini usimsaidie mkeo huyo ni kama rafiki na zaidi.
Ndoa haina kuiga bongo muvi taniana na mkeo kama washkaji hivi lazima muwe na kibwagizo chenu sio kama baba na mtoto wake hakuna kucheka.
Wanaume tuwe tunatabia ya japokuandaa vispeech mara moja moja ukimsifia mkeo juu ya jambo fulani zuri alilofanya kwako ili aone kuwa unamrespect aisee.
Ndoa haitaki wivu wa kifala wa kuchunguzana simu.
Wife namuachia simu anasoma meseji za magroup yangu na mimi ananiachia simu nasoma za magroup yake na ananiachia (sio lazima uige)
Kiufupi ndoa hasa kwa zama zetu ona kama yule ni rafiki yako.
Watu wanafunga ndoa bila kujuana vizuri kitabia.Hii inatokana na baadhi yao kuficha tabia zao halisi wakati wa uchumba na wakishaingia kwenye ndoa ndo huonyesha tabia zao halisi.Ushauri kuwe na ndoa za mkataba hili mambo yakienda ndivyo sivyo kila mtu achukue hamsini zake.Uwekwe utaratibu jinsi watoto wataishije mara mkataba utakapoisha.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Sent using
Jamii Forums mobile app