Ndoa: Mapenzi, pesa na ushirikina

westgate

JF-Expert Member
Sep 23, 2013
278
275
Kumekuwa na visa vingi vinavyotokea ndani ya ndoa kupelekea vijana wengi hasa wanaoanza maisha kuwa waoga kuingia katika taasisi hii ya ndoa!

Wanawake nao wanalalamika wanaume wa siku hizi sio waoaji na mara nyingi wanatafuta kutimiza haja zao za mapenzi!

Ni vyema tukatumia jukwaa hili kuangalia changamoto mbalimbali ndani ya ndoa na jinsi ya kuweza kukabiliana nazo ili kuwatoa uoga vijana wanaotarajia kuingia kwenye maisha mapya.

Visa mbalimbali nilivyowahi kutokea ni mauaji hasa ya waume ili mwanamke aweze kurithi mali zinazoachwa.

Vingine ni usaliti ndani ya ndoa, kufichiana siri na mengine mengi.
 
ndoa ndoa ndoa
kitu kigumu sana kukielewa na kila ndoa inachangamoto zake
 
Kwenye ndoa usiwe na wivu,uwe mvumilivu,uwe na pesa na uwe na kazi mengine yote yana tatulika
 
Ndoa ni wewe mwenyewe ukitaka iwe chungu itakua, ukitaka iwe tamu itakua, ukitaka iwe moto itakua, ukitaka ya furaha itakua.....
Maneno ya watu sio ya kuogopa kuwa ndoa ni mbaya ila pia sio ya kuyapuuzia
Na kumbuka unaeingia nae ndoani ni binadamu sio malaika ana mapungufu yake kama wewe ulivo na mapungufu yako
 
Back
Top Bottom